MARADHI YASIOAMBUKIZA UGONJWA WA SINDIKIZO LA DAMU (PRESSURE).
NA, ABDALLA AMOUR MBAROUK - PEMBA.
PENDA kujua usiyo yajua na usidharau usilo lijua , elewa uzima hauchoshi Wala haukinaishi lakini Sindikizo la Damu ni ugonjwa unaoweza kukatisha maisha kama hautakua muelewa wa ugonjwa huo .
Sindikizo la Damu (hypertantion) ni matokezeo ya msukumo wa nguvu wa wdamu unatoka kwenye moyo kuelekea sehemu nyengine za mwili ambao mskumo huo unakua sio wa kawaida .
Moyo ni kiungo muhimu na chenyekubeba kazi nyingi mwilini hivo kinapo pata hitilafu kama kushindwa kusambaza Damu kwa kiwango kinacho hitajika kwenda sehemu nyengine za viungo vya mwili kwa kuziba au kubana kwa baadhi ya mishipa ya Damu (blood versels) kutokea kwa Hali kama hiyo ndio husababisha ugonjwa huo wa sindikizo la Damu.
Kwa mujibu wa vipimo vya kitaalamu mwanadamu aliye katika Hali ya uzima wa kawaida kiafya anatakiwa awe na kiwango Cha 110 Hadi 140/80-90 Cha Damu na kuzidi kuanzia 140 na kuendelea mtu huyo atahesabiwa kua ni mgonjwa wa sindikizo la Damu Yani (hypertantion).
Ugonjwa wa sindikizo la Damu maranyingi hugundulika wakati wa kufanyiwa vipimo vya kiafya na mtaalamu wa Afya kutokana na kua maradhi ya yasio ambukiza hua na dalili zenye kufanaan na Sindikizo la Damu ni aina ya maradhi yasioambukiza yaani NCDs.
Kutokana na kua na Dalili shirikishi jamii inashauriwa kua na utamaduni wa kupima Afya mara kwa mara Ili kujua Hali zao na kuchukua hatua na tahadhari wakati watakapo bainika kupata ugonjwa au watakapo bainika kua Salama.
Akitoa ushuhuda wa namna ya ugonjwa huo unavo tokea Dr Omari Mohammed sleiman ambaye ni msimamizi wa kitengo Cha maradhi yasio ambukiza NCDs Zanzibar wakati akizungumza na mwandishi wa taarifa hii amesema wapo baadhi ya wananchi aliwo wahi kuafanyia vipimo wakiamini ni wathirika wa maradhi mengine na wengine wakiamini wapo Salama lakini baada ya vipimo walibainika kua na ugonjwa wa sindikizo la Damu.
"Mimi ni daktari mzoefu nilisha wafanyia vipimo watu wengi na wengine walikua wanakuja kupima wakiamini wapo Salama na wangine walikuja na dalili za maradhi mengine lakini tuliwabaini Wana sindikizo la Damu"alieleza Dr Omar.
Aidha Dokta Omar aliwashauri wananchi kuvitembelea vituo vya Afya kupata vipimo vya kiafya nakusema "nyakati hizi maradhi yasio ambukiza yamekua mengi na dalili zake hazijitokezi mapema na nyengine ni za kawaida sana kutokana na mfumo wa maisha ya watu" alishauri Dr huyo.
Kila jambo lina sababu zake na nyengine hua ni zamoja kwa Moja lakini kwa ugonjwa wa sindikizo la Damu imeelezwa hakuna sabuabu za Moja kwa Moja lakini mara nyingi inaweza kutokea mara baada ya matokezeo ya maradhi mengine kama vile kisukari,msongo wa mawazo au fazaa , presha, ujauzito na magonjwa mengine mengi hivo ni sawa na kusema waathirika maradhi hayo na yasio kua hayo wana uwezekano mkubwa wa kuathirika na ugonjwa huu ukilinganisha nawale ambao sio wahanga wa magonjwa haya.
Mwisho
Comments
Post a Comment