ZAN MALIPO YADAIWA KUZOROTESHA HUDUMA ZA VYETI VYA KUZALIWA WANANCHI WAIOMBA SERIKALI KULIANGALIA VYEMA SUALA HILI.

NA AMINA AHMED MOH’D, PEMBA. 

BAADHI ya Wazazi wamelalamikia   kukosa huduma zavyeti vya  kuzaiwa vya watoto wao  kwa wakati katika kituo cha  utolewaji wa huduma  hizo wilaya  ya Chake chake  kwa zaidi ya siku 5 kwa  kile wanachojibiwa na watoa huduma kuwa ni  kukosekana kwa huduma ya kimtandao katika ofisi ya wakala wa usajili wa  matukio ya huduma za kijamii. 

 Wamesema  suala hilo limekuwalikisababisha hasara kwao kutokana na kutoka masafa ya mbali  huku mchezo huo wa nenda rudi   ukikosa 40 kwa zaidi ya siku nne sasa  ambao  wanasema hifu yao ni kucheleweshewa na  baadae kuonhezew malipo katika huduma hiyo kwa kosa la kuchelewesha.

 Aidha wanachoendelea kulalamikia baadhi ya wananchi hao  wamesema ni kukosa taarifa maalum juu ya tatizo hilo  ili kuweza kupumzika mpka yatakapokuwa sawa.

 Wananchi hao ambao wengi wao ni akina mama na watoto wameiomba Serikali kuliangalia suala hilo ili kuwaondoshea usumbufu  wanaoupata  katika kuitafuta huduma hiyo muhimu. 

" Nimeshakuja hapa mara ya nne hii kila nikija naambiwa mtamdao unasumbua nisubiri nasubiri saa mbili mpka saa sita hakuna linalokuwa, sijui unasumbua nini wala mtandao gani unaosumbuwa nakosa kuelewa  kibaya zaidi  nashindwa  kujua lini huduma hiyo itarejea ili itakaporejea ndio nije  nisihangaike na mtoto kila siku" Alisema mama aliefika kufata huduma  ya cheti cha kuzaliwa cha mtoto kutoka Mchanga mrima jina linahifadhiwa. 

 "Nauli ya nenda rudi kila siku juu ya suala hili  hatunayo mimi nimekuja Jumatatu nikaambiwa nije jana sikuja  leo nimeomba  nauli nipo hapa ndio  yale yale niliyoyakuta jumatatu natoka vitongoji 800 nauli  kila siku iko wapi . 

 " Changamoto zipo lakini wangeweka taarifa tukajua mana pale tukifika tunaandika namba za simu wangetutumia ujumbe tu kama huduma  bado hazijarudi". Alidai mama mwengine kutoka Vitongoji  Chake chake. 

 "Tukiwauliza wanatuambia mfumo mfumo sisi tunajuaje kuhusu mfumo  tunasumbuka bure na watoto   kila siku kupoteza nauli zetu na tunakazi tele majumbani za kufanya tunaziwacha leo tunakaa apa tunasubiri ndege ituwe  bandaraini ". 

Miongoni mwa watoa huduma ambae sio  msemaji wa taassisi hiyo kisheria  jina lina hifadhiwa amekiri kuwepo kwa tatizo  hilo   ambalo amedai kuwa linasababishwa  na mfumo wa zan malipo pamoja na banki .

"Ili tuandike cheti nilazima kukamilika kwanstakabadhi za malipo  na malipo mwananchi anapewa namba ya  mfumo kwajili ya malipo na sisi tunasubiri uthibitisho ndipo tunatoa huduma hizo inapotokea zinachelewa kupitia huo mfumo wa kibenki na huduma huku zinachelewa ndio changamoto kubwa". 

Aidha amesema kuwa  kuhusu usumbufu wanaoupata wananchi kwenda  na kurudi  kupata  bila kupata huduma hiyo ni kutokana na kushindwa   kuwapa ahadi ya uhakika   kwa vile changamoto hiyo ipo nje ya uwezo wao kuipatia ufumbuzi. 

 Alidai kuwa kutokana na taasisi hizo za malipo na wakala kuwa mbili tofauti hupelekea  kushindwa kulidhibiti  na kuwapa usumbufu wananchi wanaotaka huduma za  vyeti vya kuzaliwa kwa watoto baadhi ya siku.

 Harakati  za kumtafuta Msemaji mwenye dhamana juu ya suala hili   kisiwani Pemba  zinaendelea kwa jili ya kupata ufafanuzi zaidi.
 

Comments

Popular posts from this blog

BARABARA 19 KUJENGWA KWA KIWANGO CHA LAMI PEMBA KUKAMILIKA DISEMBA 2024.

WAZAZI ZIDISHENI KUFUATILIA NYENENDO ZA WATOTO HUSUSAN NI VIJANA .

UONGOZI WA WILAYA CHAKE CHAKE KFHI WAPONGEZA JUHUDI