CHUO CHA UFUNDI WENI NI FURSA KWA VIJANA KUJIAJIRI YOTE NI MATUNDA YA MAPINDUZI YA ZANZIBAR
NA THUREYA GHALIB, PEMBA.
Wakwezi na Wakulima ,hapo walipokutana ,maneno waliyosema ,tutashindaa kwa nguvu zake karima,hii ni wimbo maarufu sana ya mashujaa wetu wa Mapinduzi ambao hautaweza kusahaulika katika akili za Mzalendo na Mpenzi wa Nchi yake ya Zanzibar.
Wimboo huu unakumbusha jinsi mashujaa walivojipanga na kufanya mapinduzi huku wakiwa na ujasiri wa hali ya juu huku wakielekeza matumaini yao kwa Mungu na kuamini Mapinduzi watashinda lazima.
Mapinduzi ya Zanzibar yalitokea mwaka 1964 ili kumuondoa madarakani Sultani wa Zanzibar na serikali yake, iliyoundwa hasa na Waarabu, na hatimaye kuweka uongozi mikononi mwa Waafrika chini ya Kiongozi wake Rais wa Kwanza wa Zanzibar Jemedar Hayati Abedi Amani Karume.
Kwa mujibu wa historia zinasema haikuwa kazi rahisi kufanyika kwa mapinduzi hayo,zilitumika jitihada kubwa na mioyo ya kizalendo hadi kufanikisha azma yao .
Wazanzibar waliteswa na kunyanyaswa huku wakinyimwa haki zao muhimu ikiwemo elimu nakuuzwa kama bidhaa (Biashara ya uatumwa)na manyanyaso mengine mbalimbali waliokumbana nayo kipindi hicho cha kabla ya uhuru.
Wakoloni walifahamu umuhimu wa elimu katika kuleta maendeleo ya mtu binafsi na Nchi ,hivyo kwa makusudi waliamua kuwakosesha Wafrica elimu hio ili wasiweze kupata maarifa .
Mnamo mwaka 1890 mfumo wa elimu ya kimagharibi ulianzia hapa Nchini na skuli ya mwanzo iliyoanzishwa ilijulikana kwa jina la Sir Euan Smith Madressa.
Skuli hio ilianzishwa kisiwani humo na jamii ya Wahindi ili kuwapatia elimu watoto wa jamii yao pekee.
Hadi kufikia mwaka 1907 utawala wa kifalme wa kiarabu nao ulianzisha skuli ya jamii yao tu ,na mwka 1920 utawala wa kingereza ulianzisha skuli nazo pia walisoma watu wenye asili ya kihindi na kiarabu .
Watu hao wenye asili hizo mbili nilizozitaja hapo juu walipangiwa kupatiwa elimu ya msingi na sekondari kwa muda wa miaka 12.
Kwa upande wa watu wenye asili ya Kiafrika ambao ndio wengi walipangiwa miaka minne tu ya elimu ya msingi, ambapo bado wazawa waliendelea kukosa elimu zaidi kutokana na ubaguzi uliovuka mipaka uliokua ukifanywa na watawala(Wakoloni).
Jambo la Kufurahisha baada ya Mapinduzi ya Zanzibar ya1964 Rais wa kwanza wa Zanzibar Hayati Abedi Amani Karume alitangaza elimu bila malipo kwa Wazanzibar wote bila kujali ubaguzi wa rangi kabila au dini.
Hiyo ilikua ni September 23 mwaka 1964 ndipo alipo tamka elimu itatolewa bure kabisa kwa matabaka yote na hapoo sasa ndipo wazee wetu waloiponza kupata mwangaza wa elimu.
Katika kuelekea kilele cha kusherekea miaka 60 ya Mapindizi ya Zanzibar tunaishukuru sana serikali ya mapinduzi ya Zanzibar kwani Kwasasa kuna skuli nyingi za ghorofa na zakisasa ,wanafunzin wanajufunzia katika sehemu nzuri na zenye utulivu wa kujifunzia.
Pia kuna vyuo nyingi vimezishwa vya elimu ya juu ambavyo vinatoa fani mbalimbali hapa hapa Zanzibar (Unguja na Pemba )na vinachukua wanafunzi kutoka nchi nyengine wanao amua kuja kujifunza Zanzibar.
Wizara ya Habari ,vijana ,Utamaduni na Michezo Imeanzisha vyuo vya mafunzo amali kwa vijana unguja na Pemba ili kuona jinsi gani wanayaenzi ya kuyatukuza Mapinduzi kupitia elimu .
Kwa upande wa Pemba chuo kimoja kimeshakamilika na kimeanza kutoa mafunzo yake ,kipo Weni Wilaya ya Wete Mkoa wa kaskazini Pemba.
Chuo hicho kinatoa kozi na fani mbalimbali zikiwemo ushonaji,kujifunza lugha mbalimbali ,utengezaji wa mabatiki,uchumi wa bluu pamoja urembo.
kupitia Miaka hii 60 ya Mapinduzi ya Zanzibar serikali imeweza kumkomboa kijana wa Kiafrika kwa kujifunza fani mbali mbali ili aweze kujiajiri mwenyewe.
Moja ya Kumbukumbu ya Hotuba ya Raisi wa kwanza wa Serikali ya mapinduzi ya Zanzibar hayati Abedi Amani Karume
aliwataka vijana kuwa wazalendo wa nachi yao,huku akiwakumbusha kuwa serikali yao itaendeshwa na vijana hao wazawa.
Aidha Aliwasisitiza vijana kujifunza fani mbali mbali zitakazowapelekea kujiajiri wenyewe na sio wote kutegemea ajira kutoka Serikalini.
“Huwezi kuwa mwananchi mpaka uwe na uchungu wa nchi ,huwezi kukaa pekeako ukajua uchungu wa nchi na isipokuwa utajua sehemu tu sio wajibu wako ,ili kufahamu wajibu wako nilazima uchanganyike na mwezio ujifunze”Alihimiza.
Aidha aliwasisitiza vijana ,wafanye kazi za mikono alieleza kuwa kuna skuli ya technical secondary school.skuli hiyo ilikuwa inawafunza vijana walioshindwa kuendelea na darasa la 8 kazi za mikono
Ni ukweli uliowazi kuwa Kiongozi wetu huyo alikuwa na uwezo mpana wa kufikiria na kulitakia mema taifa letu la Zanzibar kwa kupitia vijana ambao ndio tegemeo la Taifa.
Pamoja na kuwa Tulimpoteza Jemedari wetu huyo lakini maneno yake bado yanaishi na yanafanya kazi kupitia vyuo hivi tunavovianzisha.
Wizara ya habari vijana Utamaduni na Michezo ili kuhakikisha inawawezesha vijana pamoja na kuwajenga uwezo katika masuala mbalimbali ya elimu ujuzi na fursa ya kujiajiri imejenga vituo vya mafunzo kwa vijana ambavyo vitawajengea uwezo katika fani mbalimbali kwa lengo la kujikwamua kiuchumi na kupunguza utegemezi wa ajira kutoka serikalini.
Lengo kuu la mafunzo nikuweza kuwasaidia vijana kwa kuwapatia mafunzo na ujuzi utakaowasaidia katika fani za uongozi ,stadi za maisha stadi za kazi ujasiriamali kuzitambua fursa na mafunzo mengine yanayohusu ustawi wa jamii.
Vituo hivyo vimejengwa unguja na pemba.kituo cha weni pemba ni mfano mzuri wa miongoni mwa vituo hivyo
kituo hicho kina fani mbalimbali ambazo nyengine tayari zimeanza na nyengine bado,Mafunzo hayo ni fani ya uzungumzaji wa lugha za kigeni kwa muda wa miezi 6,ufugaji wa kuku wa kisasa ,mafunzo ya utotoleswaji wa mayai kwa njia ya kienyeji,mafunzo ya ufugaji wa mazao ya baharini.
Mfunzo ya ukulima , mengine ni utengezaji wa vijora na batiki,utengenezaji wa sabuni mbalimbali .,mafunzo ya utengezaji wa perfume na poda ,mafunzo ya ushonaji, kufuma na kudarizi,uchoraji na usarifu wa vitu mbalimbali .
Mafunzo hayo yalianza tarehe 1/11/2023 na yatakua endelevu kwa vituo vyote,mafunzo hayo yatakuwa yanaendeshwa na kusimamiwa na wizara ya habari kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa vijana zikiwemo tasisi za serikali, tasisi binafsi na NGos za vijanaa.
Aidha Mafunzo hayo yatakuwa niyamuda mfupi na kwa kijana yoyote aliyefikia umri wa miaka 18,Pia kutatolewa vyeti kwa wahitimu wa mafunzo hayo .
Said Muhamed Ibrahim ni mmoja wa wanafunzi wa kituo cha mafunzo ya vijana weni ambapo aliishukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kujenga kituo sahihi kwa vijana ambacho kitaweza kuwasaidia mbeleni.
Alieleza fani hizo zinazotolewa katika kituo hicho zitaweza kuwasaidia vijana siku za mbele katika kujikwamu kujiajiri na kujikwamua kiuchumi,hii tunamini nikwasababu serikali imetujali na kutupenda.
“Tunauwezo wa kufanya mengi baada ya kutoka hapa kwasababu kila tunachofundishwa tunafundishwa katika Nadharia na vitendo”Alifahamisha Said.
Aliendelea kusema malengo yake ya baadae baada ya kutoka kituoni hapo nikuwa mwalimu kwa wengine ,hivyo kuwasahauri vijana wengine kuweza kujiunga na chuo hicho na kuacha kukaa maskani na kufanya mambo maovu.
Pia Alimpomgeza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk Hussein Ali Mwinyi kwa kuendeleza na kusimamia Amani ya nchi na kuwaamini vijana kwa kuwapa fursa mbalimbali za kuweza kujiarijiwenyewe kwa lengo la kulisongesha taifa mbele.
Aidha Mwalimu wa Mafunzo ya Urembo katika chuo hicho alisema katika miaka hii 60 ya mapinduzi Zanzibar tumeona mambo mengi mazuri yanayoweza kumfanya kijana aweze kujiariji na kujikwamua kimaisha.
Alisema hapo awali suala la urembo lilichukuliwa kama jambo geni lilikua halina heshma katika jamii na nikinyume cha maadili ya mzanzibari, kupitia Awamu hii ya 8 chini ya uongozi wa Dk HUSSEIN ALI MWINYI tumeona kwa vitendo jinsi mambo yaliyobadilika .
“Sasahivi urembo unafunzwa madarasani tena kupitia kituo cha Serikali,hii ni moja kati ya Faida za Mapinduzi yetu Matukufu ya Zanzibar Kusema lakweli hata gharama inayolipwa nawanafunzi hapa ni nafuu ambayo kila mwananchi unauwezo wa kumudu gharama hizo.” Alisema Mwalimu huyo.
Mratibu idara ya Vijana Wizara ya Habari Vijana Utamaduni na Michezo Ali Mussa Bakari Alisema sera ya vijana inaoesha kuwa vijana ni suala mtambuka .
Alisema katika utekelezaji wa ilani ya chama cha Mapinduzi 2020/2025 ambayo inasema vijana wapatiwe mafunzo ya weledi na ujuzi wa kujifunza ili kuona haawachwi nyuma katika kufikia malengo yao.
Aidha mratibu huyo wa vijana alimpongeza rais mwinyi kwa kuweka mazingira wezeshi kwa vijana kujipatia fursa za kujiendeleza kielimu na kuwashsauri vijana kuchangamkia fursa hizo kadiri ya zinavyotolewa kwa mustakbali wa maisha yao na mustakbali wa taaifa kwa ujumla.
Kwa Upande wake Afisa Mdhamini Wizara ya Habari Vijana utamaduni na Michezo Mfamau Lali Mfamau katika ufunguzi wa kituo hicho cha mafunzo kwa vijana weni alisema anamatarajio makubwa kwa vijana watakaomaliza kujifunza katika kituo hicho watakuwa vijana bora na wapambanaji watakaokuwa mfano mkubwa kwa wenzao.
Alisema Rais wetu Dk Hussein Ali Mwinyi na Rais wa Tanzania Dk Samia suluhu hasana wanaimani kubwa na vijana ,hivyo tujitajhidi kuitunza Imani hio isijekuondoka na tuwaminishe kwa vitendo .
Aidha aliwasihi vijana kukitumia vizur kituo hicho ili kiwasaidie,kwanikuna fursa nyingi za kuwasaidia vijana kujiendeleza na kujikwamua na umaskini.
Pamoja na hayo aliwahidi vijana kuwapa mashirikiano bega kwa bega huku akisisitiza fursa yoyote itakayotokezea basi atahakikisha inawafikia vijana hao.
Yote kwa yote ,Tunakila sababu na wajibu wa kuyalinda,kuyapigania,kuyatetea kwa maslahi ya Taifa Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ya January 12/ 1964 na kuwakemea wale wote wanayoyabeza mapinduzi hayo na kuwabeza viongozi wetu wapendwa wanaofanya jitihada kubwa kutuletea na kutuendelezea mambo haya makubwa kwa maslahi ya watu wake.
MWISHO.
Comments
Post a Comment