AKINA MAMA WINGWI MTEMANI WAOMBA MSAADA WAKUTULIWA NA NDOO KICHWANI
- Get link
- X
- Other Apps
Na Amina Ahmed Moh’d Pemba.( minnah1202@gmail. com)
BAADHI ya akina mama Katika kijiji cha jambo nia kilichopo Shehia ya Wingwi Mtemani Wilaya ya Micheweni Mkoa wa Kaskazini wanalazimika kuchota Maji kwajili ya Matumizi huku wengine wakiwa katika Hali ya Ujauzito ni kutokana na kukosa huduma ya Maji ya Bomba ndani ya kijiji chao.
Wakizungumza baadhi ya kina mama hao mara baada ya kuonekana na kamera hizi wakiwa katika kisima cha ndoo Akina Mama hao Wamesema kuwa hulazimika kufanya hivyo ili kujipatia Maji kwajili ya kuendesha shughuli za majumbani ambazo kwa Asilimia kubwa zinahitaji maji ili kukamilika kwake.
Wamesema kukosa huduma hiyo kwa mufa mrefu kijijini kwao ndiko kunakosababisha kutumia visima hivyo kuchota maji na kuhatarisha hali za Afya zao ikiwemo kupata maradhi ya kichwa.
Akina mama hao wameiomba serikali pamoja na viongozi wao wa jimbo kuwasaidia kulipatia ufumbuzi suala hilo ili waweze kuondokana na usumbufu huo wa kubeba ndoo kichwani na kuepukana na kutumia maji ambayo uhakika na usalama wake wa kiafya sio wa uhakika.
"Maji ya Mfereji Sijui ata Muda gani sijayaona apa jambo nia, tunachota haya tupikie, vichwa vinatuuma lakini hatuna lakufanya Maji ni lazima majumbani yaweko" Alisema Mkunga Khamis Said mkaazi wa Jambo Nia.
" Kama iwezekano wa kuletewa maji ya mfereji upo bhasi tusaidiwe ndoo kichwani mudawote ni Tatizo si dogo na ivo visima vyenyewe wasi wasi mtupu Watoto tunaogopa ata kuwatuma". Aliendelea Mkunga.
Maji ya mfereji kwetu siku ya kutoka itakuwa Tunu kama Lulu Mana hayapo siku nyingi wenzetu maeneo mengine mifereji saa zote maji tele Na Sisi tunaiomba Serikali isitisahau tunaoteseka ni sisi akina Mama, Baba ata hawana muda uo" Biamu Khamis Said Alisema.
Akizungumzia suala hili sheha wa shehia ya Wingwi Mtemani Muhammed Ali Hamad amekiri kuwepo kwa tatizo hilo katika badhi ya meneo ndani ya shehia yake ikiwemo kijiji cha Jambo nia ambapo amesema uongozi wa shehia umechukua jitihada mbali mbali ikiwemo kulipfikisha suala hili katika uongozi wa wilaya.
"Ni kweli tatizo la maji ya mfereji katika baadhi ya vijiji ndani ya Shehia yangu lipo na uongozi wa Shehia tumeshalifikisha suala hili kwa wahusika ambao ni zawa pamoja na Uongozi wa Wilaya.
" Taarifa za kukosekana kwa huduma ya maji safi na salama Baadhi ya vijiji ndani ya shehia ya Wingwi mtemani tmeshalipeleka kwa uongozi wa wilaya kupatiwa ufumbuzi zaidi".
Hata hivyo Harakati za kumtafuta Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji pemba juu ya suala hili zinaendelea .
Mwisho
- Get link
- X
- Other Apps
Comments
Post a Comment