WANANCHI WAHIMIZWA KUTUMIA VYANDARUA KWA USAHIHI KUMALIZA MALARIA PEMBA

NA AMINA AHMED MOH’D. 
     Massoud Suleiman Abdulla, Mkuu kitengo Idara ya Tiba Pemba. 

WANANCHI wametakiwa kuvitumia  kwa  Usahihi vyanadarua vinavyotolewa na  na Wizara ya Afya  ili lengo la kumaliza Malaria Zanzibar  liweze kufikiwa.
Ametoa  Ombi hilo mkuu wa Idara ya Tiba Massoud Suleiman Abdulla kwa niaba ya Afisa mdhamini wizara ya Afya  Pemba   Khamis Bilali Ali wakati wa mkutano maalumu  wa  kutoa taarifa  kwa wananchi  kupitia waandishi wa habari juu ya hali ya malaria na ufuatiliaji wa ugonjwa huo  kisiwani humo.

 Amesema  ili lengo la kumaliza Malaria Zanzibar liweze kufikiwa na kuwa asilimia 0  ni vyrma wananchi kufuata taratibu zilizowekwa  juu ya matumizi sahihi ya vyandarua vinavyoendelea kutolewa bure kwa mama wajawazito na watoto wanapofika hospitali.

"Serikali inafanya kila jitihada kuona hiyo asilimia 0.4  ya ugonjwa wa Malaria uliopo inamalizika kabisa  wadau wa maendeleo pia  wanaunga mkono kuona kila mwananchi anankuwa salama  dhidi ya ugonjwa huu lakini Baadhi ya wananchi huvitumia vyandarua hivyo kwa lengo  ambalo silo kabisa lililokusudiwa".

"Wapo wanaovichana na kuzibia miche  yao shambani na wao kulala bila vyandaraua vilivyokuwa havijapigwa dawa niwaase kuacha hiyo tabia  katika kuona tunasaidia serikali kumaliza Malaria  yasiwepo kabisa".

 Aidha Mdhamini huyo amewataka wananchi kufika katika  hospitali na vituo vya afya  ili kuweza kupima Afya zao   mara wanapoziona dalili za Ugonjwa wa malaria na kuacha kuacha kutumia dawa kinyume na utaratibu uliowekwa.


 Akizungumza katika Mkutano huo  Mkuu  kitengo cha Malaria Pemba Makame Muhamed Kombo  amesema  kitengo hicho kwa sasa  kinaendelea  na hatua mbali mbali katika kudhibiti ugonjwa huo ikiwemo kupiga Dawa   kutoa vyandarua  kutoa elimu na kudhibiti wagonjwa kutoka nje kwa kupima afya  wanapoingia kisiwani humo kwa lengo la kumaliza  ugonjwa malaria.

 Aidha Mkuu huyo  Amewataka waandishi wa habari  kusaidia kufikisha elimu hiyo  kwa wananchi ili waweze kujilinda dhidi ya ugonjwa wa malaria.


Katika kipindi cha  Mwezi wa  1 hadi mwezi wa 7 mwaka 2023  jumla ya wananchi  5,755 wamefikiwa na kupewa vyandarua vilivyotiwa dawa  katika wilaya ya Wete  huku  Wilaya ya Mkoani wananchi 4,417 wilaya ya Micheweni   ni  5,474 na Wilaya ya Chake chake 5,390 ambao ni mama wajawazito na watoto waliopiga chanjo huku upimaji wa ugonjwa huo majumbani ukifikia Asilimia 96.33   na kubainika kuwa na Asilimia 0.016  ya uathirikaji wa ugonjwa huo kwa waliobanika.

Mwisho. 

Comments

Popular posts from this blog

BARABARA 19 KUJENGWA KWA KIWANGO CHA LAMI PEMBA KUKAMILIKA DISEMBA 2024.

WAZAZI ZIDISHENI KUFUATILIA NYENENDO ZA WATOTO HUSUSAN NI VIJANA .

UONGOZI WA WILAYA CHAKE CHAKE KFHI WAPONGEZA JUHUDI