Taasisi Zapaza sauti kuelekea sikiu 16 za kupinga udhalilishaji.
Na Amina Ahmed Moh’d. TAASISI zinazoshughulika na kupinga vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia kwa wanawake na watoto kisiwani pemba zimeiomba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuimarisha vyema mfumo wa upatikanaji wa takwimu za matukio ya udhalilishaji wa kijinsia ili kuonesha jamii maendeleo yaliofikiwa katika mapambano dhidi ya vitendo hivyo. Akizungumza katika Mkutano maalum na waandishi wa habari wa vyombo mbai mbali uliofanyika katika ofisi za Tamwa Mkanjuni Chake Chake Pemba Mwenyekiti wa asasi za kiraia zinazoshughulika na Mambo ya udhalilishji Nassor Bilal Ali alisema kuimarika kwa mifumo hiyo kutaweza kuonesha jitihada zinazochukuliwa na serikali pamoja na Asasi hizo katika mapambano hayo ya kupinga vitendo hivyo. Aidha Wanaasasi hao waliwataka waandishi wa habari Kuzidisha mashirikiano katika kutoa taarifa za ufuatiliaji na uendeshwaji wa...