WANANCHI KISIWANI PEMBA WAASWA KUENDELEZA MASHIRIKIANO NA TRA KATIKA KULIPA KODI KWA HIARI.
- Get link
- X
- Other Apps
Ametoa wito huo mkuu wa wilaya ya Chake Chake Abdalla Rashid Ali kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa kusini Pemba Matter Mahor Massoud alipokuwa akizungumza na wananchi huko katika uwanja wa gombani mara baada ya kumaliza matembezi maalum yalioandaliwa na mamlaka ya mapato Tanzania TRA mkoa wa kikodi kisiwani humo yalioanzia uwanja wa Tibirinzi ikiwa ni wiki maalum ya kurejesha shukurani kwa walipa kodi .
Amesema kodi zote zinazokusanywa na mamlaka hiyo kwa upande wa Zanzibar Pamoja na mamlaka ya mapato Zanzibar hutumika kwa ajili ya kuleta maendeleo kwa taifa na kuondoa changamoto za kukosekana kwa huduma muhimu kwa jamii.
‘’ Tuendelee kushirikiana na mamlaka hii ambayo imewekwa maalum katika kuisaidia serikali na kuweza kupatikana mapato ambayo yatasaidia kuimarisha huduma za kijamii, kwani kwa sasa serikali yetu haitegemei sana misaada kutoka nje kwa sasa tunategemea kodi zetu za ndani ambazo zinatolewa na wananchi‘’ .
Aidha mkuu huyo ameishukuru mamlaka hiyo kwa kuonesha uzalendo wa kurejesha shukurani kwa wananchi ambapo amesema kitendo hicho kitasaidia kuongeza hamasa kwa jamii juu ya ulipaji wa kodi .
‘’ Walipaji kodi kwetu ni watu muhimu sana katika kujenga nchi hivyo kitendo hiki cha kurejesha shukurani kwa kutoa misaada ya ujenzi na vifaa katika sekta mbali mbali kutasaidia kuongeza hmasa kwa jamii juu ya kulipa kodi ‘’ alisema mkuu huyo .
Akizungumza kaimu meneja wa mamlaka ya mapato Tanzania TRA mkoa wa kikodi Pemba Sleiman Nuhu Sleiman amesema lengo la kuandaa wiki maalum kwajili yamlipa kodi ni kurudisha shukrani kwa wananchi pamoja na kuirudisha kodi hiyo katika jamii .
SLEIMAN NUHU SLEIMAN, KAIMU MENEJA TRA PEMBA
‘’ Kila ifikapo mwezi wa 11 ni kawaida kwa mamlaka ya mapato kuandaa wiki maalum kwajili ya mlipa kodi ikiwemo kugawa zawadi kwa waliofanya vizuri katika ulipaji kodi ,kujenga majengo na miundombinu ambay mazoezi kutoka maeneo mbali mbali ,viongozi wa serikali wafanya kazi pamoja na watendaji wa TRA meneja msaidizi forodha mkoa wa kikodi Pemba Sleiman Abdalla Said amesema mamlaka hiyo itaendelea kushirikiana na kuwa karibu na wananchi na kuifikia jamii katika kutatua changamoto mbali mbali .kisiwani humo.
Wiki hiyo ya kurejesha shukurani kwa walipa kodi Pamoja na bonanza hilo pia itaadhimisha wiki hiyo kwa kutoa msaada wa vifaa kwajili ya skuli ya Michenzani wilaya ya Mkoani, ufunguzi wa jengo la ofisi ya TRA kaskazini, Pamoja na kutoa zawadi kwa washindi mbali mbali waliofanya vizuri katika ulipaji wa kodi ambapo kauli mbiu ya wiki hiyo ni ‘’Kodi Yetu Maendeleo yetu Tuwajibike’’.
Mwisho.
- Get link
- X
- Other Apps
Comments
Post a Comment