CHANGAMOTO YA MADARASA MBIONI KUPATA UFUMBUZI , WIZARA YAPONGEZA SERIKALI, MAJENGO YA GHOROFA YAENDELEA KUJENGWA KILA KONA ZANZIBAR, MAKAMU WA PILI AFANYA ZIARA KUKAGUA.
AMINA AHMED MOH’D, PEMBA - 0776859184
MAKAMU wa Pili wa rais Hemed Suleiman Abdulla Amefanya ziara ya kutembelea na kukagua ujenzi wa Skuli za ghorofa am zinaendelea kujengwa katika maeneo mbali mbali Kusini na Kaskazini mwa kisiwa cha Pemba zilizopo chini ya wizara ya elimu na mafunzo ya amali Zanzibar.
Akizungmza kwa nyakati tofauti Hemed amewataka wasimamizi wa ujenzi wa skuli hizo kuhakikisha majengo hayo yanakamilika na kukabidhiwa kwa serikali kwa wakati uliowekwa wa makabidhiano.
Amesema lengo la serikali ni kuondoa msongamano wa wanafunzi madarasani kwa kutatuanchangamoto ya madarasa hivyo kukamilika kwa wakati majengo hayo kutasaidia kuondoa changamoto hiyo na kuongeza kasi ya ufaulu.
" Niwaombe wasimamizi na wakandarasi mfaanye kazi ikibidi usiku na mchana kwavile vifaa vipo kuhakikisha majengo haya yanakabidhiwa kwa serikali kwa wakati uliokusudiwa" .
"Dhamira ya serikali ni kuona majengo haya yanakabidhiwa yakiwa yamekamilika mwishoni mwa mwezi wa mwaka huu na mengine mwanzoni mwa mwaka 2024".
"Nia njema ya serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ni kuona kila mwananchi anafurahia maendeleo mh rais anataka kuona changamoto ya madarasa inamalizika kabisa ndio mana akaona ipo haja ya kujenga majengo nane ya skuli za ghorofa ambazo zitakuwa na vyumba visivyopungua 40 na tutaendelea ili kuona wanafunzi wanasoma bila usumbufu na kupata matokeo mazuri".
Katika hatua nyengine Hemed amewataka wakandarasi na washauri elekezi kutoa fursa za ajira za muda zinazopatikana katika ujenzi wa majengo hayo kwa wazawa ili kuweza kunufaika "
Akizungumza katika ziara hiyo waziri wa elimu na mafunzo ya amali Zanzibar Leila Muhammed Mussa ameishukuru serikali ya awamu ya nane kwa kusimamia vyema changamoto za elimu ikiwemo uhaba wa madarasa.
" Baada ya kuona bado kuna changamoto ya uhaba wa madarasa kwa wanafunzi wetu wizara ya elimu tulipeleka ombi kwa mh rais tunashukuru hakusema tusubiri wahisani alisema tutatatua changamoto hii sisi wejyeqe serikali na ni kweli tunaona majengo haya yakiendelea kila kona tunatoanpongezi zeru za dhati "
" Tunashukuru Kupitia fedha za serikali wizara ya elimu imepata majengo kama haya yanaoyoendelea ujenzi wake kila kona 8 kwa kwa hapa kisiwani Pemba lakini 13 kwankisiwani unguja ambayo ni sawa na 21 ni hatua kubwa sana".
Jumla ya majengo sita ya skuli za ghorofa yanayoendelea ujenzi wake zimetembelewa kupitia ziara hiyo ikiwemo Mwambe, Kiwani, Michakaeni, Ole, Utaani, Konde Pamoja na Maziwa ngombe Micheweni ambapo changamoto zilizobainika katika ujenzi huo wkamadarasi wameahidi kuzifanyia kazi huku zinazohusu serikali makamu huyo akiahidi kuzipatia ufumbuzi ikiwemo ujenzi wa barabara ya ndani skuli mpya ya Mwambe.
Mwisho
Comments
Post a Comment