WIZARA YA AFYA PEMBA YATOA NENO KWA WANAOSAMBAZA UVUMI KUHUSU MAGONJWA YA MIRIPUKO.
NA AMINA AHMED MOH'D, PEMBA. WIZARA ya Afya Zanzibar imewataka waandishi wa habari pamoja na wahudumu wa Afya ya jamii CHV kungana pamoja katika kuiweka salama jamii juu ya majanga ya miripuko mbali mbali kwa kuelimisha na kutoa taarifa kutoka kwa vyanzo vyenye usahihi ili kuepusha mitafaruku inayowapata wananchi kutokana na uvumi hususan katika msimu wa mvua zinazoendelea kunyesha. Kauli hiyo imetolewa na Afisa Mdhamini Wizara ya Afya Pemba Khamis Bilali Ali alipokuwa akizungumza na baadhi ya wanahabari wa vyombo mbali mbali pamoja na wahudumu wa Afya jamii CHV kiswani Pemba katika mafunzo maalumu juu ya kudhibiti kusambaa kwa uvumi na maneno mbali mbali katika vipindi vya majanga huko Samail Gombani Chake. Amesema makundi hayo yanayonafasi kubwa katika kusaidia jamii kuwa na uwelewa wa kutofautisha uvumi na taarifa potofu kwa kuweka usah...