WANANCHI PEMBA WAIOMBA SERIKALI KUWASAIDIA HOSPITALI YA WAGONJWA WA AKILI PAMOJA NA MADAKATARI MAALUM
AMINA AHMED MOH’D - PEMBA , ( 0719859184.).
WANANCHI Shehia ya Wingwi Mtemani Wilaya ya Micheweni Mkoa Wa kaskazini Pemba wameiomba Serikali na wadau kuwasaidia kulipatia ufumbuzi suala la kujengewa Hospitali maalum kwajili ya wagonjwa wa Akili ili kuwaepushia kuzurura na Kuzagaa mitaani sambamba na kuwawekea Madakatari Maalumu ambao Watakuwa na Utaratibu wa kuwatembelea na kuwapatia Huduma za matibabu Wagonjwa hao Wanapokuwa Majumbani.
Wametoa Ombi hilo leo Walipokuwa wakizungumza na kutoa maoni yao juu ya habari hizi kuhusu haki ya kulindwa dhidi ya Udhalilishaji wa Kijinsia kwa Watu wenye Ulemavu wa Akili katika Maeneo mbali mbali kisiwani Pemba.
Wamesema Licha ya Kuwepo kwa Idadi kubwa ya Watu wenye Ulemavu wa Akili wanaozurura na kuzagaa katika Maeneo mbali mbali kisiwani Pemba Lakini bado kumekuwa na Changamoto ya Kukosekana na Hospitali hiyo pamoja kutokuwepo kwa Madakatari wanaotembelea Majumbani kuwapatia huduma za Matibabu jambo ambalo linapelekea kuhatarisha Usalama wao, sambamba na Kukosa Haki zao mbali mbali ikiwemo Afya Bora .
"Wagonjwa Wa Akili wapo kwa idadi Kubwa kisiwani Pemba, Hata Umtafute Daktari Umwambie mimi nina mgonjwa siwezi kumfikisha Hospitali njoo mara moja Unisaidie Humpati, Labda Unaweza ukampata ukimlipia Gari au nauli ndio akufate, Mimi ninae mgonjwa ndani mwangu mtu mzima Hajajapo Daktari kuja kumuona na Kila siku naenda Pale Hospitali kununua Dawa lakini hata ile hamu ya kutaka kujua tu anaendeleaje hawaulizi Tunaomba wadau zaidi Wizara ya Afya Itusaidie hili " Alisema Shoka Hamad Abeid Mkaazi wa Wingwi.
"Kutokana na kukosa Uelewa Tunalazimika kuwaacha tu wazurure Mimi mwanangu ni mgonjwa wa Akili ana miaka 10 nilimuandikisha Lakini alikuwa umo Darasani hakai mara anaingia madarasa mengine Hatulii niliamua nimkatishe, anazurura tunaomba wadau na wa watu wenye ulemavu, Haki za Binaadamu na wadau wa kupambana na Udhalilishaji, pamoja na Serikali, watusaidie Kupata uelewa Huenda tunawakosesha haki zao kutokana na kushindwa kujua vipi tunawasaidia kisheria kuzipata izo haki hizo " Alisema Mkongwe Khamis Said Mama Mweye mtoto ambae anaulemavu wa Akili Wingwi Jambo Nia.
Aidha Wananchi wameziomba jumuia na Mshirika ya kusaidia Upatikanaji wa haki kwa Watu wenye ulemavu Kuzidisha ukaribu wao kwa jamii ili kupata urahisi wa kufikisha changamoto zinazowakabili watu wenye Ulemavu wa Akili na nyengine mbali mbali zinazowakabili zinazohitaji msaada wa kisheria
Wakizungumza Juu ya Suala hilo Mwenyekiti wa Jumuia ya watu wenye Ulemavu Pemba Halfan Amour Muhammed Pamoja Siti Habib Muhammed Kutoka Shirika La Msaada wa Kisheria Zanzibar ofisi ya Pemba Wamesema Wataendelea kusimamia , kushawishi, pamoja na kutetea Upatikanaji wa Haki za Msingi kwa Watu wenye Ulemavu wa Akili kwa Wadau wa Maendeleo pamoja na Serikali.
Watu wenye ulemavu wa akili wamekuwa wakizurura huku wengine wakiitwa majina mabaya wengine wakifanyiwa vitendo viovu lakini Haki juu yao haipatikani, kutokana na kukosa Watetezi Jumuia ya Watu wenye ulemavu wa Akili tutaendelea kuwa bega kwa bega kuona haki wanapata haki sawa kama walivyo watu wengine" Alisema Mwenyekiti huyo.
" Watu wenye Ulemavu wa Akili wanastahiki kua na haki sawa kama Walivyo binaadamu wengine, Haki ya Kuishi, kulindwa dhidi ya majanga ikiwemo udhalilishaji, Haki ya matibabu kushirikishwa Haki ya Kusoma na nyengine nyingi Zote hizi haziwezi kupatikana iwapo wazazi na walezi hatutokuwa tayari kuwasaidia".
"Tunatakiwa tuzidishe Mara mbili Usimamizi wa Kuzitafuta haki za Watoto wenye ulemavu wa akili Shirika la Msaada wa kisheria tutaendelea kutoa mashirikiano Muda na wakati wowote hivyo wananchi muitumie fursa hii katika kuona watu wenye ulemavu wa akili na wao hawaachwi nyuma katika kupata haki na Maendeleo .
Harakati za Kumtafuta Afisa Mdhamini wizara ya Afya Pemba juu ya Maoni hayo yaliotolewa na wananchi yanaendelea.
Mwisho
Comments
Post a Comment