ZFDA PEMBA YATOA ELIMU VISIWA VIDOGO VIDOGO JUU USALAMA WA CHAKULA, YATOA NA ANGALIZO KWA WAMILIKI WA MADUKA.

Na- AMINA AHMED MOH’D, PEMBA. 

WAKAAZI wa  Visiwa Vinne Kusini  na Kaskazini mwa   Kisiwa Cha Pemba wamefikiwa  na Maafisa  wa Vitengo mbali mbali   Kutoka Taasisi ya Wakala wa Chakula  Dawa na Vipodozi   Na Kupatiwa Elimu  Juu ya Usalama wa Chakula Ikiwa ni Maadhimisho Ya Siku Ya Usalama wa Chakula Duniani  Inayoadhimishwa kila ifikapo  Tarehe 7/6.

 Akizungumza na Wanafunzi, Wananchi, Pamoja na Vijana Wa Kisiwa Cha Fundo Wilaya ya Wete katika  Mkutano Maalum wa kutoa Elimu   Kaimu Mkurugenzi wa  Taasisi ya Wakala wa  Chakula  Dawa na Vipodozi  ZFDA  Ofisi ya Pemba Makka  Khamis Ali Amesema kuwa Taasisi hiyo Kwa Upande wa kisiwani Pemba imeamua kutoa Elimu kwa Wananchi wanaoishi Maeneo ya Visiwa ili kuweka usawa  wa Upatikanaji wa Elimu hiyo kwa wananchi wote Waliomo ndani ya Visiwa  vidogo vidogo. 
        Makka Khamis Ali    - Kaimu Mkurugenzi ZFDA Pemba. 

"Tunapita na kutoa Maeneo yote lakini Kuna utofauti kwa wananchi wanaoishi Katika Visiwa vidogo vidogo na Wananchi wanaoshi  maeneo mengine   Kutokana na sababu mbali mbali ni mara chache  Wananchi wa Maeneo ya visiwa kufikiwa kupata Elimu hii  ukilinganisha na wananchi ambao hawaishi visiwani hivyo Dhamira yetu ni kuona kuna kuwa na usawa wa Elimu hii ya Usalama wa chakula kwa Watu wote". Alisema  Makka Kaimu Mkurugenzi ( ZFDA) 


Alieleza kuwa  Serikali  ya Mapinduzi ya Zanzibar imetoa Jukumu kwa Mamlaka hiyo kusimamia  na kuhakikisha Usalama Wa Vyakula kwa wananchi wote, Hivyo Mamlaka h Itaendelea kutoa Elimu  ya Usalama wa Chakula kwa ili kuweza kuhakikisha  Wananchi wanaondokana na  Madhara ambayo  kwa kutumia Vyakula Visivyosalama yataweza Kuathiri Afya zao. 

"Lengo la Maadhimisho haya ya Siku ya Usalama wa  Chakula Duniani  na tumeamua maalum kuifanya hapa, katika kisiwa  cha Fundo ni kutoa Elimu na Uelewa kwenu nyinyi wananchi juu ya Kuweza kutambua  vyakula Salama, na kuweza kuvitambua  ili kuondokana na madhara yale yote yanayoweza kujitokeza kwa kutumia ama kula vyakula ambavyo sio salama. "

Aidha Kaimu  Mkurugenzi huyo Alisema kuwa Taasisi hiyo katika kuhakikisha usalama  wa Wananchi unapatikana Inaendelea kufanya ukaguzi katika Maduka ya vyakula Maghala, Wajasiriamali wa bidhaa, Vyombo ambavyo vinasafirisha Chakula, ili kuzidisha Uelewa kwa Wamiliki juu ya Kutunza na kuhifadhi  Vyema Kwa Maslahi ya afya njema za  wananchi wake. 

 Kwa Upande wake Mkuu wa kitengo cha Udhibiti  na Usalama wa Chakula  Aweza Hassan Haji amewataka wananchi hao Kuzidisha uangalifu katika kuhifadhi vyakula ili viepukane   kuchafuliwa na vimelea vya Maradhi mbali mbali kemikali zisizo salama Takataka pamoja na Sumu kwa kuweka  na kuandaa kwa mpangilio Sahihi. 
 
 Awali Akiwakilisha Mada kwa wananchi hao  Kassim Fadhil Kassim  aliwataka kutambua vyema majukumu ya  Taasisi ya wakala wa Chakula Dawa na Vipodozi ZFDA  kuwa ni pamoja na ukaguzi, usajili, Uchunguzi wa kimaabara  sambamba na kuwataka kutambua Ubora wa chakula kwa kutumia njia hizo za kitaalamu. 
 
  Katika Hatua nyengine Taasisi hiyo Imewataka Wamiliki wa Maduka  ya Vyakula kujiepusha  Kuuza Dawa za kutibu Magonjwa ya  Binaadamu ndani ya maduka hayo ambapo imesema kufanya hivyo ni kinyume na sheria na taratibu zilizowekwa. 

"Tunaendelea kuwakumbusha Wamiliki wa Maduka  kuwa Kuuza Dawa Tiba yayote  katika Maduka ya Vyakula  ni kosa kisheria   endapo mmiliki hatokuwa na uthibitisho maalum  utakaomruhusu kuuza, Dawa zote zinahitajika kuuzwa  kwa utaratibu maalum na Maduka maalum, ZFDA haitisita kuchujua hatua Stahiki kwa atakaekwenda kinyume na suala hili " Alisema Mussa Muhammed Abdalla Afisa kutoka ZFDA Pemba. 
 

Akitoa neno la Shukurani Kwa niaba ya Wananchi wa  kisiwa cha  Fundo Naibu  Sheha Wa Shehia Hiyo  Hadia Ali Juma  ameishukuru Taasisi hiyo kwa Elimu hiyo ambapo amesema itasaidia kuongeza uelewa wa Wananchi kuweza kutambua Ubira wa vyakula kabla ya kutumia ili kuepusha madhara ya Afya Zao na kuahidi kuwa mabalozi kwa wengine juu ya Elimu hiyo. 


  Siku ya Usalama wa Chakula Duniani kisiwani Pemba imeadhimishwa kwa utolewaji wa Elimu katika Visiwa vya Kojani, Makongwe, Panza pamoja na Fundo ambapo Elimu juu ya  Chakula Salama, Chakula Kisicho salama, Madhara ya Chakula kisicho salama  Pamoja na  Majukumu ya Taasisi  hiyo ya ZFDA  Ilitolewa kwa wananchi wa visiwa Hivyo. 

Mwisho 



Comments

Popular posts from this blog

BAJAJI WAMLILIA RAIS DK MWINYI PEMBA ,WAOMBA MSAADA KWAKWE WASEMA WAMECHOSHWA NA HILI KUTOKA MAWASILIANO

Masheha wanawake wa Wilaya ya Magharib B walivyoleta mabadiliko na maendeleo kwenye shehia zao.

MPANG0 MKAKATI JUMUISHI WA JINSIA KATIKA MICHEZO UTEKELEZAJI WAKE UZINGATIWE.