KAMISHNA ZANZIBAR ATOA ANGALIZO MWENYEWE KWA MADEREVA BODA BODA

NA OMAR HASSAN     

KAMISHNA wa Polisi Zanzibar Hamad Khamis Hamad amesema Jeshi la Polisi litawashughulikia kwa mujibu wa sheria madereva wa bodaboda wanaokiuka sheria na taratibu zilizowekwa ikiwa ni pamoja na kutojisajili kwenye vyama na Jumuiya za waendesha bodaboda.   
                                                                                                            CP Hamad ametoa kauli hiyo huko Paje Mkoa wa Kusini Unguja alipokua akizungumza na wananchi wa Kijiji cha Paje, Bwejuu na Michamvi katika mkutano wa kusikiliza kero za wananchi zinazojitokeza katika maeneo yao.

 Amesema kutofuata sheria na kutojisajili kwa waendesha bodaboda wengi kunachangia kujihusisha na vitendo vya uhalifu waendesha bodaboda hao na kwamba inakuwa vigumu kudhibitiwa na  Jeshi la Polisi kutokana na kukosekana kwa taarifa zao. 

Kwa upande wao wananchi wa Maeneo hayo wamelalamikia videndo vya uvunjwaji wa Sheria vinavyofanywa na waendesha bodaboda.

Comments

Popular posts from this blog

BARABARA 19 KUJENGWA KWA KIWANGO CHA LAMI PEMBA KUKAMILIKA DISEMBA 2024.

WAZAZI ZIDISHENI KUFUATILIA NYENENDO ZA WATOTO HUSUSAN NI VIJANA .

UONGOZI WA WILAYA CHAKE CHAKE KFHI WAPONGEZA JUHUDI