MIAKA 59 YA MAPINDUZI NEEMA KWA WAZALISHAJI WA ASALI PEMBA.

Na AMINA AHMED MOH’D - Pemba 

WIZARA ya  Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar  imesema  itaendelea kutoa Mashirikiano  na   kuhakikisha inalipatia Soko la uhakika ndani na Nje ya Nchi   Zao  la Asali  inayozalishwa Kisiwani Pemba Pamoja na bidhaa zinazochakatwa kutokana na Zao hilo. 

 Akizungumza  na Wananchi  mara baada ya kufungua  Kituo cha  Usarifu  wa Mazao ya  Asali   Huko Limanda Pujini Wilaya ya Chake Chake Mkoa Wa Kusini Pemba  Waziri  Wa Biashara na Maendeleo ya Viwanda Zanzibar Omar Said Shaaban   Amesema kutokana na Ubora wa Asali  itakayozalishwa kisiwani Pemba   kuwa na ubora unaohitajika katika Soko la ndani na nje ya Nchi wizara hiyo itaitangaza Asali hiyo ili kupata Soko Zaidi na kuwakomboa wajasiriamali wanaozalisha Zao hilo.. 

"Kwa Sababu sisi ndio wenye Jukumu la kutafuta Masoko kwa bidhaa zinazozalishwa Ndani ya nchi na kuzitangaza huko Duniani tutatoa kila uahirikiano kuhakikisha kwamba Dunia  inatambua ubora na uhalisia wa  Asali inayizalishwa Zanzibar  Hapa Pujini."

 "Miundo mbinu Imara iliyowekwa katika kituo hichi nilichokifungua rasmi Leo  ndui  inayohitajika katika Soko la dunia kwa ubora wa uaandaaji mpka kukamilika kwake Naahidi kwenu wajasiriamali wa Zao la  Asali kulisimamia hili Suala la utafutaji wa soko nje ya Nchi kwajili ya bidhaa ya kuuza bidhaa zenu."Alisema. 


Aidha  Waziri Omar Amewataka  Wajasirimali wa Mazao ya Asali kutoa Mashirikiano katika kukitumia kituo hicho katika kuuza  na kupata Mafunzo ya Usarifu Bidhaa zitokanazo na Zao hilo , na Uzalishaji wa Nyuki,  ili zifikie katika kiwango kinachohitajika katika ushindani wa Soko.
 
 "Serikali Ya Mapinduzi ya Zanzibar imelipa Umuhimu Zao la Asali, Niwaombe Ndugu zangu Wajasiriamali mkitumie kituo hichi Kuuza bidhaa Zenu, kupata mafunzo ya kusarifu na kuzalisha Asali kwa mbinu za kisasa, lakini pia toeni Mashirikiano katika kuona kituo hichi kinakuwa endelevu  katika kuzalisha Asali Bora yenye kiwango.
 
 Akizungumza Katibu Mkuu Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais  Kazi Uchumi na Uwekezaji Maryam Juma Sadala  Alisema lengo l kujengwa kituo hicho Kisiwani Pemba ni kuwasaidia Wajasiriamali Kupata kituo maalum cha kuuza Asali yao Baada ya Mavuno pamoja na kupata  Elimu ya usarifu wa Bidhaa mbali mbali zinazotokana na zao la Asali,na Uzalishaji wa Nyuki kwa Njia za kisasa. 


 Aidha Katibu huyo Amewashukuru Wananchi  wa Kijiji cha Pujini na Wajasiriamali  kwa Mashirikiano waliyatoa  katika Kufanikisha ujenzi wa Kituo Hicho ambapo amewataka kuwa walinzi katika kutimiza Maelengo  yaliokusudiwa. 


Kwa upande wake  Mkuu Wa Mkoa wa Kusini Pemba Mattar Zahor Massoud Ameishukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar  Kwa kuyafanyia kazi Maoni yaliotolewa na wajasiriamali wa Mazao ya Asali kuwajengea kituo hicho  ambapo Alisema  kitasaidia  kuitambulisha Asali inayozalishwa Kisiwani Pemba pamoja na kupata soko la uhakika. 

Akitoa Shukurani kwa Niaba ya Wajasirimali wa Mazao ya Asali na Wafuga Nyuki Pemba Nassor Suleiman Nassor  wamesema kuzinduliwa kwa kituo hicho ni chachu ya Maendeleo  na Hazina  itakayisaidia  kukuza Mazao hayo.

"Tunamshukuru  sana Rais wa Zanzibar  kwa kutusaidia kupata kituo hichi  kwetu ni furaha sana kutasaidia kuongeza uzalishaji wa Asali na Mazao yatokanayo na Mazao  hayo. 
 
 Aidha  wafanya Biashara hao waemuomba Waziri huyo kuwafukisha kilio chao  kupatiwa  vifaa na vitendea kazi bure kwa hatua ya awali kutokana na hali Ngumu ya kiuchumi iliyopo kwa wafuga nyuki kisiwani Pemba. 

Ufunguzi wa Kituo ni Shamra Shamra Za kuelekea kutimia kwa Miaka 59 ya  Mapinduzi ya Zanzibar, ambapo kituo hicho cha Usarifu wa Mazao ya Asali Pujini  Limanda Wilaya ya Chake Chake Kimegharimu jumla ya Shilingi            Milioni mia sita na Arobaini na moja na Themanini  na tano hadi kukamilikaika ikiwa ni pamoja na   ujenzi ununuzi uwekeji wa vifaa, ununuzi wa Piki piki, pamoja na ununuzi  wa vitendea kazi, ambapo  kitatumika kwajili ya kutoa mafunzo, kuuzabidhaa zitokanazo na Mazao hayo, kuchakata pamoja na kuto Elimu juu ya ufugaji wa Nyuki kwa Wajasirimali kikiwa Chini ya Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais kazi Uchumi na Uwekezaji ambapo ujenzi wa kituo hicho ulianza Mnamo Mwezi 3/ mwaka 2022 Na kuzinduliwa Rasmi leo. 

Mwisho

 


Comments

Popular posts from this blog

BARABARA 19 KUJENGWA KWA KIWANGO CHA LAMI PEMBA KUKAMILIKA DISEMBA 2024.

WAZAZI ZIDISHENI KUFUATILIA NYENENDO ZA WATOTO HUSUSAN NI VIJANA .

UONGOZI WA WILAYA CHAKE CHAKE KFHI WAPONGEZA JUHUDI