KAMATI YA S JIMBO CHAMBANI YATOA MSAADA WA CHAKULA KWA WANAFUNZI WANAOKAA KAMBI , LENGO KUIMARISHA ELIMU.

Na Fatma  Suleiman, Pemba

MWENYEKITI   wa CCM wilaya ya Mkoani Pemba Ali Juma Nassor  amewataka walimu wazee na kamati za Skuli wa skuli za Jimbo la Chambani kuhakikisha wanatoa mashirikiano ya pamoja katika kuwapatia elimu na malezi bora Ili kupata kizazi kinachojielewa na kitakacholeta maslahi endelevu nchini .

Mwenyekiti  ameyasema hayo mara baada ya kukabidhi chakula kwa wanafunzi wanaokaa kambi katika Jimbo la chambani mkoani na kusini Pemba.

Amesema suala la elimu ni la wote hivyo ni vyema kulifanyia kazi kwa kina katika kuwaandaa ziongozi Bora vya baadae .

Aidha amesema Viongozi wao wa Jimbo akiwemo mbunge , Mwakilishi na madiwani wamekua na mchango mkubwa katika kuliinua suala la elimu ndani ya Jimbo Hilo hivyo kuwaomba kuendelea kujitoa kwa ajili Yao Ili kufikia malengo ya serekali ya kuiboresha sekta ya elimu nchini .

Akizungumza kwa niaba ya kamati ya Jimbo la chambani mbunge wa Jimbo Hilo Muhammad Abrahman Mwinyi amesema ni vyema walimu kujikita katika masomo ya sayansi ambapo imeonekana wanafunzi wengi wakifaulu kwa kiwango kidogo kulinganisha na masomo ya art .

Hata hivyo amesema kuwa Viongozi wao wanatambua jitihada zinazochukuliwa na walimu pamoja na kamati za shule katika kuwaandaa wanafunzi lakini Bado amewataka kuongeza bidii Ili kufikia malengo ya kuongeza kiwango Cha  ufaulu nchini .

Kwa upande wake diwani wa wadi ya ngwachani Muhammad Said Ali Amesema wameamua kuendeleza wema huo kwa ajili ya kuongeza kiwango Cha ufaulu katika  kukiandaa kizazi Bora jimboni Ili kuwa mfano .

Wakitoa shukurukani zao walimu na wanafunzi wa Jimbo Hilo wamesema kuwa awali hawakua na viongozi ambao wameliboresha suala la elimu lakini kwa sasa wanaupongeza uongozi kwa jitihada wanazozichukua .

Aidha walimu wakuu wa skuli za msingi na sekondari wa Jimbo Hilo wamesema neema ya Viongozi walionao imewaletea mabadiliko makubwa katika elimu kwani kiwango Cha ufaulu kwa wanafunzi kimeongezeka tofauti na awali .

Skuli zilizopatiwa chakula hicho ni pamoja na skuli ya ngwachani,wambaa chambani ,dodo ,mizingani ukutini na tumbi .

Zaidi ya milioni nne zimetolewa na kamati ya Jimbo la chambani akiwemo mbunge, Mwakilishi na madiwani kwa ajili ya kununulia Mahitaji ya chakula kwa wanafunzi wanaokaa dahalia ndani ya Jimbo Hilo .

Comments

Popular posts from this blog

BARABARA 19 KUJENGWA KWA KIWANGO CHA LAMI PEMBA KUKAMILIKA DISEMBA 2024.

WAZAZI ZIDISHENI KUFUATILIA NYENENDO ZA WATOTO HUSUSAN NI VIJANA .

UONGOZI WA WILAYA CHAKE CHAKE KFHI WAPONGEZA JUHUDI