Waziri wa Uchumi wa Buluu Zanzibar Aahidi Mazuri haya
Na Fatma Suleiman - Pemba.
WAZIRI wa Uchumi wa Buluu na Uvuvi Suleiman Masoud Makame amesema, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar inaendelea kuwawekea mazingira mazuri wafanyakazi kwa kujenga Ofisi mbali mbali, ili kuongeza ufanisi katika utendaji wao wa kazi.
Ameyasema hayo wakati akifungua jengo la Ofisi ya Zimamoto na Uokozi (KZU) pamoja na uwekaji wa jiwe la msingi katika Ofisi ya KMKM Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba, ikiwa ni katika shamra shamra za kuadhimisha miaka 59 ya Mapinduzi Zanzibar.
Amesema kuwa, lengo la Serikali ni kuhakikisha inawawekea mazingira mazuri wafanyakazi wake, ili kuimarisha utendaji wa kazi na kuongeza ufanisi.
Waziri huyo alieleza kuwa, kumalizika kwa majengo hayo anaamini kwamba kutaamsha ari kwa wafanyakazi katika kuendelea kutekeleza majukumu yao kwa maslahi ya Taifa.
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa Kaskazini Pemba Salama Mbarouk Khatib amesema, Serikali imejipanga kuhakikisha inaimarisha maeneo ya kazi, ili wafanyekazi kwa moyo wa imani katika kuleta maendeleo endelevu.
Akitoa maelezo ya kitaalamu Naibu Katibu mkuu ofisi ya raisi tawala za mikoa serekali za mitaa na idara maalum za Smz Mikidadi Mbarouk Mzee amesema kukamilika kwa miradi hio kutapelekea kuongezeka ufanisi katika kazi zao kwani imekuja kuondoa changamoto zilizokuepo
Comments
Post a Comment