MASAUNI AZUNGUMZA HAYA NA WANANCHI
NA OMAR HASSAN – UNGUJA
WAZIRI wa Mambo ya ndani ya Nchi Mhe. Hamad Yussuf Masauni amewataka Maafisa wa Jeshi la Polisi Kamisheni ya Zanzibar kuongeza nguvu katika kuzuia na kupambana na uhalifu ili Zanzibar iendelee kuwa salama kwa wananchi na wageni.
Akizungumza na Maafisa wa Jeshi hilo huko Makao Makuu ya Polisi Zanzibar amesema pamoja na kuwa takwimu zinaonesha kupungua kwa baadhi ya Makosa ya jinai bado zipo changamoto za kiuhalifu ambazo zinawasumbua wananchi
Kamishna wa Polisi Zanzibar Hamad Khamis Hamad ameeleza kuwa uchache na uchakafu wa magari pamoja na uchache wa Askari ni miongoni mwa changamoto zinazokwamisha utendaji wa Jeshi hilo.
Akitoa taarifa ya Uhalifu wa Makosa ya jinai kwa kipindi cha miezi tisa mwaka 2022 ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka 2021, Naibu Mkurugenzi wa Upelelezi wa Makosa ya Jinai, kamishna Msaidizi wa Polisi Zubeir Chembela amesema kuna upungufu wa matukio 64 ya Udhalilishaji wa Jinsia na watoto.
Mwisho
Comments
Post a Comment