MKURUGENZI BARAZA LA MJI WETE "NITASIMIA UJENZI SOKO MZAMBARAUNI KUSOGEZA KARIBU HUDUMA KWA WANANCHI
Na AMINA AHMED MOH’D, PEMBA.
KUFUATIA Maombi na kilio cha Muda Mrefu kwa Wakaazi Mzambarauni takao Wilaya ya Wete Mkoa wa Kaskazini Pemba juu ya kujengewa Soko katika Kijiji chao Hatimae Uongozi wa Baraza la Mji wete Umepitisha Azimio la kujengwa soko kijijini Hapo. SALMA ABUU HAMAD MKURUGENZI BARAZA LA MJI WETE
Adhimio hilo limepitishwa na Mkurugenzi wa Baraza la Mji Wilaya ya Wete Salma Abuu Hamad kwa kushirikiana na Madiwani wa wilaya ya Wete Ambapo amesema adhimio hilo limelenga kuwaondoshea Usumbufu Wananchi.
Aidha Mkurugenzi huyo alisema kuwa Kupitishwa kwa Adhimio hilo kumetokana na Maombi ya Muda Mrefu kutoka kwa wananchi wa Mzambaruni Kuhitaji soko karibu na Maeneo yao ambalo litawasaidia kurahisisha upatikanaji wa bidha na kuwaondoshea usumbufu wa kufata bidhaa maeneo ya mbali.
"Mlikuwa mnaleta sana Barua nyengine kabla hata mimi sijawa mkurigenzi, Ombi na kilio chenu mnahitaji Mjengewe soko, Hapa Mzambarauni, lakini leo sisi kama uongozi tumeamua kupitisha azimio la kujengwa meadi hapa mzambaraunitakao na tumepitisha uamuzi huo baada ya kuona katika kijiji hichi na vijij jirani hakuna soko la karibu na lililopo halikidhi haja. " Alisema
Katika hatua nyengine Mkurugenzi huyo M alieleza kuwa Kwa Baraza la Mji Wete linaendelea na shughuli mbali mbali za kuimarisha huduma za wananchi ikiwa ni pamoja na ujenzi wa sehemu za kukaa Abiria katika maeneo mbali mbali ya Wilaya ya hiyo ili Kuondosha usumbufu wanaoupata Abiria.
" Kwa Sasa baraza la Mji Wete limeweza Kujenga vibanda Kwa ajili ya kupumzikia abiria katika maeneo mbali mbali ya Wilaya ya Wete na hii imeweza kuleta faraja Kwa wananchi wetu kwani walikuwa wanahangaika sana wakati wakisubiri Usafi katika vituo vya gari na Tunazidi kuimarisha na kuongeza vituo hivyo maeneo mbali mbali ," alisema Mkurugenzi.
Mwenyekiti wa Baraza la Mji Wete Zulfa Abdalla Said alieleza kuwa endapo soko Hilo litajengwa na kukamilika litasaidia kutoa fursa za Ajira kwa vijana walio wengi na kuwasaidia kujikimu kimaisha.
Ni kweli Uongozi wa Baraza umedhamiria na umeshapitisha Adhimio hilo na Tunatarajia kujenga soko la kisasa ambalo litakidhi mahitaji ya watu wote na pia kuzalisha fursa za vijana kujiajiri na kujipatia kipato chao.
Akizungumzia juu ya Suala hilo Diwani wa wadi ya Pandani Khalid Hamad Ali alieleza kuwa mipango ya ujenzi wa soko Hilo umekamilika na hivyo uongozi hautorudi nyuma katika kutekeleza suala hilo ambapo amewataka wanachi kuwa tayari kutoa mashirikiano katika kulifanikisha suala hilo.
Wakizungumza baadhi ya wananchi wa Shehia ya Mzambarauni wameuomba uongozi huo wa baraza la mji Wete kutosikiliza kauli za baadhi ya wananchi wanaotufisha nyuma maenedeleo katika Wilaya hiyo.
"Ni faraja kwametu kuona Baraza la Mji Wete limedhamiria Kujenga soko la kisasa katika eneo la mzambarauni takao jambo hili litaweza kuinua Hali ya Uchumi katika eneo letu kuna fursa zitapatikana , Alisema Said Mbarouk Ali mkaazi wa Mzambarauni.
Ali Abdalla Chande Alisema kuwa Wananchi wa kijiji hicho wanahitaji zaidi maendeleo ambayo yatawasaidia kuwapa fursa mbali mbali za kujiendeleza kimaisha.
"Hamu kubwa kijijini kwetu ni Maendeleo endelevu ambayo yatatusaidia kutukomboa lakini kuacha Alama kwa vizazi katika Kujiendeleza kiuchumi Soko ni jambo moja wapo la Maendeleo tunakupongeza Mkurugenzi kwa uamuzi huo wenye maslahi kwetu tunaahidi kukuunga mkono kwa nguvu zetu zote.
"Niupongeze uongozi wa Baraza la Mji Wete Kwa kufikiria Kujenga soko katika Kijiji chetu, hii inaonesha dhahiri kuwa uongozi uliopo unajali wananchi wake kwani jambo hili ni njia moja wapo ya kupata maendeleo, hivyo Kwa Umoja wetu Wana Mzambarauni tunasema kuwa tuko tayari kujengewa soko na hili halina mjadala wowote. Alisema Salama Saidi Khamis .
Azimio hilo la kujengwa soko la kisasa kijijini humo kwajili ya kurahisha upatikanaji wa huduma na uuzaji wa bidhaa kwa wananchi wa Mzambarauni sambamba na maeneo jirani unatarajiwa Kutekelezwa muda wowote ndani ya kipindi hiki cha 2023/2024.
Mwisho.
Comments
Post a Comment