Wizara ya kilimo yahidi neema wadudu wanaothiti mazao.
NA FATMA SLEIMAN.
WIZARA ya kilimo maliasili mifugo na uvuvi imedhamiria kuondoa changamoto ya wadudu Nzi wa matunda kwa wakulima Ili waweze kujiingizia kipato kulingana na ukulima wao na kuondokana na umaskini .
Akizungumza mara baada ya zoezi la ugawaji wa dawa hizo kwa wakulima Kaimu Afisa msaidizi wa mradi wa udhibiti wa wadudu Nzi waharibifu wa matunda Pemba Fatma Nassor Sharif amesema wizara inategemea kugawa mitego hiyo katika shehi ya zote za Pemba mara tu vitakapofika vifaa vyengine Ili kuondoa kabisa tatizo Hilo .
Sheha wa shehia ya ole amewanasihi wakulima wa matunda uongeza umakini pamoja kuzitumia dawa hizo ipasavyo Ili kutimiza lengo la serekali la kuhakikisha wadudu Nzi waharibifu wanaondoka kabisa .
Naao baadhi ya wakulima wameishukuru serekali kupitia mradi wa kudhibiti wadudu Nzi wa matunda kwa kuwapatia dawa ambazo ndio kimbilio lao .
Zaidi ya Mitego 2090 ya kuulia wadudu hao waharibifu wa matunda , imesambazwa kisiwani Pemba katika shehiya zote 36 za Wilaya yw Mkoani na shehiya 3 za Wilaya ya chake chake.
Mwisho
Comments
Post a Comment