TRA MKOA WA KIKODI YATOA MSAADA WA VIFAA HOSPITALI YA WILAYA KINYASINI WETE, WIZARA YATOA UJUMBE HUU.
NA- AMINA AHMED, PEMBA. minnah1202@gmail. com.
KAMISHNA wa Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA amewataka wananchi kisiwani Pemba Kuendeleza harakati za ulipaji wa kodi ili kuisaidia serikali kutekeleza miradi mbali mbali itakayitumiwa kwa na wananchi pamoja na kusaidia kutekeleza huduma nyengine muhimu za kijamii.
Wito wa kamishna wa mamlaka hiyo umetolewa kwa niaba yake na kaimu naibu kamishna wa huduma za kiufundi wa mamlaka hiyo Venance alipokuwa akizungumza na wananchi pamoja na watendaji wa hospitali ya wilaya kinyasini Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba katika Ghaflaya kukabidhi vifaa tiba pamoja na Dawa kwa hospitali hiyo ikiwa ni muendelezo wa wiki ya kurejesha shukurani kwa mlipa kodi .
Amesema iwapo wananchi wataendelea kuwajibika ipasavyo katika ulipaji kodi malengo yaliyowekwa na serikali ya utowaji wa huduma bora kwa wananchi yataweza kufikiwa.
Aidha amesema kuwa lengo la kukabidhi msaada huo wa vifaa tiba pamoja na dawa ni katika kuwashukuru wananchi ambao ndio walipa kodi zinatumika kusaidia upatikanaji wa huduma pamoja na uimarishaji wa maendeleo.
Nae Afisa Mdhamini wizara ya Afya Pemba Khamis Bilali Ali ameishukuru mamlaka hiyo kwa kuendelea kuunga mkono juhudi za serikali ambapo amesema kuwa vifaa hivyo vilivyotolewa vitatumika kwa walengwa na malengo yaliokusudiwa.
Akitoa neno la shukurani mara baada ya kukabidhiwa vifaa hivyo Daktari dhamana wa hospitali hiyo Ramadhan Faki Ali ameziasa taasisi nawadau wengine kuendelea kuiga mfano wa kzalendo ulioneshwa na TRA kwa kujitokeza kusaidia vifaa tiba pamoja na dawa kwa vile ni jambo linalohitajika kila siku kwajili ya matumizi yake kwa wananchi.
Miongoni mwa vifaa vilivyokabidhiwa ni Pamoja na Mashuka 50, Nepi za watoto, na watu wazima, Nguo za Madaktari pamoja na Dawa mbali mbali.
Comments
Post a Comment