MWENGE WA UHURU WAFIKA WILAYA YA MICHEWENI PEMBA

Na Amina Ahmed Moh’d   Pemba 
JUMLA ya Miradi 5 ya Maendeleo katika Sekta ya Kilimo, Biashara, Elimu, Afya,  umeme na Maji Yenye Thamani ya Shilingi Bilion 13 Milioni  349   Laki Moja 67  imetembelewa kukaguliwa  na kuwekewa  Mawe ya Msingi Katika Wilaya ya Wete Ikiwa ni Muendelezo wa   Ziara Ya Matembezi ya Mwenge Wa Uhuru  Nchini Ambao Uliwasili Katika Mkoa wa Kaskazini Pemba Mapema Jana Asubuhi huku   kukimbizwa Umbali wa Kilo mita 80  katika Maeneo mbali mbali wilayani  Humo. 


Ameyasema  hayo Katibu Tawala Wilaya ya Wete  Mkufu Faki Ali Alipokuwa Akitoa  Taarifa  kwa Niaba ya Uongozi wa Wilaya  hiyo katika Ghafla  ya Makabidhiano ya  Mwenge Wa Uhuru pamoja na Wakimbiza Mwenge huo  kutoka Wilaya ya Wete kwenda Wilaya Micheweni kwajili ya kuendeleza Shughuli za Ufunguzi wa Miradi mbali mbali  ya Maendeleo  Mapemba  Leo  Asubuhi Katika  Viwanja vya Skuli ya Msingi Finya. 

 Amesema  kuwa Miradi hiyo Ambayo imekuwa Tija  Fursa na  Maendeleo ya Wananchi wa wilaya ya  Wete zaidi ya  shilingi  Bilioni 7 Milion 491  Miatatu 34, ni Mchango Wa Serikali  kwa wananchi wake  Huku zilizosalia zikiwa ni  Fedha kutoka kwa Wahisani mbali mbali Pamoja na Wananchi. 

 "Miradi iliyokaguliwa na Mwenge wa Uhuru Mwaka huu 2023 katika Wilaya  ya Wete  Imegusa moja kwa moja Maendeleo ya Wananchi katika sekta mbali mbali ambapo Serikali yetu ndio ambayo Imewekeza Fedha nyingi katika Miradi hiyo".

Aidha Alieleza kuwa Kupitia Mkesha wa Mwenge Wa uhuru katika Wikaya hiyo wananchi mbali mbali Waliweza Kutumia fursa Ya Kupima Afya zao ju ya Maradhi mbali mbali, ikiwemo Virusi vya ukimwi, Sambamba na wajasiriamali Kuuza bidhaa  na kuweza  kujipatia kipato.

"Neema hii ya Mwenge wa  Uhuru imeleta tija kwa wananchi  mbali mbali katika Wilaya  ya Wete  ikiwemo wajasiriamali Kutumia Shamra shamra hizo kuuza bidhaa  zaona kujipatia Kipato, Pamoja na kupima Afya zao bure." 

 Aidha Kwa upande wake Kiongozi  Mkuu wa Mbio za Mwenge wa  Uhuru  2023 Ndugu Abdalla Shaibu   ameutaka Uongozi wa Wilaya ya Micheweni Kutoa Mashirikiano  Kwa Wakimbiza Mwenge  hao   ili kuweza Kutimiza Malengo Yao waliyakusudia

" Tumepata Mashirikiano na Tumeridhishwa na Miradi mbali mbali Tuliyoitembelea Katika  Wilaya ya Wete  Tuntarajia Mashirikiano Haoa katika Wilaya ya Micheweni ambapo Mwenge wetu wa uhuru Umepiga Hodi leo hii ili kuona Lengo kutembelea Na kukagua Miradi ya  Maendeleo Linafikiwa Ipasavyo . 

Kwa Upande wake Mkuu wa Wilaya Ya Micheweni Mgeni Khatib Yahya Amesema kuwa  Uongozi Wa Wilaya hiyo Umeandaa na kuratibu vyema Shughuli za Ukaguzi  wa Miradi  ya Maendeleo katika Wilaya ya Micheweni.


 Ukiwa  Katika Wilaya hiyo Ya Micheweni  Kiongozi huyo wa  Mwenge wa Uhuru  Ameshiriki  Zoezi, la Upandaji wa Miti Katika Eneo la Kishindeni, Wingwi Mapofu,    Kuweka Jiwe la Msingi  katika Maabara ya Skuli ya Sekondari Shumba Viamboni, Ulazaji wa Mabomba ya Maji safi na salama Katika kijiji cha Kironjo Wingwi huku Ukitarajiwa Kuendelea na Ukaguzi wa miradi mbali mbali ndani ya wilaya hiyo Ambapo kauli mbiu ya Mwenge wa uhuru Mwaka huu ni Tunza Mazingira Okoa Vyanzo Vya Maji, kwa Ustawi wa viumbe Hai kwa Ustawi wa Taifa. 

Mwisho.

Comments

Popular posts from this blog

BAJAJI WAMLILIA RAIS DK MWINYI PEMBA ,WAOMBA MSAADA KWAKWE WASEMA WAMECHOSHWA NA HILI KUTOKA MAWASILIANO

Masheha wanawake wa Wilaya ya Magharib B walivyoleta mabadiliko na maendeleo kwenye shehia zao.

MPANG0 MKAKATI JUMUISHI WA JINSIA KATIKA MICHEZO UTEKELEZAJI WAKE UZINGATIWE.