ZAPDO, ZALHO WAFIKA WINGWI KUZUNGUMZA NA WANANCHI JUU YA HAKI ZA WATU WENYE ULEMAVU WA AKILI.
Wananchi Shehia ya Wingwi Mtemani Wilaya ya Micheweni Mkoa wa kasakzini Pemba Wameiomba Jumuia ya watu wenye Ulemavu wa Akili Pamoja na Shirika la Msaada wa kisheria kuwasaidia kulipatia ufumbuzi suala la kupatikana Hospitali maalum kwa wagonjwa wa Akili sambamba na hi kuwawekea Madakatari maalumu ambao Watakuwa na Utaratibu Wa kuwatembelea na kuwapatia Huduma za afya na Matibabu wagonjwa Wa Akili waliopo katika Maeneo mbali mbali kisiwani Pemba.
Wametoa Ombi hilo leo Walipokuwa wakizungumza Katika Mkutano Maalum ulioandaliwa na Jumuia ya Watu wenye Ulemavu wa Akili Zanzibar pamoja Shirika la Msaada wa kisheria huko Wingi Jambo nia.
Wamesema Licha ya Kuwepo kwa Idadi kubwa ya Watu wenye Ulemavu wa Akili wanaozurura na kuzagaa katika Maeneo mbali mbali kisiwani Pemba Lakini bado kumekuwa na Changamoto ya Kukosekana na Hospitali hiyo pamoja Madakatari wanaotembelea majumbani kuwapatia huduma Za matibabu jambo ambalo linapelekea kuhatarisha Usalama wao, sambamba na Kukosa Haki zao mbali mbali .
"Wagonjwa Wa Akili wapo kwa idadi Kubwa kisiwani Pemba, Hata Umtafute Daktari Umwambie mimi nina mgonjwa siwezi kumfikisha Hospitali njoo mara moja Unisaidie Humpati, Unaweza ukampata ukimlipia Gari au nauli, Mimi ninae Mgonjwa ndani mwangu mtu mzima Hajajapo Daktari kuja kumuona na Kila siku naenda Pale Hospitali kununua Dawa lakini hata ile hamu ya kutaka kujua tu anaendeleaje hawaulizi Tunaomba Wizara ya Afya Itusaidie hili" Alisema Shoka Hamad Abeid Mkaazi wa Wingwi.
"Kutokana na kukosa Uelewa Tunalazimika kuwaacha tu wazurure Mimi mwanangu ni mgonjwa wa Akili ana miaka 10 nilimuandikisha Lakini alikuwa umo darasani hakai mara anaingia madarasa mengine Hatulii niliamua nimkatishe, anazurura tu jumuia ya watu wenye ulemavu wa akili, Shirika la Msaada wa kisheria pamojana Serikali Litusaidie Kupata uelewa Huenda tunawakosesha haki zao kutokana na kushindwa kujua vipi tunawasaidia kisheria kuzipata izo haki" Alisema Mkongwe Khamis Said Mama Mweye mtoto ambae anaulemavu wa Akili Wingwi Jambo Nia.
Aidha Wananchi hao Wameiomba jumuia na Shirika hilo kuendelea Kujitambulisha kwa wananchi Ili kuweza kujulikana vyema na kuwarahisha kufikisha changamoto Nyingi zinazowakabili watu wenye Ulemavu wa Akili na nyengine mbali mbali zinazowakabili zinazohitaji msaada wa kisheria.
Wakizungumza Katika Mkutano huo Mratibu wa Jumuia ya watu wenye Ulemavu Pemba Halfan Amour Muhammed Pamoja Siti Habib Muhammed Kutoka Shirika La Msaada wa Kisheria Zanzibar Ofisi ya Pemba Wamesema Wataendelea kusimamia , kushawishi, pamoja na kutetea Upatikanaji wa Haki za Msingi kwa Watu wenye Ulemavu wa Akili kwa Wadau wa Maendeleo pamoja na Serikali.
"Watu wenye ulemavu wa akili wamekuwa wakizurura huku wengine wakiitwa majina mabaya wengine wakifanyiwa vitendo viovu lakini Haki juu yao haipatikani, kutokana na kukosa Watetezi Jumuia ya Watu wenye ulemavu wa Akili tutaendelea kuwa bega kwa bega kuona haki wanapata haki sawa kama walivyo watu wengine" Alisema Mwenyekiti huyo.
"Watu wenye Ulemavu wa Akili wanastahiki kua na haki sawa kama Walivyo binaadamu wengine, Haki ya Kuishi, kulindwa dhidi ya Majanga ikiwemo udhalilishaji, Haki ya Matibabu kushirikishwa Haki ya Kusoma na nyengine nyingi Zote hizi haziwezi kupatikana iwapo wazazi na walezi hatutokuwa tayari kuwasaidia".
"Tunatakiwa tuzidishe Mara mbili Usimamizi wa Kuzitafuta haki za Watoto wenye ulemavu wa akili Shirika la Msaada wa kisheria tutaendelea kutoa mashirikiano Muda na wakati wowote hivyo wananchi muitumie fursa hii katika kuona watu wenye ulemavu wa akili na wao hawaachwi nyuma katika kupata haki na Maendeleo .
Elimu juu ya Upatikanaji Haki za Watu wenye Ulemavu wa Akili, Huduma Za Msaada wa kisheria ni Miongoni mwa Mada Zilizotolewa kwa Wananchi waliohudhuria katika Mkutano huo Maalum Uliondaliwa Kwa Wananchi hao Huko katika Kijiji cha Jambo Nia .
Comments
Post a Comment