Posts

TAMWA YAKUTANA NA WADAU ZANZ ADAPT PEMBA.

Image
Time khamis Mwinyi Redio Micheweni ‎ ‎Chama  cha wandishi Wahabari wanawake Tamwa kisiwani Pemba wamezitaka asasi za kiraiya na tasisi za Serekali kutowa ushirikiano katika kutekeleza mradi wa Mabadiliko ya Tabia nchi. ‎ ‎kauli hio imetolewa na Meneja wa Mradi wa ZANZADPT  Zoni ya Pemba  Ali Hamad wakati alipokuwa akitowa utambulisho wa mradi kwa asasi za kiraiya na tasisi za Serekali katika ofis za SHIJUWAZA  Chake Chake Pemba. ‎  ‎Amesema katika mradi huo wa ‎kukabiliana na mabadiliko ya Tabiya  nchi yamekuja kuwakomboa wanawake Katika nyanja mbali ikiweo kiuchumi na kuweza kupaza sauti katika kutetea haki zao. ‎ ‎Wakati huo huo Nairat Abdullah Ali Afisa Program kutoka  ‎TAMWA_Zanzibar amesema Kila mmoja anajukumu la kuchukuwa hatua ya kukabiliana na mabadiliko ya Tabiayanchi hasa Kwa kutumza mazingira kwakupanda Miti Ili kukabiliana na mabadiliko hayo ambayo yamekuwepo Kwa kiasi kikubwa. ‎ ‎Nae Juma Bakari Alawi mratibu AZASPO Pemba amei...

WAANDISHI TUMIENI KALAMU ZENU TUPATE SHERIA MPYA HABARI

Image
NA MARYAM SALUM AFISA Programu na mchechemuzi wa mapitio ya sheria za habari Zanzibar, Zaina Abdulla Mzee amewataka waandishi wa habari Kisiwani Pemba kutumia kalamu zao vizuri kuendelea kutilia mkazo upatikanaji wa sheria mpya ya habari  itakayosaidia tasnia ya habari Zanzibar.  Ameyasema hayo wakati akifungua mafunzo ya ukumbusho wa hizo, kwa waandishi wa vyombo mbali mbali Kisiwani humo, ambayo yalifanyika katika Ofisi ndogo ya TAMWA iliyopo Mkanjuni Chake Chake. Afisa huyo alisema kuwa waandishi wa habari ndio wahusika wakubwa wa sheria hiyo mpya, hivyo wanaowajibu mkubwa kwao kutoa sauti zao sambamba na kuandika yale ,adhara mbali mbali ambayo yapo kwenye sheria zilizopo kwa sasa. Ameeleza kuwa mchakato mzima wa upatikanaji wa sheria hiyuo mpya, umekuwa ukionekana ni wakusuasua, hivyo kama waandishi wenye kiu ya sheria ambayo itakuwa rafiki kwao ni vyema kiutumia kalamu zao, kupiga debe mchakato huo ili iweze kupatikana. Alifahamisha kuwa wanahabari wanao uwez...

MAGUMU YA WAGOMBEA WANAWAKE WAKATI WA UCHAGUZI

Image
I  NA, AMINA AHMED MOH’D  PEMBA.   IKIWA imebaki miezi michache  Tanzania  yenye idadi ya watu  61,741,120 wanawake 31,687,990  na wanaume 30,053130 kuufikia uchaguzi mkuu wa nchi mwaka 2025 ,tusiyasahau magumu waliyopitia wagombea wanawake wakati wa uchaguzi.  Uchaguzi  ambao kikawaida hufanyika kila baada ya miaka 5 na kutoa fursa kwa  watu wote waliotimiza sifa na mashrti yaliyowekwa kwa mujibu wa sheria kuwania nafasi za kuwakilisha wananchi katika vyombo vya maamuzi ikiwemo bunge baraza la wawakilishi pamoja Na baraza la Madiwani .  Changamoto hizo zilizojitokeza  2020 kwa baadhi ya  wagombea wanawake ambazo huenda zisiposemewa bhasi  ushiriki wa wao   katika mchakato wa uchaguzi unaweza ukaendelea kubaki  nyuma bila kufikia malengo ya usawa wa kijinsia asilimia 50 kwa 50 katika vyombo  vya kutolea maamuzi  .  Chanagamoto hizo ambazo ni kutokuwepo kwa maafisa wasiyokuwa w...

TAMWA YAWAASA WANAHARAKATI

NA ASIA MWALIM  MJUMBE Wa Bodi kutoka Chama Cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA-ZNZ) Mwatima Issa Rashid, amewataka wanaharakati kuzitumia siku 16 za kupinga udhalilishaji kuleta mabadiliko ya muda mrefu katika kujenga jamii yenye utu, heshima amani na utulivu nchini. Alitoa wito huo katika maadhimisho ya kupinga siku 16 za udhalilishaji yalioandaliwa na TAMWA Zanzibar, kwa kushirikiana na Shirika la Maendeleo la Ujerumani (GIZ) hafla iliyofanyika ukumbi wa Bima, Mperani Mjini Unguja. Alisema michango ya wanaharakati ina nafasi kubwa na inathaminika kusaidia mapambano ya vitendo vya udhalilishaji na unyanyasaji wa kijinsia nchini. Aidha aliwataka wanaharakati kuitumia siku hiyo kupokea na kujadiliana mchango mbali mbali itakayowasilishwa ili kuwa chanzo cha kujenga ari mpya kuwavutia wengine kuungana nao kupinga vitendo hivyo. Alisema kwa sasa TAMWA ina nafasi kubwa ya kupaisha sauti za wanawake na makundi mengine kwa kua mstari wa mbele kushajihisha na kutoa taaluma k...

WANAHARAKATI WAASWA NA TAMWA

NA ASIA MWALIM  MJUMBE Wa Bodi kutoka Chama Cha Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA) Mwatima Issa Kassim, amewataka wanaharakati kuzitumia siku 16 za kupinga udhalilishaji kuleta mabadiliko ya muda mrefu katika kujenga jamii yenye utu, heshima amani na utulivu nchini. Alitoa wito huo katika maadhimisho ya kupinga siku 16 za udhalilishaji yalioandaliwa na TAMWA Zanzibar, hafla iliyofanyika ukumbi wa Bima, Mperani Mjini Unguja. Alisema michango ya wanaharakati ina nafasi kubwa na inathaminika kusaidia mapambano ya vitendo vya udhalilishaji na unyanyasaji wa kijinsia nchini. Aidha aliwataka wanaharakati kuitumia siku hiyo kupokea na kujadiliana mchango mbali mbali itakayowasilishwa ili kuwa chanzo cha kujenga ari mpya kuwavutia wengine kuungana nao kupinga vita hivyo. Alisema kwa sasa TAMWA ina nafasi kubwa ya kupaisha sauti za wanawake na makundi mengine kwa kua mstari wa mbele kushajihisha na kutoa taaluma kupitia vyombo vya habari ili kufikia jamii kubwa na kwa wakati. Ali...

MTU MMOJA MIKONONI MWA POLISI AKITUHUMIWA KUBAKA NA KUSABABISHA KIFO CHA MTOTO WA MIAKA SITA

Jeshi la Polisi Mkoa wa Kusini Unguja linamshikilia mtu mmoja aitwae Maulid Hassan Maulid  (18) mkaazi wa Mwera Pongwe katika Wilaya ya Kati,  Mkoa wa Kusini Unguja kwa tuhuma za mauaji ya mtoto mdogo Khadija Dadi Mhoda (06) mwanafunzi wa chekechea mkaazi wa Mwera Vichaka mabundi, shehia ya ubago. Akizungumza na waandishi wa habari huko Tunguu , Makao Makuu ya Polisi Mkoa wa Kusini unguja, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi Daniel Shillah amesema tukio hilo la Mauaji lilitokea Novemba 14, 2024 huko Mwera Vichaka Mabundi ambapo Mtuhumiwa huyo alimwingilia kimwili na kumsababishia kifo chake. Kamanda SHILLAH amesema Jeshi la Polisi Katika Mkoa huo linaendelea kufanya upelelezi ili mtuhumiwa huyo afikishwe Mahakamani.

CHADEMA ZANZIBAR YATUMA NENO KWA VIONGOZI

Na,Amina Ahmed Moh'd Pemba. MAKAMU  Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Said Issa Moh`d amelitaka Bazara la viongozi wa chama hicho kanda ya Pemba kufanya kazi kubwa wa kukipambania chama hicho ili kiweze kushinda katika nafasi mbali mbali za uongozi kisiwani humo katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2025. Amesema chama hicho kwa sasa kimekuwa kikiendelea kuimarika kila kukicha na kupata uungwaji mkono kutoka kwa wananchi hasa vijana, hivyo viongozi hao wakiendelea kufanya kazi nzuri nafasi ya kushinda katika uchaguzi mkuu wa mwakani ipo wazi. Issa ameyasema hayo leo alipokuwa akizungumza na viongozi wa Bazara hilo kanda ya Pemba katika mkutano mkuu wa kanda ulioambana na uchaguzi wa kuwachagua viongozi wa kanda hiyo uliofanyika huko  Hifadhi Hotel Tibirinzi Chake Chake. Amesema baada ya muda mrefu wa kupambana na kukijenga chama hicho hapa visiwani Zanzibar sasa kina fursa ya kusimamia wagombea katika nafasi mbali mbali na kushindwa kwani tayari kimekubalika k...