Posts

ZFDA PEMBA YATOA ELIMU VISIWA VIDOGO VIDOGO JUU USALAMA WA CHAKULA, YATOA NA ANGALIZO KWA WAMILIKI WA MADUKA.

Image
Na-  AMINA AHMED MOH’D, PEMBA.  WAKAAZI wa  Visiwa Vinne Kusini  na Kaskazini mwa   Kisiwa Cha Pemba wamefikiwa  na Maafisa  wa Vitengo mbali mbali   Kutoka Taasisi ya Wakala wa Chakula  Dawa na Vipodozi   Na Kupatiwa Elimu  Juu ya Usalama wa Chakula Ikiwa ni Maadhimisho Ya Siku Ya Usalama wa Chakula Duniani  Inayoadhimishwa kila ifikapo  Tarehe 7/6.   Akizungumza na Wanafunzi, Wananchi, Pamoja na Vijana Wa Kisiwa Cha Fundo Wilaya ya Wete katika  Mkutano Maalum wa kutoa Elimu   Kaimu Mkurugenzi wa  Taasisi ya Wakala wa  Chakula  Dawa na Vipodozi  ZFDA  Ofisi ya Pemba Makka  Khamis Ali Amesema kuwa Taasisi hiyo Kwa Upande wa kisiwani Pemba imeamua kutoa Elimu kwa Wananchi wanaoishi Maeneo ya Visiwa ili kuweka usawa  wa Upatikanaji wa Elimu hiyo kwa wananchi wote Waliomo ndani ya Visiwa  vidogo vidogo.      ...

MWENYEKITI UVCCM JIMBO LA MALINDI, KIJANA MDOGO MWENYE NIA YA KUSAIDIA WANAWAKE WENZAKE KUPITIA MAJUKWAA YA KISIASA

Image
Na- Massoud Juma, Unguja   KHAYAM  Musatafa Yakuti bado anaendelea kuwashangaza na kuwastaajabisha wengi kutokana na kuwa na umri mdogo lakini kwa kuwa na uelewa, uthubutu na uhodari wa kujenga hoja katika mada tofauti za kimaendeleo hususani katika masuala ya siasa hapa Zanzibar. Kwa sasa Khayam ana umri wa miaka 23 tu, lakini tayari ameshapata uzoefu wa uongozi tokea ana umri wa miaka nane, mwenyewe anasema alianza kuingia katika mabaraza ya watoto ndani ya shehia, baadae wilaya na hatimae kushika nafasi ya makamu mwenyekiti wa baraza la watoto la Tanzania.  Kama yalivyo malengo ya mabaraza hayo, kumjenga mtoto kuwa na uthubutu na kujiamini, hilo lilifanikiwa sana kwa Khayam, kwani katika harakati za baraza hili za kulinda na kutetea haki za watoto yeye alijifunza mengi na hatimae kuingia katika siasa ili aweze kutumia majukwaa ya siasa kutetea na kulinda haki za wanawake, vijana na watoto. Kwa sasa Khayam ni mwenyekiti wa UVCCM katika jimbo la ...

SALHA MWINJUMA; MWAKILISHI WA VIJANA KUTOKA WILAYA YA KUSINI UNGUJA YAJUE USIYOYAJUA AMBAYO NI MUONGOZO KWA WENGINE WENYE NDOTO ZA KUFIKA ALIPOFIKA YEYE.

Image
NA MASOUD JUMA, UNGUJA SALHA Mohamed Mwinjuma ni mwakilishi wa Viti Maalumu  anayewakilisha vijana kwenye Baraza hilo, ambapo safari yake ya siasa ameianzia akiwa na umri wa miaka 18.  Mwaka 2020 alimaliza masomo yake ya shahada ya kwanza ya Uhusiano wa Kimataifa. Mnamo mwaka 2015 Salha aliwania viti maalumu na hatimaye kufanikiwa kuingia kwenye Baraza hilo akiwakilisha vijana kutoka Mkoa wa Kusini Unguja. Kijana huyo anasema kuwa ameanza harakati zake kwenye umoja wa vijana wa CCM mwaka 2012 kabla ya kujitosa rasmi mwaka 2015 baada ya kuona anaweza kusimama na kutetea vijana wenzake. Anasema amepata wakati mgumu kueleweka na jamii, lakini vijana na wanawake baadhi walimuelewa na sasa wanamuelewa zaidi kwani amekuwa akifanya kazi kwa ushirikiano wa hali ya juu na matokeo yake yamekuwa yakionekana siku hadi siku. “Haikuwa kazi rahisi kwa wakati ule nilikuwa mdogo nina miaka 18 tu, nimejikita kwenye siasa nikiwa sina utani hata kidogo, kwa kweli wengi hawakunielewa w...

MWENGE WA UHURU WAFIKA WILAYA YA MICHEWENI PEMBA

Image
Na Amina Ahmed Moh’d   Pemba  JUMLA ya Miradi 5 ya Maendeleo katika Sekta ya Kilimo, Biashara, Elimu, Afya,  umeme na Maji Yenye Thamani ya Shilingi Bilion 13 Milioni  349   Laki Moja 67  imetembelewa kukaguliwa  na kuwekewa  Mawe ya Msingi Katika Wilaya ya Wete Ikiwa ni Muendelezo wa   Ziara Ya Matembezi ya Mwenge Wa Uhuru  Nchini Ambao Uliwasili Katika Mkoa wa Kaskazini Pemba Mapema Jana Asubuhi huku   kukimbizwa Umbali wa Kilo mita 80  katika Maeneo mbali mbali wilayani  Humo.  Ameyasema  hayo Katibu Tawala Wilaya ya Wete  Mkufu Faki Ali Alipokuwa Akitoa  Taarifa  kwa Niaba ya Uongozi wa Wilaya  hiyo katika Ghafla  ya Makabidhiano ya  Mwenge Wa Uhuru pamoja na Wakimbiza Mwenge huo  kutoka Wilaya ya Wete kwenda Wilaya Micheweni kwajili ya kuendeleza Shughuli za Ufunguzi wa Miradi mbali mbali  ya Maendeleo  Mapemba  Leo  Asub...

MWANAMKE ALIEVUNJA VIKWAZO KATIKA TASNIA YA SANAA YA MUZIKI DJ, HIJAB

Image
Na MASSOUD JUMA UNGUJA JINA lake halisi ni Aisha Bakary lakini anajulikana sana kwa jina lake la kazi ambalo ni HIJAB DJ, binti ambae anatokea hapa visiwani Zanzibar na kazi yake kubwa ni kupiga muziki katika maeneo mbali mbali ya burudani na starehe na amekua mwanamke wa kwanza katika kazi hiyo ya kupiga na kuongoza muziki (DJ) hapa Zanzibar. Aisha ameamua kuvunja mfumo dume ambao umetawala katika tasnia ya muziki, na anawashawishi vijana wenzake wa kike wasizuiwe kutimiza ndoto zao eti tu kwa kujali kuwa tasnia hiyo ni kwa ajili ya wanaume. Aisha pia kwa kupitia kazi yake hiyo mwaka 2019 amejishindia tuzo ya mwanamke wa mwaka ambayo hutolewa na shirika la Women Future ambayo ina lengo la kupongeza, kukuza na kutangaza mafanikio ya wanawake. Aisha anasema tofauti na ilivyozoeleka kwa mavazi ya wadau wa muziki, yeye anafanya kazi zake siku zote akiwa amevaa hijabu na anafanya hivyo ili kuiwelesha jamii kubwa ya kizanzibari kuwa  hakuna ubaya kwa mwanamke kujiajiri kati...

TAULO ZA KIKE KWA WANAFUNZI SKULINI, BILA HUDUMA YA MAJI, DAMPO NA VYUMBA MAALUM HAKUNA HEDHI SALAMA,NI HATARI KWA AFYA ZAO NA ATHARI KATIKA UFAULU WAO.

Image
NA AMINA AHMED MOH’D, PEMBA. ( 0719859184)   IKIWA JANA  28 /5/ Dunia iliaadhimisha siku ya Hedhi  Salama bado kuna mengi yanahitaji kuangaliwa na wadau Serikali na wote wanaopenda Maendeleo bora ya Elimu kwa watoto wa kike kwa Shamra shamra mbali mbali ikiwemo kutoa Elimu  ya Afya ya uzazi kwa baadhi ya wanafunzi, kugawa Sabuni pamoja na Taulo zakike lakini bado kuna changamoto Nyingi ambapo zisipoangalia kwa jicho la Tatu na wadau pamoja na serikali kwakuwekewa mkakati Endelevu Kugawa Taulo kutoa Elimu na Sabuni hizo  hautokuwa Msaada kwa Wanafunzi Wakike Maskulin i.  Jee ni kwa namna gani yataweza kufikiwa Maendeleo ya Elimu ambayo itakuja kuwa mkombozi baadae katika maisha ya mtoto wa kike ni pamoja na kuwa na Afya imara mazingira salama na upatikanaji wa huduma muhimu ambazo zitasaidia kuondosha usumbufu wanapokuwa katika kipindi cha Hedhi. Wanafunzi wengi wakike ambao wamefikia umri wa baleghe ( kuvunja ungo) wakiwa katika hara...

UELEWA WA KURIPOTI MATUKIO YA UDHALILISHAJI WA KIJINISIA KATIKA JAMII UMEONGEZEKA, WANAMTANDAO WAPEWA MASHIRIKIANO NI BAADA YA KUANDALIWA NA TAMWA-ZANZIBAR KUIFIKIA JAMII.

Image
Na Amina Ahmed Moh’d, Pemba  ( 0719859184).  UELEWA katika  Kuripoti Matukio mbali mbali ya Udhalilishaji wakijinsia kwa wanawake na watoto yanapojitokeza katika Jamii kisiwani Pemba Imeelezwa kuongezeka baada ya wanachi kuendelea kutoa mashirikiano kwa wanamtandao  pamoja na kutumiaJukwaa la Habari kuripoti Matendo hayo yanapojitokeza.   Hayo yameelezwa na Wanamtandao wa kupinga udhalilishaji  wa Kijinsia Kisiwani Pemba katika Mkutano maalum wa kuwasilisha Ripoti ya Ufuatiliaji wa matukio ya ukatili na Udhalilishaji   walioifanya katika kipindi cha Miezi 5 kutoka maeneo mbali mbali  ya shehia za Kusini na Kaskazini Pemba.  Wamesema  awali Jamii ilikosa Imani juu ya Mtandao huo wa kufatilia Masuala hayo Lakini kwa sasa  uelewa umeongezeka na wanaendelea kupata Mashirikiano  katika kuendeleza mapambano  hayo.  " Jamiii, Walikuwa wanaona kama sisi hatuna nia ya kupambana na Udhalilishaji, lakini ki...