WAKULIMA WA MBOGA A MBOGA PEMBA WAPEWA ELIMU JUU YA KUTAMBUA UDONGO WENYE AFYA KWA KILIMO, LENGO KUPATA TIJA NA MAENDELEO
- Get link
- X
- Other Apps
NA AMINA AHMED MOH’D, PEMBA.
ZAIDI ya Wakulima 120 wa Mboga mboga na Matunda Kutoka maeneo mbali mbali ya kisiwa cha Pemba wamepatiwa mafunzo maalumu juu ya Afya Bora ya Udongo na usimamizi Wa rutuba kutoka Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Zanzibar.
Akitoa elimu elekezi katika mafunzo hayo mkuu wa division ya Utafiti wa udongo na mimea Zanzibar Ali Hamad Ali alisema kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuwasaidia wakulima kuweza kuchunguza afya ya Udongo kabla ya kulima mazao yao kuepuka hasara na kujipatia faida kupitia kilimo chao.
"Udongo ndio tegemeo kubwa la wakulima katika masuala ya kilimo tumeona ni vyema kufikisha elimu hii kwa wakulima kutokana na waliowengi kukosa elimu hii na kupata hasara mbali mbali ikiwemo mazao kuharibika pamoja na miche" .
Alisema Kutokana na wakulima wengi kuendelea kutumia mashamba ambayo yalishatumika kwa muda mrefu na mashamba hayo kuondokana na virutubisho na kupelekea kutofikiwa malengo ya kunufaika na mazao kwa wakulima taasisi hiyo imeamua kuwa karibu na wakulima kutoa Elimu hiyo itakayobadilisha maisha yao .
"Ili kufanya kilimo kiwe Endelevu na wakulima waweze kupata tija na mazao mazuri tumeona ni bora kueneza elimu hii ya uhuwishaji na utunzaji wa udongo lengo ni kulima kitaalamu kwa kutumia teknologia yenye kuutambua udongo".
Akitoa Elimu hiyo elekezi kwa wakulima hao Asha Muhamed Shoka kutoka Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Zanzibar kiteng cha udongo amewataka wakulima hao kufanya uchungizi na kupima udongo kabla ya kuanza harakati za kilimo ili kuwasaidia kutambua aina za udogo.
"Kupima udongo kutaweza kuwasaidia wakulima kujua aina gani ya udongo inafaa kwa kilimo au mazao fulani hiyo itawadaia kuwaepushia hasara mbali mbali mnazozipata katika mashamba yenu".
Katika udongo kuna P, H tofauti tofauti ambazo ni maalum kwajili ya mboga mboga za aina fulani kuupima kabla ya kuanza kulima ni bora zaidi ili kuendana sambamba na teknologia katika kukuza kilimo.
Wakizungumza mara baada ya mafunzo hayo baadhi ya wakulima waliopatiwa mafunzo Maryam Rashid salum Ali kutoka Mjini Ole pamoja na Mafunda Bakari Ali wamesema elimu hiyo itasaidia kulima kilimo cha kisasa ambacho kitawasaidia kuikomboa kiuchumi ambapo pia wamesema wataifikisha kwa wakulima wengine ambao walikosa mafunzo hayo ili kuwanufaisha.
Mradi wa kufikisha Teknologiya ya kutunza afya ya udongo kwa wakulima wa mboga mboga, na matunda World Vigitable umefadhiliwa washirika wa maendeleo mbali mbali ya maendeleo ikiwemo IFDC pamoja na USAID ambapo wakulima mabwana shamba viongozi wanshehia na maafisa kilimo wilaya zote nne za pemba walishiriki katika mafunzo hayo Ambapo Mafunzo hayo ya siku moja yalifunguliwa na Afisa Mdhamini wizara ya kilimo Pemba .
- Get link
- X
- Other Apps
Comments
Post a Comment