WADAU NA SERIKALI TUSHIKENI MIKONO KUTIMIZA MALENGO YETU
Aliyasema hayo katibu wa kikundi hicho Time Juma Said Alipokuwa akizungumza na habari hizi huko katika ofisi za kikundi hicho wilaya Micheweni Shehia ya Majenzi ambapo kwa sasa wanaendelea kufanya shughuli zao za Ususi na Ufumaji.
Alisema kutokana na wanakikundi hao asilimia 60 kuwa na ulemavu wa uoni Suala la kukosa ofisi hupeekea kusua sua kufanya shuhguli zao na wanapofanya hupelekea kubaki nazo nyumbani jambo ambalo linarudisha nyuma Juhudi zao za kutaka kujikomboa kiuchumi.
"Tunaiomba Serikali wadau pia Watusaidie kumalizia ujenzi wa ofisi yetu sisi wanakikundi cha tupendane ni Wajasiriamali ambao tumeamua kujikomboa kuondoshea mzigo wa utegemezi Serikali, Kwa kufanya shuguhli za kujipatia maendeleo lakini Changamoto kubwa kwa sasa imekuwa ni ofisi inayotambulika.
Aidha Katibu huyo Amesema kwa sasa tayari Ujenzi huo umefika katika hatua kubwa ambapo wamepata baadhi ya vifaa ambavyo vitasaidia kusegeza mbele ujenzi huo lakini kutokana na kukosa uwezo wamelazimika vifaa hivyo kuviwka ndani ili kusubiri msaada kutoka kwa wahisani pamoja na Serikali.
"Nikiwa kama Katibu nimejitahidi kuomba Msaada juu ya hili nashirikiana na Wenzangu kila pahali kuona kwamba Tunapata Ofisi yetu lakini bado hatujafanikiwa kumaliza licha ya kupata msaada wa baadhi ya vitu tunaomba Serikali izidi kutusaidia, Serikali izidi kutuangalia bado hatujafikia malengo tuliojiwekea kama wajasirimali wenye ulemavu changamoto ni ofisi.
Miongoni Mwa wanankikundi hicho Ambae ni mwenye Ulemavu wa Macho Mpeta Seif Alisema kuwa kutokana na kukosa Jengo la uhakika hulazimika kusitiaha Shuguhli zao za ufumaji wa Mashuka ambayo kwa Asilimia kubwa yamekuwa yakiwapatia faida kuliko bidhaa nyengine wanazozalisha.
"Eneo tulilopo kwa sasa sio letu tumejiweka tu kwa mtu tunafanya shughuli zaidi hizi za ususi tu kwa sababu ni enwo finyu ambalo charahani zetu haziwezi kukaa kwaio zinaharibika malengo hayafikiwi ya kujikomboa.
Akizungumiza Juu ya sula hilo Afisa Kutoka Baraza la watu wenye Ulemavu wilaya ya Micheweni Ali Hassan Ali Alisema kuwa Baraza hilo kwa kushirikian na taasisi mbali mbali litaendelea kushighulikia suala hilo ili kuona linapata ufumbuzi na kuwasaidia kuondokana na chagamoto hiyo.
Kikindi hicho cha Tupendane kina jumla ya wanachama 11 Ambao Sita kati ya hao ni wanawake weye ulemavu wa Macho Ambapo kutokana na kukosa ofisi rasmi kunapelekea kurudisha nyuma harakati zao wanazofanya za ususi na Ushoni wa Mashuka ambayo hutumia bidhaa hizo kwa ajili ya kujiendeleza kimaisha.
Mwisho.
Comments
Post a Comment