Wananchi Msipuuze Chukueni Tahadhari Ugonjwa Bado Upo.
Na AMINA AHMED MOH’D- PEMBA
WANANACHI wa Maeneo mbali mbali Kisiwani Pemba Wameshauriwa kuendelea Kuchukua Tahadhari dhidi ya Ugonjwa Wa Malaria kwa kuendekea kulala jatika vyandarua vilivyotiwa dawa, kufanya vipimo vya mara kwa mara juu ya Ugonjwa huo wanapofika Hospitali, Sambamba na kuacha kutymiandawa bila mpangilio wanapobaini dalili za Ugonjwa.
Ushauri huo umetolewa na Muhamasishaji Kazi za Malaria Pemba Dk Yussuf Ali Juma Alipokuwa Akizungumza na wananchi wa kisiwani Pemba kupitia Waandishi wa Habari wa Vyombo mbali mbali katika Mkutano Maalum wa kutoa tathimini ya Ufuatailiaji na Mwenendo wa Ugonjwa wa Malaria kwa Mwaka 2020 2022 Uliofanyika katika Ukumbi wa Kitengo Cha Malaria Wete Mkoa Wa Kaskazini Pemba.
Amesema Baadhi ya Wananchi wamekuwa wakipuuza kulala katika Vyadarua vilivyowekwa Dawa, Kupima na kuweza kujua hali za Afya zao Pamoja na kutumia Dawa bila Mpangilio wanapobaini Dalili za Ugonjwa wa Malaria jambo ambalo Linapelekea kuwepo kwa kesi za Malaria katika Baadhi ya Maeneo kisiwani Pemba.
"Ugonjwa Wa Malaria Bado Upo Kupitia Vyombo vya habari Niwaase Wananchi Maeneo Mbali mbali Kuchukua Tahadhari kwanza kulala katika vyandarua vilivyotiwa Dawa,wasivifungie kwenye Makabati tu, Kupima Afya zao wanapofika katika hospitali na vituo vya Afya na waache kutumia dawa kiholela mtu anapobaini ana dalili za Malaria asinunue tu Dawa bila kuoata maelekezo ya Dakatari Licha Ya Asilimia iliyopo lakini Bado Ugonjwa Haujamaliza.
Aidha Yussuf Amesema kitengo cha Malaria Pemba kinaendelea na Mapambano dhidi ya kumaliza Ugonjwa huo kwa kufanya uchungzi Wa Mbu wa Malaria kupitia mitego maalum , pamoja na kuendelea kutoa Vyandarua kwa Mama wajawazito, watoto,na Makundi mengine lengo ni kuweza kuwakinga Na Ugonjwa Huo .
"Mikakati yetu ni kumaliza Malaria 2023 tunawafikia Wagonjwa, kitengo kinafanya Uchunguzi kwa kubaka Mbu na kuwafanyia uchunguzi ili kuweza kujua bado wapo Mbu wanaosababisha Malaria lakini pia tunaendelea na huu mpango endelevu wa kutoa vyandarua vyenye dawa Kwa Mama wajawazito na watoto ili kuona wanaendelea kuchukua Tahadhari.
Akizungumza Katika Mkutanao huo Afisa Ufuatiliaji wa Wagonjwa wa Malaria Pemba Said Massoud Mbarouk Amewataka waandishi kufikisha ujumbe kwa jamii ili iweze kuchukua Tahadhari juu ya Ugonjwa huu kwani kwa sasa wananchi waliowengi wamepunguza kasi katika kuendeleza Mapambano haya ya Kudhibiti na kumaliza Malaria Zanzibar.
SAID MASSOUD MBAROUK - AFISA UFUATILIAJI WAGONJWA MALARIA PEMBA
Kwa Upande wake Afisa Uchunguzi Ugonjwa wa Malaria Pemba Bimkubwa Khamis Kombo Amesema kitengo hicho cha Malaria kitaendelea kutoa Huduma kwa Wananchi Katika Maeneno Mbali mbali kwa Kupima na kuchunguza Wagonjwa wanaofika katika hospitali na vituo vya Afya sabamba na kufuatilia wagonjwa nyumba hadi nyumba,watakaobainika kuwa na dalili za Ugonjwa huo.
Aidha kwa Upande wake Fatma Khamis Haji Mhamasishaji Kutoka kitengo Cha Malaria Pemba Amesema kuwa Huduma za upimaji wa malaria zinatolewa bure Hivyo ni vyema wananchi kuendelea kuitumia fursa hiyo kufanya vipimo na watakapobainika kuanza kutumia tiba ya Malaria.
Mkutano huo wa siku Moja umeandaliwa na ZAMEK kwa waandishi wa Habari ulikiwa na lengo la kueleza mikakati iliyofikiwa katika kuendeleza na Kupambana na Ugonjwa Wa Malaria Pemba.
Mwisho
Comments
Post a Comment