SERIKALI YAAHIDI KUKIFUNGUA ZAIDI KISIWA CHA KOJANI KWA KUTATUA CHANGAMOTO MBALI MBALI ZINAZORUDISHA NYUMA MAENDELEO KISIWANI HUMO.
NA AMINA AHMED MOH'D, PEMBA ZIARA ya makamu wa pili wa rais Zanzibar Hemed Suleiman Abdulla kuendelea kukagua ujenzi wa skuli za ghorofa maeneo mbali mbali kisiwani Pemba leo hii imefika katika wilaya ndogo ya Kojani mkoa wa kaskazini kukagua mradi huo pamoja kuzungumza na wananchi na kuweza kusikiliza changamoto zinazowakabili . Akizungumza na wanachi katika kijiji cha Kipata Kojani eneo ambalo linajengwa skuli hiyo kwajili ya Wanafunzi wa Msingi makamu huyo amesema kuwa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kuboresha maenedeleo ya elimu kisiwani humo ili kupata Viongozi bora watakoasimamia taifa katika nyanja mbali mbali. " Tunataka tutoe wasomi zaidi na zaidi katika kisiwa hichi, ambao watakuwa wasaidizi na viongozi katika sekta mbali mbali, lengo la serikali ni kuona kojani inabadilika na kuwa kojani yenye maendeleo zaidi lakini pia kuona wasomi wa fani mbalo mbali wa...