Tume ya kurekebisha Sheria Yaahidi Mashirikiano kurekebisha Sheria



NA ASIA MWALIM - UNGUJA 

TUME ya Kurekebisha sheria Zanzibar, imesema itashirikisha na Tume ya Sheria Jamhuri ya Muungano ya Tanzania katika kuzifanyia mapitio sheria zisizo zingatia jinsia katika ushiriki wa wanawake katika uongozi na ngazi za maamuzi . 

Katibu wa Tume ya Kurekebisha sheria Zanzibar, Mussa Kombo Bakari, aliyasema hayo wakati wa semina ya majadiliano ya sheria yaliandaliwa na shirika la Women in Law and Development Africa (WILDAF), huko Beach Resort Mazizini Unguja. 


Alisema tume hizo kwa pamoja zitazingatia suala la wanawake wakati wa kufanya mapitio ya sheria ya vyama vya siasa na sheria ya taifa ya uchaguzi, ili kuona kundi hilo linakua mstari wa mbele. 


Aidha alisema lengo la semina hiyo ni kujenga uwezo wanasheria ili wapate kuwakisi masuala ya wanawake wakati wa kuzipitia sheria, hatimae kutoa miongozo mizuri kwa makundi yote. 


Katibu alifahamisha kuwa, sheria za awali zilishindwa kuzingatia jinsia, ni muhimu kujenga uelewa kwa wanasheria ili kuweka uhamasishaji kwenye suala la sheria mbalimbali zinazofanyiwa mapitio. 


Aidha alieleza kuwa, hatua hiyo itasaidia kunyanyua makundi yote hasa wanawake kupata fursa za uongozi, ambapo kihistoria kundi hilo limekua nyuma katika harakati za maendeleo ya  kisiasa, uchumi na kijamii. 


Katibu Mussa, alisema kikao hicho kimenufaisha kwa namna kubwa na kufanikiwa kuona mikataba ya kitaifa, na sheria zote mbili jinsi zilivyotambua na kuweka umuhimu kwa kuzingatia masula ya Jinsia katika kuleta maendeleo. 


Nae Mkurugenzi wa Shirika la Wanawake katika sheria na maendeleo barani Afrika (WILDAF) Anna Kulaya, alisema sheria nyingi zilipoanzishwa hazikua na muitikio wa kijinsia kutokana na historia iliyokuwa awali.


Alisema tume hizo ni wadau wakubwa wa sheria,  wameamua kufanya kazi kwa pamoja kuona sheria zinazokuja zinazingatia masuala ya jinsia, katika kulinda na kutoa fursa za kupata rasilimali za nchi kwa makundi yote. 


Alisema baadhi ya vipengele kwenye sheria hizo zinamnyima mwanamke kupata fursa ya urithi na umiliki wa ardhi, kutoa ubaguzi kwa wanawake, hivyo wadau wanapaswa kuwasilisha mapendekezo namna ya kuongeza ushiriki wa wanawake katika uongozi na ngazi za maamuzi. 


Mohammed Hassan Ali mmoja kati ya washiriki wa mkutano huo alisema, sheria ya vyama vya siasa zimewachukilia wanawake kwa kiwango kidogo, kuna ulazima kwa wanasheria kuhakikisha sheria zinazingatia jinsia kila kipengele. 


Aidha alisema, amegundua kuwa sheria ya uchaguzi haijakidhi matakwa ya kimataifa, wabunge wanapata changamoto katika utendaji wao na kukosa haki zao kwa mujibu wa sheria. 


Thumaiya Awadh, Mwanasheria alieshiriki mjadala huo alisema, kiuhalisia wanawake ushiriki wao ni mdogo, ni vyema kuondoa ubaguzi kuanzia kwenye sheria ili kupata wepesi katika masuala ya uongozi na maeneo mengine ya maendeleo.

Mwisho 

Comments

Popular posts from this blog

BARABARA 19 KUJENGWA KWA KIWANGO CHA LAMI PEMBA KUKAMILIKA DISEMBA 2024.

WAZAZI ZIDISHENI KUFUATILIA NYENENDO ZA WATOTO HUSUSAN NI VIJANA .

UONGOZI WA WILAYA CHAKE CHAKE KFHI WAPONGEZA JUHUDI