TRA YATAKIWA KUFANYA HAYA NA BARAZA LA WAWAKILISHI.

Na Is Haka  Muhammed Pemba. 

KAMATI ya Bajeti ya Baraza la Wawakilishi imetaka Mamlaka ya Mapato Tanzania(TRA) kuharakisha mpango wao mkakati wa kusaidia wafanyabiashara wa kisiwani Pemba kuweza kuingiza bidhaa zao moja kwa moja kisiwani Pemba ili kupunguza gharama za bei za bidhaa kisiwani hapa na kuwaondoshea mzigo mkubwa wananchi.

Kauli ya Kamati hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Kamati hiyo Abdalla Hussein Kombo wakati ilipofanya ziara katika ofisi za TRA Mkoa wa Kikodi Pemba ikiwa katika kazi zake za kawaida za kamati za kufuatilia utekelezaji wa kazi za wizara ya fedha na taasisi zake.

Amesema gharama za bidhaa mbali mbali ikiwemo chakula zimekuwa za juu sana kisiwani Pemba kutokana na wafanyabiashara kutoingiza moja kwa moja bidhaa hizo kisiwani hapa na hatimae mzigo wa gharama hizo kuwaelemea wananchi.

Awali akiwasilisha   taarifa ya utekelezaji wa kazi za TRA Mkoa wa Kikodi Pemba Naibu Waziri (OR) Fedha na Mipango Zanzibar Ali Suleiman Ameir amesema kuwa ufinyu katika bandari za  Mkoani na Wete  pamoja na uhaba wa nyenzo za kushushia mizigo kunapelekea waingizaji wengi wa mizigo kutotumia bandari hizo.



Comments

Popular posts from this blog

BARABARA 19 KUJENGWA KWA KIWANGO CHA LAMI PEMBA KUKAMILIKA DISEMBA 2024.

WAZAZI ZIDISHENI KUFUATILIA NYENENDO ZA WATOTO HUSUSAN NI VIJANA .

UONGOZI WA WILAYA CHAKE CHAKE KFHI WAPONGEZA JUHUDI