WAANDIKISHAJI DAFTARI LA KUDUMU LA WAPIGA KURA WAASWA UADILIFU.
- Get link
- X
- Other Apps
Amina Ahmed Moh’d
Tume ya Uchaguzi Zanzibar ZEC inaendelea na mafunzo ya siku mbili kwa Wakuu wa vituo na Makarani wapya waliochaguliwa kusimamia zoezi la uandikishaji wa daftari la wapiga kura wapya linalotarajiwa kuanza rasmi tarehe tarehe 2 /12/ mwaka 2023 kwa awamu ya kwanza katika wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba.
Mpango huo wa matayarisho ya uendelezaji wa uandikishaji wa daftari la kudumu la wapiga kura kwa wapiga kura wapya wapya kuelekea uchaguzi mkuu mwaka 2025 ni miongoni mwa utekelezaji wa majukumu ya msingi ya Tume ya Uchaguzi.
Akizungumza na na watendaji hao mkuu wa kurugenzi ya mifumo ya uchaguzi Tume ya Uchaguzi Zanzibar ZEC Mwanakombo Machano Abuu amewataka kufanya kazi hiyo kwa mujibu wa haki na malengo yaliokusudiwa.
Amesema watendaji wanapaswa kutambua kuwa jukumu hilo wanalokwenda kulisimamia ni jukumu la kitaifa linalohitaji kuendeshwa kwa uweledi na kutimiza malengo ya taifa kupitia mfumo wa kidemocrasia.
"Zoezi la uandikishaji halihitaji ushabiki wa kisiasa, niwaombe sana jiepusheni kushabikia vyama wakati wa uandikishaji kwani kufanya hivyo kutaweza kupelekea kutia dosari zoezi zima la uandikishaji, niwatake kila mmoja wenu aelekeze akili yake katika kazi hiyo kwa kuzingatia haki na sheria bila kujali mtu anatokea chama gani".
Aidha amewataka kutoa vipaumbele kwa watu wenye mahitaji maalum ikiwemo wazee, wajawazito, watu wenyw ulemavu , ili kuweza kuipata haki hiyo bila usumbufu.
Nae kwa upande wake mkuu wa wakurugenzi huduma kwa wapiga kura kutoka Tume ya Uchaguzi Salum Juma amewataka watendaji hao kuwa makini katika suala la utunzaji wa vifaa vya uandikishaji, sambamba na kuepuka kuchezea mifumo ya kuandikia.
Kama tunavyojua zoezi hili la uandikishaji mara hii ni la kidigitali zaidi kwahiyo tunatakiwa vifaa tuvitunze vizuri ili vitumike mara nyingi zaidi katika uandikishaji".
Kwa Upande wake Afisa uandikishaji Tume ya Uchaguzi, wilaya ya mkoani Juma Fumu Makame amesema lengo la mafunzo hayo kwa wakuu wa vituo na makarani hao ni kuwafundisha na ujuzi utakaosaidia kufanikisha zoezi hilo kwa umakini zaidi.
Mafunzo hayo ya siku mbili juu ya mfumo wa uandikishaji kwa makarani na wakuu wa vituo yamefanyika katika ukumbi wa Kiwanda cha makonyo wawi Chake Chake ambapo Zoezi hilo linatarajiwa kuanza kesho Tarehe 2 katika wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini Pemba.
Mwisho.
- Get link
- X
- Other Apps
Comments
Post a Comment