HABARI ZINAZOHUSU AFYA YA UZAZI KWA WANAWAKE NA WASICHANA YAJA NA SURA MPYA PEMBA NI BAADA TAMWA-ZNZ KUTAFUTA 40 JUU YA UTOLEWAJI MDOGO WA TAARIFA HIZI.
Na - AMINA AHMED MOH’D , PEMBA. ZAIDI ya Waandishi wa Habari 15 Kutoka vyombo mbali mbali Kisiwani Pemba wamepatiwa Mafunzo ya siku tatu juu ya Afya ya Uzazi ambayo yamelenga kuongeza uelewa juu ya kuandika kwa Ubora na kuelimisha kupitia kalamu zao na kuondosha Changamoto zinazoendelea kujitokeza kutokana na kukosekana kwa Afya na Uzazi kwa Makundi mbali mbali ya wanawake katika Jamii. Akifunga Mafunzo kwa Waandishi hao Afisa Mdhamini Wizara ya Afya Pemba Khamis Bilali Ali amewataka Waandishi hao kuitumia Elimu hiyo iliyotolewa kwa kuandika Habari zitakazoisaidia Kupunguza Vifo vya kina Mama na watoto . Amesema Miongoni mwa vipengele Muhimu ambavyo vinahitaji kufanyiwa kazi na Waandishi wa Habari kufikisha Elimu na Kusaidia Serikali ni Afya ya Uzazi ambayo Wanawake na Wasi...