Wakandarasi Miradi ya Elimu Pemba wapewa Neno
NA FATMA SULEIMAN-PEMBA
KATIBU mkuu wizara ya Elimu na mafunzo ya amali Zanzibar Khamis Abdalah Said amewataka wasimamizi wakuu wa ujenzi wa miradi ya Elimu kusimamia na kutekeleza kwa wakati ujenzi wa skuli na madarasa mbali mbali Ili kutimiza lengo la Serekali la kuimarisha Majengo Ili kutoa eElimu bora kwa wanafunzi .
Said Ameyasema hayo kwa nyakati tofauti katika ziara ya ya siku Moja ya kutembea miradi ya elimu inayoendelea kujengewa kisiwani Pemba.
Amesema ni vyema wakandarasi kuongeza Kasi ya utendaji kazi kwa wafanya kazi wao ili waweze kukabidhi miradi hiyo kwa wakati husika ikiwa imekamilika na kwa ubora uliotarajiwa.
Katika hatua nyengine Katibu Mkuu amewataka walimu kutoa ushirikiano wa dhati katika kueka msingi nzuri kwa wanafunzi utakaowezesha kupata Viongozi Bora wa baadae.
Kwa upande wao wakandarasi wa miradi hiyo wameelezea baadhi ya changamoto zinazowakabili hatahivyo wameahidi kumalizia ujenzi huo kwa wakati husika na kwa viwango vya ubora vinavyohitajika licha ya changamoto hizo.
Katika ziara yake hio Katibu Mkuu alitembelea kituo Cha Wakorea kilichopo Madungu, Skuli ya Wanafunzi wenye mahitaji maalum Pujini ,pamoja na Sekondari ambazo zinazoendelea na ujenzi, pia ametembelea Skuli ya Mwambe , Kwale , pamoja na kuzungumza na Walimu Wakuu wa Skuli za Sekondari kisiwani Pemba.
Hii ni ziara yake ya kwanza ya kikazi kisiwani Pemba tokea kuapishwa kukamata nyadhifa hio kufuatia mabadiliko yaliyofanywa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Hussein Ali Mwinyi.
Mwisho
Comments
Post a Comment