SERIKALI YAAHIDI KUKIFUNGUA ZAIDI KISIWA CHA KOJANI KWA KUTATUA CHANGAMOTO MBALI MBALI ZINAZORUDISHA NYUMA MAENDELEO KISIWANI HUMO.
NA AMINA AHMED MOH'D, PEMBA
ZIARA ya makamu wa pili wa rais Zanzibar Hemed Suleiman Abdulla kuendelea kukagua ujenzi wa skuli za ghorofa maeneo mbali mbali kisiwani Pemba leo hii imefika katika wilaya ndogo ya Kojani mkoa wa kaskazini kukagua mradi huo pamoja kuzungumza na wananchi na kuweza kusikiliza changamoto zinazowakabili .
Akizungumza na wanachi katika kijiji cha Kipata Kojani eneo ambalo linajengwa skuli hiyo kwajili ya Wanafunzi wa Msingi makamu huyo amesema kuwa serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kuboresha maenedeleo ya elimu kisiwani humo ili kupata Viongozi bora watakoasimamia taifa katika nyanja mbali mbali.
" Tunataka tutoe wasomi zaidi na zaidi katika kisiwa hichi, ambao watakuwa wasaidizi na viongozi katika sekta mbali mbali, lengo la serikali ni kuona kojani inabadilika na kuwa kojani yenye maendeleo zaidi lakini pia kuona wasomi wa fani mbalo mbali wanaendelea kutoka huku .
Aidha Makamu huyo amewataka wanachi wa kojani kutoa mashirikiano kwa wasimamizi wa jengo hilo ili kuona linakamlika kwa wakati lna kuanza kutumiwa na wanachi.
Katika hatua nyengine makamu huyo amesema serikali itaendelea kulipatia ufumbuzi suala la kituo cha afya ambacho kwa sasa hakikidhi mahitaji kwa wananchi kisiwani humo kutokana na udogo wake.
"Salam kutoka kwa mh rais kaniambia serikali ipo mbioni kuzipatia ufumbuzi changamoto zote zinazorudisha nyuma maendeleo ya kojani ikiwemo kuongeza kituo cha Afya amabacho kitasaidia wananchi kuondoa changamoto zinazowakabili".
"Jumla ya shilingi bilioni 20 mh rais ameshazitenga kwajili ya kuleta maendeleo ikiwemo kisiwa cha kojani maendeleo ya elimu, afya maji na mengineyo, na ifikapo 2030 kojani itakuwa kojani nyengine.
Sambamba na hayo Hemed amewataka wananchi kuendelea kuhamasishana maendeleo na kuacha mambo yasio na maana yanayirudisha nyuma harakati za kufikiamaendeleo.
Awali akizungumza katika mkutano huo waziri wa elimu na mafunzo ya amali Zanzibar leila Muhammed Mussa amesema utakapokamilika ujenzi wa ghorofa hiyo kutasaidia kutatua changamoto ya uhaba wa madarasa kisiwani humo na kuwaondoshea usumbufu.
" Miongoni mwa changamoto kubwa katika elimu kisiwa cha Kojani ilikuwa ni skuli ya msingi kutokana na iliyopo kuwa haikidhi matakwa ya wanafunzi, ni wengi madarasa hayatoshi kukamilika kwa ujenzi kutasaidia kuondoa changamoto hiyo.
Kwa Upande wake mkandarasi wa kampuni hiyo Sinic construction Hawa Abdalla Said amesema itasimamia ujenzi huo kukamilika mapema kabla ya muda uliowekwa kwa ubora.
Mwisho
Comments
Post a Comment