DC WETE ATOA NENO HILI KWA MAMLAKA YA MAPATO TRA MKOA WA KIKODI PEMBA.
NA AMINA AHMED MOH’D PEMBA. 0776 859184
MAMLAKA ya Mapato Tanzania TRA imetakiwa kuandaa mifumo imara itakayosaidia kuongeza uelewa kwa wananchi kisiwanibPemba juu ya usahihi wa ulipaji kodi zinazokusanywa na mamlaka hiyo .
Kauli hiyo ya mkuu wa mkoa wa kaskazini Pemba Salama Mbarouk Khatib iliyotolewa kwa niaba yake na mkuu wa wilaya ya Wete Hamad Omar Bakari alipokuwa akizungumza na watendaji, na wafanya kazi wa mamlaka hiyo mkoa wa kikodi Pemba mara baada ya kumalizika ghafla ya ufunguzi wa ofisi za mamlaka hiyo Wete mapema Leo.
Amesema bado ni wananchi wachache hususan ni kisiwani Pemba ambao wanauelewa wa kutosha juu ya kulipa kodi kwa mamlaka hiyo na wengine kukwepa kwa makusudi kutokana na kutokuwepo kwa mifumo imara ya ukusanyaji wa kodi jambo ambalo hupelekea kukosekana kwa mapato ambayo yangeongeza ufanisi katika uimarishaji wa huduma mbali mbali za maendeleo.
" Hayo yote yataweza kutusadia kupiga hatua kubwa za kimaendeeo, iwapo mfumo utaimarishwa na elimu itatolewa kwa wananchi bado uhitaji wa mambo haya mawili hususan ni huku kisiwani Pemba yanahitajika " Alisema Hamad.
Aidha amewataka wananchi kuendeleza uzalendo wa nchi kwa kulipa kodi kwa maslahi ya taifa na kuongeza zaidi maendeleo yanayoendelea kuletwa na viongozi wa nchi.
" Nchi zote zilizoendelea wananchi ndio wanaolipa kodi wala hawazikwepi kadhalika na sisi tumuunge mkono rais wetu wa Tanzania Dk Samia Suluhu Hassan lakini na Rais wetu Dk hussein Ali Mwinyi katika kulipa kodi kwa mamlaka zilizopewa dhamana ya kukusanya kodi ambazo ndizo ambazo zinatumika kwajili ya maendeleo mbali mbali".
Akizungumza kwa niaba ya kamishna mkuu wa TRA Kaimu Naibu Kamishna wa huduma za kiufundi wa mamlaka hiyo Venance Mshana amesema kuwa Kwa kipindi cha mwaka 2022 mamlaka hiyo imeupandisha Pemba hadhi kikodi na kuwa mkoa rasmi wa kikodi lengo ni kusaidia kuongeza usimamizi wa masuala yite yanayohusu kodi mbali mbali kuweza kufanyiwa kazi bila usumbufu woqote wa kuzifata nje ya kisiwa hicho.
Nae kwa upande wake Meneja wa Mkoa kikodi Pemba Arif Said Amesema kuwa dhamira ya kufungua ofisi hiyo kwa upande wa kaskazini Pemba ni kusogeza karibu huduma za kikodi kwa wananchi ambao awali walikuwa wanazifuata huduma hizo ofisi kuu ya mkoa iliyopo Chake Mkoa Kusini Pemba.
Ufunguzi wa ofisi hiyo ya TRA wilaya ya Wete imeambatana na burudani mbali mbali ikiwemo musiki wa kizazi kipya pamoja na ngoma ya msewe kutoka kambini kichokochwe.
Mwisho
Comments
Post a Comment