HABARI ZINAZOHUSU AFYA YA UZAZI KWA WANAWAKE NA WASICHANA YAJA NA SURA MPYA PEMBA NI BAADA TAMWA-ZNZ KUTAFUTA 40 JUU YA UTOLEWAJI MDOGO WA TAARIFA HIZI.
Na - AMINA AHMED MOH’D , PEMBA.
ZAIDI ya Waandishi wa Habari 15 Kutoka vyombo mbali mbali Kisiwani Pemba wamepatiwa Mafunzo ya siku tatu juu ya Afya ya Uzazi ambayo yamelenga kuongeza uelewa juu ya kuandika kwa Ubora na kuelimisha kupitia kalamu zao na kuondosha Changamoto zinazoendelea kujitokeza kutokana na kukosekana kwa Afya na Uzazi kwa Makundi mbali mbali ya wanawake katika Jamii.
Akifunga Mafunzo kwa Waandishi hao Afisa Mdhamini Wizara ya Afya Pemba Khamis Bilali Ali amewataka Waandishi hao kuitumia Elimu hiyo iliyotolewa kwa kuandika Habari zitakazoisaidia Kupunguza Vifo vya kina Mama na watoto .
Amesema Miongoni mwa vipengele Muhimu ambavyo vinahitaji kufanyiwa kazi na Waandishi wa Habari kufikisha Elimu na Kusaidia Serikali ni Afya ya Uzazi ambayo Wanawake na Wasichana waliowengi wanaikosa Elimu hiyo hiyo na kupelekea Kupata Changamoto mbali mbali za Kiafya.
"Afya ya Uzazi kwa ni Taaluma ambayo ni pana sana, hili ni Jambo Zuri lililofanywa na Ndugu Zetu wa Tamwa kwa sababu kupitia Elimu hii Mliopatiwa Mtaweza kuandika Habari mbali mbali zinazohusu Afya ya uzazi, kuna Mimba za Umri Mdogo, Uzazi wa Mpango, kwaio taaluma hii itakuwa ni msaada wa kuondoa zile changamoto zilizopo katika jamii zikiwemo Ndoa za Mapema na Watu kupata Uelewa wa Kutosha na kujua Masuala Mazima ya Uzazi Salama" Alisema Khamis Bilali Afisa Mdhamini wizara ya Afya Pemba.
Aidha Mdhamini Huyo Alisema kuwa Moja kati ya Vipaumbele vya Wizara ya Afya Zanzibar ni kupunguza Vifo vya Mama na watoto hivyo kupitia Elimu hiyo iliyotolea kwa Waandishi Jamii itaweza kujikinga na Kuzuia Upatikanaji wa mimba za Mapema kwa Wanawake pamoja na kuondosha Mimba za umri Mdogo kwa Wasichana pamoja na kuongeza uelewa kwa Wananchi juu ya Kutumia Uzazi salama pamoja na utumiaji wa Uzazi wa Mpango.
Awali Akizungumza kwa Niaba ya Mkurugenzi wa Chama Cha Waandishi wa Habari Wanawake TAMWA Zanzibar Muhammed Khatib Muhammed ambae ni Afisa Ufuatiliaji na Tathmini kutoka Chama hicho amesema Mafunzo hayo yalilenga zaidi kuongeza uelewa wa Kuripoti Habari zinazohusu Afya ya Uzazi kwa waandishi wa Habari ikiwa ni Pamoja na kuzungumzia Elimu na Upatikanaji wa Huduma Mbali mbali katika Vituo vya Afya.
"Tumeona kuna changamoto kubwa kwa Waandishi wa Habari ni Kushindwa kuandika Habari zinazohusu Afya ya Uzazi na kabla ya haya Mafunzo Tulifanya utafiti tukagundua kama tatizo kubwa ni Waandishi waliopo katika vyombo Vya Habari vingi Elimu juu ya Afya ya Uzazi ni Ndogo ndio mana tukaamua kutoa Elimu hii ili kuona wanatekeleza majukumu yao kwa Uweledi katika Kutetea Haki za wanawake katika Masuala hayo ya Afya ya Uzazi" Alisema.
Rahila Salim Omar Dakatari wa Magonjwa ya Uzazi Pemba Amesema Jamii inaweza kujiepusha na Magonjwa ya Kujamiana, na kuweza kujifungua Salama, kujilinda pamoja na kujikinga na Magonjwa Saratani kwa Kufanya uchunguzi wa kitaalamu juu ya Afya Ya Uzazi kwa kupima Magonjwa mbali mbali ambayo hupelekea kuathiri Viungo na Afya ya Uzazi na Kusababisha Vifo.
Akitoa Elimu juu ya Afya ya Uzazi Ali Mbarouk Omar Mratibu wa Tume ya Ukimwi Pemba ambae pia ni Mwandishi wa Habari Mwandamizi, alisema kuwa Miongoni mwa njia Bora za kulinda Afya Kwa Wanawake na Wasichana ni vyema wazazi kujiwekea Utamaduni wa kuchunguza Watoto Afya za watoto wakike katika Sehemu za Viungo vya Uzazi ili kuweza kubaini endapo kutakuwa Mabadiliko katika viungo vya uzazi kwa Watoto wao na kuweza kupatiwa Matibabu Katika hatua Za Awali wanapobainika kuwa na Magonjwa ya Afya ya Uzazi.
Nae Sheik Abdalla Nassor Abdalla (Almaul) kutoka Jumuia ya Maimamu Zanzibar (JUMAZA ) Amesema Afya ya Uzazi iliyo Salama kwa Wanawake inahitaji Maandalizi ya Mapema katika Dini Utamaduni na Mazingira ikiwemo Chakula Malazi Malezi na Makuzi kwa watoto, Wanawake na wanaume.
Sheikh Abdalla Nassor Abdalla Maul - JUMAZA
Mafunzo hayo ya siku 3 yaliondaliwa na Tamwa Zanzibar kwa Kushirikiana na TAMWA Tanzania kwa Ufadhili wa Shirika la Well Spring juu ya Haki ya Afya ya Uzazi kwa Wanawake na Wasichana Mjini na Vijijini yamefanyika katika Ukumbi wa Ofisi za Chama hicho Mkanjuni Chake Chake Ambapo Waandishi hao walijengewa Uelewa juu ya Elimu ya Afya ya Uzazi, Hedhi salama, Saratani ya Matiti, Saratani ya Shingo ya Mlango wa Kizazi, Uzazi Wa Mpango, Mazingira ya Kidini kiutamaduni juu ya Afya ya Uzazi, Maradhi ya kujamiiana, Mimba za Umri Mdogo, Ndoa za Mapema Pamoja na Lishe bora kwa mama wajawazito na watoto.
Mwisho.
.
Comments
Post a Comment