Waziti Leila Anena haya kwa wasimamizi wa miradi
NA FATMA SLEIMAN ABRAHMAN PEMBA.
WAZIRI wa Elimu na Mafunzo ya Amali Lela Mohamed Mussa amewataka watendaji wa Wizara ya Elimu kutobweteka kwa sifa Walizozipata kutokana na usimamizi wa miradi ya Maendeleo na badala yake wajiandae kusimamia kwa umakini zaidi utekelezaji wa miradi katika mwaka huu wa 2023.
Waziri Lela ameyasema hayo katika kikao maalumu kilichowashirikisha watendaji wa Wizara ya Elimu, kilichofanyika katika Ukumbi wa Afisa Mdhamini Wizara ya Elimu Chake Chake Pemba.
Amesema Serika ya Mapinduzi ya Zanzibar inayoongozwa na Rais Dkt. Hussein Ali Mwinyi imeweka kipaombele katika swala la Elimu na kuwekeza kiwango kikubwa cha fedha hivyo imeitaka Wizara hio kusimamia ujenzi wa madarasa zaid ya 2000 katika mwaka 2023.
Aidha amesema katika utekelezaji wa Miradi hiyo Wizara itatoa kipaombele katika sehemu ambazo watoto wanasoma katika mazingira magumu zaidi.
Nae Katibu Mkuu Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Nd. Khamis Abdullah Said amewataka maafisa Elimu Wilaya na Mikoa kusimamia upatikanaji wa matokeo bora ya Wanafunzi ili kuitendea haki Miradi inayojengwa na Serikali katika kuimarisha sekta ya Elimu.
Aidha amesema Wizara ya Elimu inatarajia kutoa Vishkwambi kwa Maafisa Elimu Mikoa na Wilaya, Wlimu Wakuu na Walimu wa kawaida kwa idadi ya Wanafunzi hivyo amewataka Walimu kujifunza matumizi ya Teknojia.
Wakati huo huo amewataka Watendaji wa Wizara kufanya maamuzi kwa kuzingatia kanuni na sheria ili waweze kutoa huduma zilizotukuka.
Kwa Upande wake Afisa Mdhamini Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Mwalimu Mohammad Nassor Salim ameipongeza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuwekeza fedha nyingi katika miradi ya Elimu hivyo amesema ataweka umakini zaidi katika kuaimamia utekelezaji wa Miradi hiyo.
Mwalimu Moh'd amesema licha ya Skuli ambazo zina mahitaji angependa pia kuona nguvu kubwa zinaelekezwa kwa Skuli ya Sekondary ya Fidel Castro na Chuo cha Ufundi Kengeja.
Mwisho
Comments
Post a Comment