UHABA MAAFISA USTAWI JAMII WALALAMIKIWA WADAU WALIA NA SERIKALI.
NA AMINA AHMED MOH'D PEMBA.
WADAU wa kupinga vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia kisiwani Pemba Wameiomba Serikali kuongeza idadi ya maafisa ustawi jamii katika wilaya ili kusaidia kuongeza kasi ya kupambana na changamotoza vitendo vya Udhalilishaji wa kijinsia kwa watoto.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti baadhi ya wadau hao wamesema kuwa kutokana na uhitaji wa watu hao katika kusaidia kupambana na vitendo hivyo utaratibu wa Afisa mmoja katika kila wilaya ni miongoni mwa changamoto inayopelekea kuongezeka kwa changamoto katika kesi za udhalilishaji.
"Wilaya mfano wilaya ya mkoani ina shehia 32 ambazo shehia zote hizo vitendo na kadhia za udhalilishaji kwa watoto zinajitokeza Afisa mmoja tu ndie analazimika kushuhulika haisaidii kuondoa changamoto", Fathiya Mussa Said.
Serikali iliangalie suala hili kuona kwamba ipo haja ya kuongeza idadi ya hawa watu katika wilaya ikiwezekana iwaweke kwa shehia ili kuondoa usumbufu katika kesi za udhalilishaji kwa watoto ".Siti Habibu Muhamed kutoka Shirika la msaada wa kiaheria
Kutokana na umbali ambao wapo maafisa ustawi jamii waliowengi wamekuwa wakibadilisha maamuzi hivyo ni vyema kusogezwa kwa karibu ili Tuweze kupata mashirikiano katika kupambana na vita hii, Alisema Tatu Abdalla Msellem Wanaharakati masuala ya udhalilishaji.
Aidha kwa Upande wake Asha Massoud Salim kutoka kituo cha mkono kwa mkono Chake Chake ameiomba Serikali kuongeza vituo vya ushauri nasihi ili kuondoa athari kwa wahanga kwa kuwashirikisha wadau ambao wataweza kuanzisha vituo hivyo.
Changamoto kubwa iliyopo sisi watu wa mkono kwa mkono ni lazima tufanye kazi na watu wa ustawi wa jamii, lakini kiukweli hawa watu wapo mbali inakuwa ni usumbufu kwa wahanga kuwapeleka katika kitengo chao
Alisema licha ya kutolewa huduma hiyo kwa wahanga wanaothirika lakini bado waliowengi wamekuwa wakishindwa kufika katika kituo hicho hususan n kwa wananchi wanaoishi mbali na kituo hicho.
Maafisa ustawi ni moja kati ya wasimamia miongozo ya utekelezaji wa kutoa huduma za kisaikologia kwa jamii kwa lengo la kupunguza matatizi yanayotokea hususan ni vitendo vya ukatili.
Comments
Post a Comment