BARABARA 19 KUJENGWA KWA KIWANGO CHA LAMI PEMBA KUKAMILIKA DISEMBA 2024.
NA,AMINA AHMED MOH'D. JUMLA ya barabara 19 kutoka maeneo mbali mbali kusini na kaskazini Pemba ambazo zitakuwa na urefu kilo mita 99.4 zinatarajiwa kujengwa kwa kiwango cha lami na kukamilika ujenzi wake mwezi Disemba mwaka huu 2024 . Barabara zenye urefu tofauti ikiwemo kubwa yenye kilo mita 12 kutoka Konde makangale mnarani ni mkakati maalum uliowekwa na serikali ya mapinduzi ya zanzibar kupitia mwaka mpya wa bajeti unaoanza mwezi july . Akizungumza mara baada ya kumaliza ziara maalum ya kuangalia utekelezaji wa sekta ya barabara na bandari kisiwani humo katibu mkuu wizara ya mawasiliano ujenzi na uchukuzi Zanzibar Dk Mngereza Mzee Miraji amesema kuwa serikali imedhamiria kuzikamilisha kwa wakati barabara hizo za kimkakati zilizowekwa na wizara hiyo kupitia bajeti mpya . ...
Comments
Post a Comment