SOKO LA OLE LA ZINDULIWA
Na Fatma Suleiman.
MWAKILISHI wa jimbo la Ole Masoud Ali Muhammed
amewataka wafanya biashara wa jimbo la ole kulitumia ipasavyo soko la mboga
mboga lililopo olee kianga bila ya kuingiza itikadi za kisiasa ili kuendelea kujipatia
rizki za halali .
Akizungumza
na wana jimbo mara baada ya uzinduzi wa
soko hilo mh Massoud ambae ni waziri wanchi Ofisi ya Raisi Tawala za Mikoa Serikali za Mitaa na Idara Maalum za SMZ amesema soko hilo amelijenga kwa ajili
ya wanachi wote na sio la mtu binafsi hivyo ni vyema litumike kama lilivyo
kusudiwa.
Kwa
upande wake mkuu wa wilaya ya chake chake Abdala Rashid Ali amewataka wanachi
wa ole kuthamini jitihada za viongozi wao pamoja na kulitunza ili liweze
kutumika kwa muda mrefu .
Akitoa
maelezo juu ya matumizi ya soko msimamizi wa ujenzi wa mradi huo Thabit Othman
Abdalla amesema soko hilo litatumika na
wauzaji zaidi ya 20 ambapo watauza
biashara zao katika mazingira rafiki na salama.
Wakitoa
neno la shukurani kwa niaba ya wafanya biashara wengine Hamad Salum amesema
awali ilikua wakiteseka wao na hata wateja lakini kwa sasa mwakilishi
amewakomboa kutoka kwenye kilio .
Comments
Post a Comment