Taasisi Zapaza sauti kuelekea sikiu 16 za kupinga udhalilishaji.
- Get link
- X
- Other Apps
Na Amina Ahmed Moh’d.
TAASISI zinazoshughulika na kupinga vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia kwa wanawake na watoto kisiwani pemba zimeiomba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuimarisha vyema mfumo wa upatikanaji wa takwimu za matukio ya udhalilishaji wa kijinsia ili kuonesha jamii maendeleo yaliofikiwa katika mapambano dhidi ya vitendo hivyo.
Akizungumza katika Mkutano maalum na waandishi wa habari wa vyombo mbai mbali uliofanyika katika ofisi za Tamwa Mkanjuni Chake Chake Pemba Mwenyekiti wa asasi za kiraia zinazoshughulika na Mambo ya udhalilishji Nassor Bilal Ali alisema kuimarika kwa mifumo hiyo kutaweza kuonesha jitihada zinazochukuliwa na serikali pamoja na Asasi hizo katika mapambano hayo ya kupinga vitendo hivyo.
Aidha Wanaasasi hao waliwataka waandishi wa habari Kuzidisha mashirikiano katika kutoa taarifa za ufuatiliaji na uendeshwaji wa kesi za udhalilishaji katika Mahakama mbali mbali .
Aidha asasi hizo zimempngeza rais wa Zanzibar Dk Hussein Ali Mwinyi kwa kuanzisha mahakam maalum za udhalilishaji ambapo wamesema maahakam hizo zimekuwa zikifanya kazi vyema katikaa kusimamioa kesi za
udhalilishaji. Akizungumza katika Mkutwno huo Tatu Abdalla Msellem, Mkurugenzi wa jumuiya Tumaini Jipya Pemba (TUJIPE) amesema katika kupambana na vitendo vya ukatili wa kijinsia na udhalilishaji wanashirikiana na wadau mbali mbali ikiwemo viongozi wa dini ili kila mdau aweze kushiriki katika mapambano hayo.
Nae kwa upande wake Hafidh Abdi Said ni Mkurugenzi wa jumuiya ya Kupunguza Umaskini na Kuboresha Hali za Wananchi (KUKHAWA)Amesema kutokana na uzito wa tatizo la udhalilishji wa kijinsia na udhalilishaji jumuiya hiyo imechukua jitihada za kuhakikisha wanatoa elimu kwa wananmchi maeneo mbali mbali.
Mkutano huo wa waandishi wa habari kisiwani Pemba uliikuwwa na lengo laa kutoa taarifa maalum kuelekea kilele cha siku 16 za kupinga vitendo vya ukatili wa wanawake na watoto wa kike duniani, ambayo huazimishwa kila ifikapo Diosemba 10 ambapo kaulimbiu ya kimaitaifa ya mwaka huu 2022 inasema “KUUNGANISHA UANAHARAKATI KUTOKOMEZA UKATILI DHIDI YA WANWAKE NA WASICHANA.
Ambapo Taasisi hizo ni Chama cha waandishi wa habari wanawake Tanzania ( Tamwa Zanzibar) , Jumuia za wasaidizi wa sheria wilaya 4 za pemba Pegapo, Kukhawa,, Zayco, jumuia ya watu wenyer ulemavu wa akili Zanzibar, ZAPDD, Blog ya Pemba Today pamoja na wizara inayosimamia haki za watoto.
Mwisho.
- Get link
- X
- Other Apps
Comments
Post a Comment