UONGOZI WA SHEHIA WAAHIDI MASHIRIKIANO KWA WASAIDIZI WA SHERIA PEMBA.
NA AMINA AHMED MOH’D - PEMBA.
UONGOZI wa Shehia ya Wawi wilaya ya Chake Chake Mkoa wa kusini Pemba umesema Utatoa mashirikiano na wasaidizi wa Sheria katika kutatua changamoto mbali mbali za jamii zikiwemo kero na udhalilishaji wa kijinsia ambazo kwa muda mrefu zilikuwa zikikosa ufumbuzi na kukosa msaada kutokana na kukosa wasaidizi hao.
Aliyasema hayo Sheha wa Shehia ya Wawi Sharifa Ramadhan Abdalla Alipokuwa akifungua Mkutano Maalum wa kutoa Elimu na Kujitambulisha kwa uongozi wa wa shehia hiyo Msaidizi wa sheria Kutoka Jumuia ya Wasaidizi wa Sheria Chake Chake Pemba.
Alisema Chamgamoto mbali mbali ikiwemo kero ambazo zinaendelea zinajitokeza katika vijiji vilivyomo ndani ya shehia hiyo hukosa Msaada wa kisheria kutokana na kukosekana ufumbuzi na kupelekea kuishia kienyeji bila kupatiwa ufumbuzi , hivyo ujio wa wasaidizi hao kutapelekea kupatikana suluhu ya Matukio mbali mbali yanayojitokeza.
"Ujio huu wa Msaidizi wa sheria Katika Shehia hii utakuwa msaada mkubwa kwa wananchi katika kutatua baadhi ya kesi kwani zipo kesi mbali mbali ambazo huishia kienyeji ni kutokana na kukosa msaada wa kisheria naahidi tutashirikiana katika suala hili na kufanya kazi kwa pamoja katika kuondoa kero za jamii.
Akizungumza katika Mkutano huo Afisa kutoka jumuia ya wasaidizi wa sheria Chake Chake ambae ni msaidizi mpya wa sheria katika shehia ya Wawi Haji Nassor Muhamed Alisema kuwa Kwa kushirikiana na Uongozi wa shehia Msaada wa kisheria utawafikia wananchi katika mawneo mbali mbali kwa kuandaa vikao na kutia elimu juu ya mambo mbali mbali .
Aidha Afisa huyo alisema kuwa ataendelea kusimamia vyema na kufuatilia masuala hayo ya usaidizi wa kisheria ili kuona haki zinapatikana kwa mujibu wa sheria.
Nao baadhi ya washiriki wa Mkutano huo akiwemo Mjumbe wa sheha wa shehia hiyo katika kijiji cha Wawi Mtemani Nassor Rashid aliwataka wananchi Wa Wawi kutodharau Viongozi wa Shehia wanapofikwa na changamoto mbali mbali na kukimbilia vyombo vikubwa kabla kupitia katika uongozi wa shehia ili kuepusha Mivutano isiyoya lazima.
Katika Mkutano huo Elimu ya msaada wa kisheria juu ya Mambo ya udhalilishaji, Haki za mtoto, Rushwa Muhali, Namna ya kutoa ushahidi, pamoja na Masuali mbali mbali ambayo yaliolizwa na washiriki qa Mkutano huo yalitolewa ufafanuzi na Afisa huyo kutoka jumuia ya wasaidizi wa Sheria.
Mwisho.
Comments
Post a Comment