UDHALILISHAJI UNAVYOSABASISHA WATOTO KUATHIRIKA KISAIKOLOJIA KATIKA JAMII HAPA ZANZIBAR
NA SALMA AMOUR, UNGUJA.
KWA MIAKA mingi, tunashuhudia watoto ndio waathirika wakubwa wa vitendo cya ukatil wa kijinsia, hali inayoleta taswira ya kupata idadi kubwa ya watoto walioatharika kisaikolojia kwenye Jamii na hata katika Taifa Kwa ujumla
Wataalamu wa afya ya akili wamekiri kuwa, tatizo la udhalilishaji kwa watoto linaweza kusababishia msongo wa mawazo hivyo kukabiliwa na tatizo la afya ya akili.
Chama Cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania, Zanzibar ni moja ya taasisi inayotoa elimu ya saikolojia kwa familia zinazokabiliwa na tatizo la udhalilishaji wa kijinsia.
Kwa mujibu wa takwimu kutoka mtatwimu mkuu wa serikali takwimu za ukatili na udhalilisha wa kijinsia hutoa taarifa za idadi ya matukio yaliyotolewa aina ya waathirika na hali ya waathirika Baada ya ukatili na udhalilisha wa kijinsia muda wa matukio yalipotokea na wafanyakazi wa matukio.takwimu hizo hutoa taarifa kuhusu matukio amvbayo yameainishwa .
Idadi ya watoto waathirika wa matukio ya ukatili na udhalilisha wa kijinsia Kwa mwezio wa Septemba 2023 yamepungua Kwa asilimia 19.7 kufikia matukio 122 Kwa miezi wa Septemba kutoka 152 Kwa mwezi wa Septemba 2022 .amvao
Watoto wenye umri wa 15 hadi 17 wameripotiwa kuwa na idadi kubwa ya matukio ambapo matukio 44 sawa na asilimia 36 ya matukio yote ya watoto yalioripotiwa ikifuatiwa na umri wa 11 hadi 14 ambapo ni 39 sawa na asilimia 32.0
Katika tukio la ubakaji Kwa wasichana mwezio agosti walikuwa 73 mwezi Septemba walikuwa 52 na upande wa wavulana katika upande wa wavulana katika mwezi agosti tukio la ubakaji hakuna hatamoja lililoripotiwa na mwezi Septemba pia hakuna hata Moja.
Tukio la kulawiti Kwa wasichana ambao ni waathirika mwezi agosti hakuna na katika mwezi wa Septemba pia hakuna tukio ,na wavulana katika matukio ya kulawiti mwezi agosti ni 23 na Septemba ni 15 .
Na katika tukio la kulinganisha Kwa wasichana mwezio agosti ni 5 na Septemba ni 5 na wavulana mwezi wa agosti hakuna tukio lolote na tukio la kuingiliwa kinyume na maumbile.
Hata hivyo matukio ya kutoroshwa Kwa upande wa wasichana mwezi agosti kulikuwa na matukio 10 na Septemba matukio 11 na wavulana agosti hakuna tukio na Septemba pia hakuna tukio lolote lililoripotiwa.
Katika matukio ya shambulio la aibu au kashfa Kwa wasichana mwezi agosti ni 10 na mwezi Septemba ni 14 na wavulana mwezi agosti hakuna na Septemba ni 2
Aidha Katika matukio ya shambulio Kwa upande wa watoto wasichana ni 11 mwezi wa agosti na mwezi wa Septemba ni 11 na Kwa upande wa wavulana mwezio agosti ni 11 na mwezi Septemba ni 12.
Hivyo basi jumla ya matukio Kwa watoto waathirika waliofanyiwa ukatili na udhalilisha wa kijinsia baina ya mwezi agosti 2023 na Septemba 2023 Kwa watoto wasichana na mwezi agosti ni 109 na mwezi Septemba ni 93 na Kwa wavulana jumla ya matukio katıka mwezi wa agosti ni 34 na mwezi wa Septemba ni 29
Kwa mujibu wa takwimu hizo, endapo jamii itawatenga, kuwatolea maneno mabaya au kuwakosa elimu ya ushauri nasaha mapema, watoto hao wanaweza kuathirika kisaikolojia.
WATU WA DAWATİ WANAWASAİDİAJE WAATHİRİKA
Vilevile Mkuu wa Dawati la Jinsia ya Watoto Inspector Mohammed Mwadini Alisema kuna hasara mbalimbali zinatokea ikiwepo mtu amefanyiwa Vitendo vya Udhalilishaji na kukaa kimia ikiwemo kukosa haki yake ya Msingi.
" Jambo hili la Udhalilishaji linakua lishabadilisha mfumo wa maisha ya watu hususan watoto ambao ndio wanategemewa kuwa ni nguvu ya Taifa halo baada
İnatuwia vigumu sana kupata ushahidi wa kudhibitisha kuwa watoto wamefanyiwa ukafiti wengi wanaripoti baadae ambapo ni ngumu kuthibitisha kuwa tukio vimete deka
Tunaiomba jamii ielewe kuwa kama Kuna tukio lolote la aina him Basi wameze kuwafikiwa hospital Kwa haraka Ili waugizi na madaktari waweze kuwapatia vipimo ili Kujua Afya ya mtoto inavyoendelea pasipo kupata maambukizi kwa urahisi, vilevile anaweza kuendelezwa kufanyiwa vitendo hivyo kutokana na ukimia wake na kupelekea kuathirika kisaikolojia zitakazomfanya mtoto kushindwa hata Kufanya vizuri Katika masomo
Pia alisema Licha ya hasara, kuna faida ambayo anapata Muhanga endapo akitoa tarifa mapema ikiwemo kukingwa na maradhi mbalimbali ikiwemo Ukimwi.
"Akiwahi kutoa tarifa Mapema atapelekwa hospital kwa ajili ya kuangaliwa Maradhi mbalimbali ikiwemo Ukimwi ndani ya Masaa 72 kuna dawa ambazo atapatiwa kwa ajili ya kumkinga na maambukizi pamoja na Ujauzito.vilevile inakuwa rahisi kupatikana kwa Ushahidi katika Sehemu ya tukio".alisema
Pia alisema Sababu Mbalimbali zinazopelekea kuchelewa kuripotiwa kesi hizo ikiwemo kuwepo kwa vitisho,wazazi kutochukua hatua ya kuripoti kutokana na aibu.
Sambamba na hayo alisema wanatoa elimu ya kisaikolojia endapo mtu amefanyiwa vitendo vya Udhalilishaji.
Hivyo amewaasaa Jamii kutofumbia macho vitendo hivyo kwa ajili ya kusaidia kumuokoa Muhanga pamoja na kuwasaa watoto kumueleza mtu yoyote wa Karibu yake ikiwemo walimu,majirani na kueza kumsaidia pale ambapo amefanyiwa vitendo hivyo.
WAZAZI NA WALEZI WANAVYOLIZUNGUMZIA SUALA LA UDHALILISHA KWENYE JAMII.
Kulingana na takwimu hizo makala haya imebahatika kuzungumza na wazazi wenye watoto waliofanyiwa vitendo vya udhalilishaji, ambapo walisema kwa miaka 10 ijayo watoto wengi Zanzibar watakuwa na tatizo la kisaikolojia kutokana na kukosa elimu ya ushauri nasaha mapema.
Mashaka khamis mkazi wa shehia ya darajabovu alisema tangu mtoto wake mwenye umri wa miaka 12, kufanyiwa udhalilishaji wa kijinsia, amebadilika mwenendo wa maisha yake na kumpa wasiwasi mara mara amekua na hasira.
“maumivu aliyoyapata mwanangu tangu siku alipofanyiwa kitendo hicho, amebadilisha tabia zake na maamuzi ya hasira anayofanya” alisema mama.
Alieleza ni miaka miwili sasa, tangu mtoto wake afanyiwe kitendo hicho, bado ametawaliwa na hofu, woga, kwa sababu ya kukosa ushauri nasaha mtaalamu ambae ataweza kumponyesha maumivu hayo ya kisaikolojia anayoyapata.
Alieleza kuwa Mtoto wake hajapatiwa elimu ya saikolojia hata mara moja, ijapokua taarifa za mtoto huyo kufanyiwa udhalilishaji alizipeleka sehemu husika, ikiwemo uongozi wa shehia, kituo cha Polisi na hospitali kufanyiwa vipimo.
Alisema miongoni mwa athari alizopata mtoto huyo ni kukatisha masomo yake ya darasa la 3, mwaka 2022, kutokana na hofu ya watu wake wa karibu na watu anaokutana nao.
Akizungumza juu ya makuzi ya mtoto wake alisema, kabla ya kufanyiwa udhalilishaji alikuwa mchangamfu, alipenda kucheza michezo mingi ya kitoto, sasa imekua tofauti hataki kujichanganya na watoto wala hapendi kucheza.
"Tatizo kubwa linalojitokeza kwa mtoto wangu ni kuchanganyikiwa na kupata hasira mara kwa mara na zaidi anapokumbuka au kutajiwa vitendo vya udhalilishaji" alisema
Akieleza hali ya ufaulu kwa mtoto huyo mwenye umri wa miaka 12, anaesoma darasa la 4, ambae alifanyiwa kitendo cha udhalilishaji alipokua darasa la 2, alisema alikua akipata nafasi ya kwanza darasani lakini kwa sasa anapata nafasi ya 4 katika darasa la wanafunzi 45 hadi 50.
Mtoto mwenye umri wa miaka 12, alikiri kuwa, amefanyiwa kitendo cha udhalilishaji na mjoba wake, miaka 2 iliyopita ambae alimchukua hadi nyumbani kwake, na baada ya tukio alimuacha barabarani, akiwa analia.
Hadi leo mtoto huyo anahofia kupita njia aliyopitishwa na mjomba wake siku ya tukio na pia asiposhikwa mkono na mama yake kumpeleka safari hataki kutoka nyumbani kwao.
Mzazi mwengine, mtoto wake alibakwa akiwa na umri wa miaka 9, alisema utofauti wa tabia za mtoto wake, kwa sasa, anapenda kukaa eneo lenye utulivu, hapendi kujichanganya na watu, pia anapoona wageni hukimbilia chini ya mvungu wa kitanda, kuanza kulia hadi apitiwe na usingizi.
“Kuna siku nilimwambia mwanangu nenda nje ukacheze na wenzako ghafla alikimbia, nilimtafuta kwa muda nilipokuja kumuona amelala chini ya kitata amejifunika mashuka, akiwa analia” alisema mama.
Alieleza hali hiyo ni kutokana na mfanyaji wa kitendo hicho alikua mtu wa karibu kwenye familia, (mjomba) alietoroka Zanzibar na kwenda kuishi Tanzania bara.
Mama huyo, aliomba serikali ya awamu ya nane kuhakikisha watoto waliofanyiwa vitendo vya udhalilishaji wanapatiwa elimu ya saikolojia, ili kuepusha athari zaidi kwa watoto ambao ndio taifa la kesho.
“Kwa mfano kesi ya mwanangu nimezungushwa vituo vyote, leo Mwera, kesho Madema hatimae kutolewa maneno machafu na maafisa wa vituo vya Polisi, mtoto hakupewa elimu na mtuhumiwa kakimbia mwanangu amekosa haki zake” alisema.
MAONI YA JAMII KWENYE SUALA HILI
Fatma mbwana shehe, alisema hali za watoto wanaofanyiwa vitendo vya udhalilishaji zinasikitisha, ipo haja kwa serikali kuangalie namna ya kuwafikia watoto wote waliokabiliwa na tatizo hilo ili kuwaepusha na athari kubwa za kisaikolojia siku zijazo.
Alisema tatizo la saikolojia linaweza kuleta athari zaidi kwa jamii, kwani msongo wa mawazo anaokuwa nao mtoto aliedhalilishwa hujisikia vibaya na mara nyengine kuchukua maamuzi magumu ya kujitoa uhai.
Aidha alisema kuna haja ya serikali kuangalia kwa makini utoaji wa hukumu wa kesi za udhlilishaji, kwani mara nyingi wanyonyge wanakoseshwa haki zao baada ya watuhumiwa kutoa hongo ya pesa kwa wakubwa, na kesi hizo kuishia njiani.
WANAHARAKATI WA MAENDELEA NA KUPINGA UKTiLI WA KIJINSIA
Zaina Abdallah, Mwanasheria kutoka Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania upande wa Zanzibar, TAMWA, alisema kwa mujibu wa sheria ya mtoto namba 6 ya mwaka 2011, inaeleza kuwa mtoto anatakiwa kutunzwa, kulindwa na nyanja nyingi ikiwemo serikali, familia na jamii, hivyo jamii kuendeleza hilo.
Aidha alisema sheria hiyo, inamekua na changamoto ya kukinzana na sheria katika kuutambua umri wa mtoto kuwa ni mika 18, ambapo sheria nyengine imeweka miaka 14, sambamba na kupendekeza uwepo wa skuli za kurekebisha tabia kwa watoto kama ilivyotambuliwa na serikali.
Aidha aliomba serikali kuweka kipengele maalumu katika sheria, juu ya kufanywa ukaguzi wa makaazi ya mtoto anapotaka kupelekwa ili kujiridhisha na kuepuka kumuweka katika mazingira magumu.
"Mapendekezo yangu kwa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Amali Zanzibar kutengeneza muongozo maalumu wa mafunzo ya ziada ili kuwawekea mazingira mazuri katika ulinzi wa watoto wanapokuwa katika masomo ya ziada" alisema.
Akizungumza katika kikao cha kuwajengea uwezo Maofisa ustawi wa jamii 20, kutoka taasisi mbali mbali za Zanzibar, Msimamizi wa mradi wa upatikanaji wa haki, kutoka Jumuiya ya Wanasheria Wanawake Zanzibar (ZAFELA), Mwanaisha Mustafa, alisema kwa muda mrefu sasa watoto wanaopata udhalilishaji wa kijinsia wanakosa huduma ya ushauri nasaha kutokana na kutokuepo mifumo rasmi ya utoaji wa huduma hiyo.
Alieleza tatizo hilo linazidi kukua siku hadi siku kutokana na idadi ya watoto wanaofanyiwa udhalilishaji inazidi kuongezeka hapa Zanzibar, na kuhatarisha afya za akili kwa watoto.
Alieleza jitihada wanazochukua kuhakikisha watoto waliodhalilishwa wanapata elimu ya ushauri nasaha, alisema ni mwaka wa tatu sasa, Jumuiya hiyo inautaratibu wa kuwapatia wanawake na watoto huduma ya saikolojia kupitia wanasaikolojia tofauti.
Akizungumza idadi ya wataalamu inayotumika sasa kutoa elimu hiyo, alisema wanasaikolojia ni wachache sana kuweza kutosheleza mahitaji ya Zanzibar.
Mkufunzi kutoka Chuo cha Taifa cha Zanzibar (SUZA) Nassor Omar, alisema waathirika wa vitendo vya udhalilishaji wanahitaji sana msaada wa saikolojia, jitihada zianahitajika kwa Serikali na wadau wa maendeleo ili kuepusha msongo wa mawazo kwa watoto.
OFISA USHAURI NASAHA
Mwanasikolojia na mshauri nasaha, kutoka jumuiya wa wanasaikolojia na ushauri nasiha Zanzibar, Ramadhan Mohammed Hassan, alisema athari zinazowapata watoto waliofanyiwa udhalilishaji na kukosa ushauri wa kitaalamu (kisaikolojia) pamoja na msongo wa mawazo uliopitiliza.
Alisema elimu ya saikolojia inahitaji kufanyika mapema ili kusaidia kupona kwa haraka mtoto huyo, hivyo wazazi wanatakiwa kuripoti mapema.
Alieza kuwa kwa mujibu wa sheria walizoweka wanasaikolojia kwatika kutoa matibabu, kila muhanga mmoja anatakiwa kuhudumiwa kwa dakika 45 hadi lisaa moja kwa siku, ambapo wanasaikolojia wengi wana uwezo wa kutoa huduma hiyo takriban watu 5 hadi 7 kwa siku kulingana na masaa ya kazi.
Mikakati inayopaswa kutumika ili kuwafikia wahanga wengi ni kutoa elimu hiyo mara kwa mara kupitia vyombo vya Habari, sambamba na kuitaka jamii kuondoa dhana potofu juu ya utolewaji wa elimu hiyo kuoita hospitali mbalimbali za Zanzibar.
Msongo baada ya janga kwa kujirejea jea katika akili yake, na kukosa tumaini la maisha kwa kutamani kuchukua mawazo mabaya, kushindwa kujiamini, kushindwa kuzingatia masomo, kulala kupita kiasi au kushindwa kulala kabisa na kujitenga.
Alisema licha ya elimu ya saikolojia wanayotoa elimu ya tumaini la maisha (kifikra) ili kujiona ni watu wenye thamani kama watu wengine, kuelimisha juu ya tabia za watu wengine, staid za maisha na kuwarudisha skuli watoto walioacha masomo.
Alisema matibabu hutoa kwa njia ya usiri na kuangalia Maendeleo ya watoto hao kila baada ya muda wa wiki moja au wiki mbili.
Akizungumzia mbinu zinazotumika kutoa elimu ya saikolojia kwa familia, vikundi na mtu mmoja mmoja, kwa kufanya tiba ya mazungumzo, kuangalia mabadiliko ya kiakili, kubadilisha tabia kwa kumjenga akili yake katika hya kawaida, michezo, mazingira, ulaji, kazi za vitendo, na mazoezi.
licha ya elimu hiyo kuitoa, mara nyingi muhanga anachukua muda mrefu kurudi katika hali yake ya kawaida.
Aliomba serikali kuengeza nguvu na idadi ya wanasaikolojia kupitia taasisi mbali mbali za serikali na zi sizo za serikali ili kupunguza changamoto zinazojitokeza wakati huu.
OFISA USTAWI WA JAMII
Nae, Afia ustawi Kitengo cha Hifadhi ya Mtoto Idara ya Wazee na Ustawi, Fatma Maulid Haji, alisema wanapopokea watoto waliofanyiwa vitendo vya udhalilishaji na kugundua wamepata tatizo la afya ya akili, hufanya jitihada za kuwapayia ushauri nasaha pia kuwapeleka katika nyumba salama, ili kuhifadhiwa mpaka wanapokuwa sawa kiakili.
Aliwasisitiza wazazi kuwa walinzi kwa watoto wao ili kuepusha kufanyiwa vitendo vya udhalilishaji kwani wanaofanya vitendo hivyo ni watu wa karibu kwenye familia.
DAKTARI WA MAGONJWA YA AKILI
Khadija Abdulrahman, Daktari wa Afya ya Kili Kidongochekundu, alisema miongoni mwa watu waliopata tatizo la afya ya akili, wamekabiliwa na tatizo la udhalilishaji wa kijinsia.
Aidha alisema kwa kiasi kikubwa athari za udhalilishaji zinaweza kuchangia tatizo hilo, jambo ambalo linasababaisha kuongeza idadi ya wagonjwa wa akili hapa nchini.
MKURUGENZI WA IDARA YA MAENDELEA
Mkurugenzi Idara ya Maendeo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Siti Abasi Ali, alisema wizara kupitia kitengo cha Idara inakitengo maalumu cha saikolojia, hutoa elimu hiyo siku hadi siku, ili kurejesha watoto hao katika hali za kawaida.
Alisema katika kuhakikisha wizara inaweka usalama kwa watoto waliodhalilishwa ambao wanaendelea na masomo, wanatoa elimu kwa walimu wa skuli mbalimbali katika matumizi ya lugha zinazopaswa kutumiwa kwa watoto hao ili kuepusha athari zaidi.
Alieleza kuwa elimu ya saikolojia inatolewa bure kws upana zaidi kwenye maeneo mengi kuanzia ngazi za shehia, na maeneo mbalimbali ya kutolea huduma za jamii.
Alieleza kuwa Dira ya mpango wa maendeleo ya Zanzibar ya mwaka 2050, inaeleza kudumisha mfumo ulio sawa na endelevu wa huduma ya afya kwa wote unaofikiwa na wote unaotolewa na wataalamu wa afya wenye ujuzi wa hali ya juu na kuungwa mkono na vifaa vya kisasa vya teknolojia ya matibabu.
KATIBU MKUU WIZARA MAENDELEO YA JAMII
KATIBU Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Zanzibar, Abeda Rashid Abdallah, alisema, serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imelipa kipaumbele suala hilo kwa kutafuta ufumbuzi wa haraka matukio ya udhalilishaji.
Alisema kikawaida wanapokea na kufatilia kesi hizo kwa karibu ili kupata taarifa kamili kwa wahusika wa pande mbili, ili watoto waliofanyiwa vitendo vya udhalilishaji hawapati tatizo la saikolojia, na wafanyaji wasiweze kurudia.
Lakini pia alibainisha kuwa katika kupiga vita suala hilo, serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, imeweka Sheria ya mtoto no.6 ya mwaka 2011, na kubainisha namna gani mtoto anatakiwa kupata malezi pamoja na stahiki zote kama mtoto, sambamba na kulindwa na matendo mabaya ikiwemo vitendo vya udhalilishaji.
Pia njia nyengine inayotumika ni kuwapeleka katika nyumba salama kwaajili ya kupatiwa ushauri nasaha, hadi watakapo rudi katika hali zao za kawaida.
"Serikali imeweka nyumba salama moja ambayo imeanza kutumika mwaka 2017, ambapo mwaka 2021, imetunza watoto 81, mwaka 2022 imetunza watoto 73, kwa sasa serikali inasimamia nyumba hiyo ambapo awali nyumba hiyo ilikua chini ya shirika la AIDS," alisema.
Aidha alisema changamoto inayojitokeza ni kuwakosa watuhumiwa waliofanya matendo hayo, na kusababisha kukosa taarifa kamili, licha ya juhudi wanazochukua.
Alieleza mikakati mengine ya wizara katika kuhakikisha watoto waliodhalilishwa hawapati tatizo la kisaikolojia, alisema Wizara inafanya mapitio ya mpango mkakati wa kupambana na ukatili, kwa wanawake na watoto ili kuona namna ya kuimarisha ulinzi wa mtoto.
Alieleza Mkakati huo utaeleza mueleko wa taifa na mapendekezo yatakayo fanywa na wadau wa masuala ya udhalilishaji, ambapo ifikapo Disemba mwaka huu, wanatarajia kupata miongozo, sera mpya inayokwenda na wakati na mueleko wa nchini
Comments
Post a Comment