KADUARA ATOA AGIZO HILI KWA WATENDAJI WA IDARA ZAKE KUHUSU KUIMARISHA HUDUMA KWA WANANCHI.
NA, FATMA ABRAHMAN, PEMBA.
WAZIRI wa Maji Nishati na Madini Shaibu Hassan Kaduara amezitaka idara zote za serekali kushirikiana kwa pamoja katika kuboresha miundombinu kwa lengo lakuleta maendeeleo Bora kwa wananchi.
Waziri huyo ameyasema hayo wakati akiwa katika ziara yake yakagua miradi ya matangi ya maji ikiwemo la chanjaani , pujini na kendwa kwa lengo la kuangalia miundombinu na kutaka kufahamu changamoto zinazojitokeza katika maeneo hayo .
Amesema kwa sasa wananchi hawataki tena maneno bali wanataka vitendo Ili kuona huduma Bora za maendeeleo zinafanikiwa kwa lengo la kuimarisha shuhuli zao huku wakiinua Pato la taifa.
Mapema kaimu mkurugenzi wa mamlaka ya maji zawa Hamad Mussa Rashid amesema serekali Ina nia ya kuboresha huduma ya maji safi na salama mjini na vijijini hivyo kuwataka wananchi kuchangia huduma hio kwa lengo la kumudu gharama za kutatua changamoto mbali mbali zinazoweza kujitokeza .
Comments
Post a Comment