MRADI WA VIUNGO PEMBA WALETA MAGEUZI KWA WAKULIMA, WASEMA NI CHACHU YA KUKOMBOKA KIUCHUMI.
NA AMINA AHMED MOH’D, PEMBA :0719859184
WAKULIMA wa viungo mboga mboga na matunda kisiwani Pemba wamewataka wananchi kuzitumia fursa kujiinua kiuchumi kupitia fursa za kilimo hicho ambacho kitawaletea tija.
Ushauri huo umetolewa na Wakulima kwa nyakati tofauti huko katika Mashamba yao walipokuwa wakizungumza na waandishi wa habari ikiwa ni ziara maalum ya kuangalia mafanikio kwa wakulima wa mradi wa viungo unaofadhiliwa na umoja wa wa ulaya EU kwa kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar kupitia Wizara ya kilimo na kutekelezwa na TAMWA-Zanzibar, PDF pamoja na Community forest Pemba CFP ikiwa ni mpango Maalum Wa kukuza kilimo " Agri conect".
Wamesema Kilimo Cha Viungo mbga mboga na matunda Ni Fursa Pekee inayoweza kuwakomboa wananchi kiuchumi na kuwawezesha kuwainua Kiuchumi Na kuacha utegemezi.
" Awali kabla sijapata fursa hii ya kuwa mnufaika kulima kilimo hichi cha Viungo, Vanilla na Mdalasini nilikuwa nashindwa kujikimu vizuri kimaisha, lakini sasa naendesha shuguli zangu bila wasi wasi wowote, Kilimo ndio Imekuwa Mafanikio yangu mradi wa viungo umenikomboa, Alisema Salma Hamad Ali Mkulima wa Mdalasini Gando Mkoa wa Kaskazini.
" Mradi wa viungo Umenikomboa na umabadilisha maisha yangu kwa kipindi kifupi sana, Mimi ni mmoja kati ya wakulima wanufaika katika mradi wa Viungo, Nimeongeza uzalishaji wa midalasini zaidi ya 10000, wakati mwanzoni nilikuwa na midalasini miamoja tu ambayo hiyo naishughulikia bila kupata faida wala kujua kudhibiti mabadiliko ya Tabia ya nchi.
"Nina zaidi ya Eka 6 za Midalasini tu, wakati mwanzoni hata kabla ya kuja kwa mradi nilikuwa sijui kuhusu zao la vanilla pia Nimehamasika kulima vanilla na saivi Ninayo mivanilla Zaidi ya elf 5 Shambani kwangu ".
" Nilikuwa sina Elimu sina Taaluma wala sijui jinsi gani nitaendeleza zao la vanilla mradi wa viungo umenitoa kutoka kilimo ambacho sielewi chochote mpka kufika kwenye kilimo cha kitaalamu chenye Tija kwangu, Naendesha Familia yangu, najiptia kipato, naweka hakiba ya kiendeleza shuguli zangu ".
"Tulikuwa Tunapata shida sana kuwafikia wakulima kuwapatia pembejeo za kilimo, kuwapa Elimu lakini mara tu baada ya kuja mradi huu wa viungo Taasisi ambazo zinashughulikia Na kusimamia huu mradi kumerahisisha kuwafikia wakulima wote Waliomo ndani ya jumia mbao ni zaidi ya 800 wanaojishughulisha na upandaji wa viungo kuwapa elimu na mbinu za ulimaji wa kisasa pembejeo pamoja na mbegu " Alisema Sleiman Ali Mfaki mkulima wa Vanilla na Mdalasini ambae pia ni mwenyekiti wa Jumuia ya wakulima wa viungo na mazao (Pemba Spice producer coorperative).
Asha Ali Omar Anasmea kuwa kupitia mradi wa viungo kwa upande wake Hakuwahi kujua nini haswa faida ya Kulima Mazao ya viungo licha ya kulima kwa muda mrefu.
"Nilikuwa naona tu watu wanalima wanapanda na mimi nikawa najitia tu kundini nafanya kama ni mazoea ya kawaida tu napanda pembeni mwa nyumba zetu , lakini Mradi huu ulipokuja tukapewa Elimu tukahamasika na kuanza kutafuta mashamba kwa vile nilikuwa nayo nalima tu Mihogo tukaanza kupanda Midalasini, nimepanda eka kama moja, Na ndani ya hiyo eka nimepanda pia vanilla Miche 150 Faida nimeiyona nasomeshea wanangu, baada ya kuvuna mara ya kwanza, Mara ya pili Nimepata pesa ya Kumlupia mwanagu kusomea udereva, nakata nauza napata kipato nimeanza kujenga nyumba na nafanya shughuli nyengine kupitia kilimo pia ninayo hakiba ambayo naendeleza shughuli za kilimo.
Subira Mkubwa Muhammed pamoja na Ali Khamis Abdalla Ambao wamekuwa wakijishughulisha na kilimo cha Matunda, na Mboga mboga ikiwemo Mananasi, Mapensheni Matikiti,Pili pili boga na matikiti kutoka kijiji cha Kwale Mpona Wamesema kuwa mradi mara baada ya kuwa wanufaika wa mrafi huo Kasi ya maendeleo ya kiuchumi na uzalishaji imeongezeka mara mbili zaidi ya ilivyokuwa awali kabla ya kuja kwa mradi huo.
Tulikuwa tunaanika Mdalasini baada ya kuchuna kwenye barabara unaingia michanga mavumbi, siku nyengine unaroa Lakini kupitia Mradi huu tunatumiaSolara draya kukaushia Kwa haraka na rahisi Zaidi . ni mafanikio makubwa kwa upande wetu.
"Nimetia umeme tumeuvuta mbali sana ushawishi kwa serikali umeongezeka Tumekuwa tukitumia fursa ya mikopo inayotolewa na serikali bila kipingamizi, Kilimo chetu kwa sasa tunatumia umwagiliaji wa dripu, Tumeajiri vijana ajira za Msimu na wao kutusaidia wanajipatia kipato Tumekuwa shamba darasa kwa wakulima wengine mbali mbali kupitia Mradi wa viungo watu wanaiga kutoka kwetu namna ya kulima kilimo hichi .
" Tayari kupitia Mradi huu wa viungo Tumeanza kujenga Nyumba fondesheni ile mnayoiona, Soko leru la bidhaa ni la kila siku tunaingiza na faida inapatikama kubwa sitaki kuitaja hapa lakini inajitosheleza Tunapata kuweka kuendesha gharama za kilimo, na nyengine inabakia kiasi ambacho hata mradi umalizike kesho b hihasi hatutorudi nyuma kuendeleza kilimo.
Nae Kwa Upande wake Mkunga Hamad Sadala Mkulima mnufaika Mradi wa Viungo Vitongoji Wilaya ya Chake Chake Ambae anajishugulisha na kilimo cha Matunda na mboga mboga Ameseeleza kuwa Faida mbali mbali amabzo amezipata kupitia kilimo cha mboga mboga kupitia mradi wa viungo Amefanikiwa kuhamasisha vijana kuwekeza katika Kilimo, sambamba na kujipatia mtaji mwengine wa kuendeleza shughuli zake ikiwemo Mifugo Ikiwemo mbuzi pamoja na kuku.
Akizungumza kuhusu Maendeleo kwa wakulima hao Afisa Viungo Kupitia Mradi wa Viungo unaosimamiwa na Agri Conect upande wa Pemba Haziel Gilbert Sezero amesema lengo la kushughulika na wakulima wa mazao ya viungo matunfa na mboga mboga , ni kusaidia kupunguza changamoto mbali mbali ambazo zilikuwa zinawakabili na kupelekea kurudi nyuma kimaendeleo.
"Mradi huu umekuja kusaidia kupunguza changmoto za wakulima wa mazao ya viungo, walikuwa wakikabiliwa na changamoto mbali mbali ikiwemo eneo la kukaushia Mazao yao kipindi cha mvua, ambayo yalikuwa yakiharibika kutokana na kupata Sumu Kuvu, Kwaio baad ya kuona hivyo Mradi ulisadia upatikanaji wa Solar Draya ambayo , Lakini pia Changamoto ya Mbegu lengo ni kuoma wakulima Wetu wanapata tija na kipato kupitia kilimo jambo ambalo limefanikiwa kwa kiasi kikubwa.
Ziara hiyo ya waandishi wa habari kutembelea wakulima wanaufaika Mradi wa viungo pemba Imeandaliwa na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania TAMWA Zanzibar, ikiwa ni utekelezaji wa Mradi wa Viungo ambao unatekelezwa kwa mashirikiano kati ya Tamwa Zanzibar, PDf, CFP kwa ufadhili wa Umoja wa Ulaya EU kulitia mpango wa Agri conect ambapo zaidi ya Mashamba ya wakulima 5 kutoka maeneo mbali mbali ya kisiwa hicho yametembelewa na Waandishi hao
.
Mwisho.
Comments
Post a Comment