Suluhu ya Wadudu Nzi wanaothiri mazao hii hapa kutoka wizara ya kilimo.
Fatma Suleiman.
Wizara ya kilimo maliasili mifugo na uvuvi imedhamiria kuondoa kabisa changamoto ya wadudu Nzi wa matunda kwa wakulima Ili waweze kujiingizia kipato kulingana na ukulima wao na kuondokana na umaskini .
Akizungumza mara baada ya zoezi la ugawaji wa dawa hizo kwa wakulima Kaimu Afisa msaidizi wa mradi wa udhibiti wa wadudu Nzi waharibifu wa matunda Pemba Fatma Nassor Sharif amesema wizara inategemea kugawa mitego hiyo katika shehi ya zote za Pemba mara tu vitakapofika vifaa vyengine Ili kuondoa kabisa tatizo Hilo .
"Kutokana na Hawa nzi waharibifu wamekua wengi na wanaathiri matunda hivyo serekali kupitia wizara imeamua ni kuwaondoa kabisa na ndio tukaamua kutoa dawa hii kwa shehia zote kisiwani Pemba Ili kuwanusuru wakulima kujikwamua kiuchumi .alisema Fatma "
Sheha wa shehia ya ole shida khamis Othman amewanasihi wakulima wa matunda uongeza umakini pamoja kuzitumia dawa hizo ipasavyo Ili kutimiza lengo la serekali la kuhakikisha wadudu Nzi waharibifu wanaondoka kabisa
"Wakulima tunaomba muongeze umakini, dawa ambazo mumepewa mzifikishe mashambani na sio kuviweka ndani ya majumba , tuwe mfano kwa wakulima wengine Ili kutimiza lengo la serekali yetu na kupata manufaa . Alisema sheha shinda "
Naao baadhi ya wakulima wameishukuru serekali kupitia mradi wa kudhibiti wadudu Nzi wa matunda kwa kuwapatia dawa ambazo ndio kimbilio lao .
"Tunaishukuru serekali kupitia mradi huu wa kudhibiti nzi waharibifu wa matunda kwa kutupatia dawa tunaamini kwa mavuno yajayo yatakua na manufaa kwani awali ilikua tuna kilio kikubwa kutokana na wadudu hao kutuathiri . walisema wakulima hao"
Zaidi ya Mitego 2090 ya kuulia wadudu hao waharibifu wa matunda , imesambazwa kisiwani Pemba katika shehiya zote 36 za Wilaya yw Mkoani na shehiya 3 za Wilaya ya chake chake.
Mwisho
Comments
Post a Comment