MWENYEKITI WA TAASISI YA MAISHA BORA FAUNDATION MARYAM MWINYI AWAHIMIZA WANANCHI KUSINI PEMBA UMUHIMU WA KUFANYA MAZOEZI KUIMARISHA AFYA KUEPUKANA NA MARADHI YASIOAMBUKIZA.
NA AMINA AHMED MOH’D PEMBA
MWENYEKITI wa Zanzibar Maisha Bora Faundation ambae pia ni Mke wa Rais wa Zanzibar mama Maryam Mwinyi Ameongoza matembembezi maalum ya kuhamasisha umuhimu wa kufanya mazoezi kwa Wananchi Mkoa wa Kusini Pemba yalioanza eneo la Kiwanda cha Makonyo wawi Chake Chake na Kumalizia katika Viwanja vya Gombani ya kale wilaya hiyo.
Akizungumza na Wananchi mara baada ya kumalizika kwa Matembezi hayo Mwenyekiti huyo Amewataka wananchi Wa kusini Pemba Kuendelea kufanya mazoezi ili kuimarisha afya zao na kuepukana na Maradhi mbali mbali.
"Tunafahamu kuwa Mazoezi yanaimarisha Afya yanatukinga na Maradhi, Yasioambukiza kama vile Pressure ambayo ni sindikizo la Damu , Kisukari, Uzitowa Kupindukia, Magonjwa ya Moyo haya yote tukiwa na tabia ya kufanya mazoezi tutaondokana nayo na kuepuka kuenda hospitali mara kwa mara na kuisaidia kupunguza mzigo kwa Serikali yetu wa kuagiza dawa za magonjwa haya yasioambukiza " Alisema .
Amesema Taasisi hiyo imeweka Mpango huo maalum wa kuhamisha umuhimu wa kufanya Mazoezi kwa Wazanzibari wote ili kuenda sambamba na Kasi ya Maendeleo iliyopo ambayo inahitaji Wananchi wenye Afya Imara.
"Kwa Kasi ya 5G iliyopo inayoletwa na Rais wetu Dk Hussein Mwinyi ni lazima inahitaji Afya imara ya wananchi wake na ndio sababu ambayo Taasisi ya Zanzibar Maisha Bora Faundation ikaweka kipaumbele muhimu suala hili la Kufanya mazoezi kwa Wananchi".
Aidha Maryam amesema licha ya kuimarisha Afya pia Ufanyaji wa mazoezi Unasaidia kukuza Umoja na amani na kuimarisha zaidi Mshikamano uliopo.
"Michezo inatuletea amani na furaha kama ambavyo tunajiona hapa leo kupitia mazoezi haya ya pamoja Tumefurahi tumekusanyika tumejuana watu kutoka meneo na itikafi mbali mbali kwa pamoja mumeitikia kwa hamasa jambo hili kwa pamoja Nasema Ahsanteni na nikiri muitikio huu nimefurahi hivyo tuzidishe umoja na mshikamano huu ili kuzidisha Amani iliyopo".
Akizungumzia kuhusu Taasisi hiyo ya Zanzibar Maisha Bora Faundation iliyoanzishwa mwaka 20121 na kuanza Rasmi kazi zake Mwaka 2022 Mama Mwinyi Amesema kuwa lengo la kuanzishwa kwa Taasisi hiyo imeundwa maalum kwa lengola kuisaida Serikali Kuleta Maendeleo kwa Wananchi Wake.
"Lengo la kuanzisha taasisi ni kuunga mkono Serikali hususan ni kwa akina Mama, Vijana na watoto ambapo Zanzibar Maishabora Faundation inasaidia zaidi katika maeneo manne Ambayo ni uwezeshaji kwa Akina mama wakulima wa Mwani, Masuala ya Afya ya Mama na Mtoto, Ushajihishaji wa Uchanjaji chanjo ya Uviko 19 katika maeneo ambayo yako nyuma Vile vile kutoa Elimu Afya ya Uzazi na Hedhi salama kwa Vijana Sambamba na kupinga ukatili na Udhalilishaji wa akina mama na Watoto.
Awali Akizungumza Mku wa Mkoa wa Kusini Pemba Mattar Zahor Massoud Amemshukuru Mwenyekiti huyo kwa Kutimiza Ahadi yake ya kuungana pamoja na wananchi wa Mkoa wa kusini Pemba katika Matemebezi hayo ya kuhamasisha Suala hilo la kuimarisha Afya .
" Tunakushukuru Mwenyekiti Ambae pia ni Mke wa Rais wa Zanzibar kwa kutimiza Adhma hii ya kujumuika na Wananchi Wa Kusini Pemba , tunakuombea heri katika Kumsidia Rais kutimiza majukumu yake ya Kuleta Maendeleo kwa Taifa tunakuomba uendelee na moyo huo wa kumsaidia Kuleta Maendeleo Kwa Wananchi".
Awali akitoa Salamu za wizara ya Habari, Vijana Utamaduni na Michezo kwa Niaba ya Waziri wa wizara hiyo Tabia Maulid Mwita, Kamishna Idara ya Michezo Pemba Ameir Muhamed Makame Amesema kuwa wizara itaendelea kushirikiana na Taasisi hiyo katika kuona Suala la kuhamaisha michezo linakiwa Endelevu Kwa Wananchi wa Zanzibar pamoja na kuongeza hamasa juu ya Suala hilo .
Pamoja na Mambo Mengine Mwenyekiti huyo Pia Amekabidhi Taulo za Kike 200 kwa Wanafunzi wa Skuli ya Skuli ya Sekondari Dk Philip Mpango na Skuli ya Msingi Uzalendo ikiwa lengo ni kuimarisha Afya ya Uzazi kwa Watoto wakike.
Matembezi hayo ambayo yalianza mapema katika Eneo la kiwanda cha Makonyo Wawi na Kumalizia katika Viwanja vya Gombani ya kale yamewashirikisha wananchi, viongozi wa Serikali za Wilaya zote Mbili Chake Chake na Mkoani, Viongozi wa vyama vya siasa Taasisi mbali mbali pamoja na Vikundi vya Mazoezi vilivyomo katika Mkoa huo.
Comments
Post a Comment