MAGUMU YA WAGOMBEA WANAWAKE WAKATI WA UCHAGUZI

NA, AMINA AHMED MOH’D  PEMBA.
  IKIWA imebaki miezi michache  Tanzania  yenye idadi ya watu  61,741,120 wanawake 31,687,990  na wanaume 30,053130 kuufikia uchaguzi mkuu wa nchi mwaka 2025 ,tusiyasahau magumu waliyopitia wagombea wanawake wakati wa uchaguzi. 

Uchaguzi  ambao kikawaida hufanyika kila baada ya miaka 5 na kutoa fursa kwa  watu wote waliotimiza sifa na mashrti yaliyowekwa kwa mujibu wa sheria kuwania nafasi za kuwakilisha wananchi katika vyombo vya maamuzi ikiwemo bunge baraza la wawakilishi pamoja Na baraza la Madiwani . 
Changamoto hizo zilizojitokeza  2020 kwa baadhi ya  wagombea wanawake ambazo huenda zisiposemewa bhasi  ushiriki wa wao   katika mchakato wa uchaguzi unaweza ukaendelea kubaki  nyuma bila kufikia malengo ya usawa wa kijinsia asilimia 50 kwa 50 katika vyombo  vya kutolea maamuzi  .
 Chanagamoto hizo ambazo ni kutokuwepo kwa maafisa wasiyokuwa waaminifu  kutoka Tume ya uchaguzi , Vikwazo,Vitisho,Dharau,Kukosa Fedha za kuendeshea Kampeni, Kukosa na kuondolewa Mawakala kutokuwepo kwa Tume huru kukosa ulinzi  pamoja na udanganyifu. 

Wanawake wengi ambao baada ya kupata ridhaa ya chama chochote kati ya vyama  19 vya siasa vinavyotambuliwa na msajili wa vyama vya siasa  nchini Tanzania na kupata ,fursa ya  kuingia katika mchakato wa  kuwakilisha  moja  kati ya  majimbo 264 ya uchaguzi yaliopo Tanzania ambayo   214  yapo na mengine 50  yapo Zanzibar  .
Makala hii maalum imezungumza na baadhi ya wanawake waliowahi kugombea nafasi ya ubunge   katika uchaguzi mkuu uliopita wa mwaka 2020  na kukumbana na kadhia hizo  ambapo wanaamini iwapo zitadhibitiwa  ushiriki wao utaweza kuongezeka kuelekea 2025 na kufikia usawa wa kijinsia katika vyombo vya maamuzi.
Rukia Abuu bakar Muhammed  mwenye umri wa Miaka  34 Mzaliwa wa Chake Chake  ambayo ina jumla ya  wakaazi  136,298  Wanawake 70,912 na  wanaume 65,386  Aliyepata  taaluma yake ya ualimu katika chuo  kukuu cha Taifa Zanzibar  SUZA ,   Mama wa watoto wa 5 mkaazi wa mtaa wa  Chachani   wenye  idadai ya wakazi 990  wanaume 509 na wanawake 481  wadi ya Tibirinzi  yenye idadi ya wakazi 11,089 wanaume 5304  na wanawake 5785  Mkoa wa kusini pemba ambao una jumla ya wakazi  271,350 wanaume 131,373 na wanawake 139,977.
Rukia  Abuu ni mwanasiasa aliyezianza harakati hizo  mnamo mwaka 2014  ni baada ya kupenda siasa,utayari  na sera za   Chama cha Democrasia na Maendeleo CHADEMA chama ambacho anaendelea kukitumikia hadi sasa  huku akishika nafasi mbali mbali kabla ya kuwania ubunge kwa miongo miwili mfululizo bila mafanikio ambapo nje ya ulingo wa siasa Mwanamke huyo ni mwalimu katika skuli ya Msingi  Michakaeni  .
‘’Niligombea  ubunge  jimbo la Chake Chake  kupitia  Chadema mwaka 2020 lakini niseme tu Uchaguzi  kwa  sisi Wanawake  bado mfumo Dume haujaondoka tunabezwa’’
 Licha ya kuwa bado vijana  utaskia  wengine wanasema aaah !! vijana awa bado hawajui siasa bila kujuwa kuwa siasa haihitaji umri  inahitaji utayari na  uwajibikaji katika kuleta maendeleo’’
‘’ Bado wanaamini  wanaume ambao   age- go  ndio wana maendeleo  , muitikio  unakuwa sio mzuri na tunakosa izo fursa  kwa sababu za hovyo  kama hizo watu hawasikilizi  kile ambacho tunakizungumza wala kukichambua  na hizo ndizo siasa zetu wazanzibari takriban sote.‘’ Alimaliza  Rukia 
Licha ya kutokata tamaa kwa sababu hizo za ubaguzi wa kijinsia na umri  kutoka kwa aliyekuwa mgombea ubunge jimbo la Chake chake kwa tiket ya Chadema  Rukia  anasema kuwa ukosefu wa fedha za kuendeshea kampeni  pia zilikuwa changamoto kubwa .
‘’kwa upande wetu chadema   mwaka 2020 hatukuwa na ruzuku asilimia ndogo tuliyopewa na chama haikukidhi na tulilazmika kufanya kampeni katika mazingira magumu’' . 
Kwa sababu nilikuwa natembea maeneo mbali mbali kwa miguu kuomba ridhaa Wapo vijana waliwahi kuniambia wakati napita kuomba kura tukikupa na sisi utatupa nini mtoto mzuri nia yao sio njema Ilikuwa’’
‘’Naamini ningelikuwa mwanaume wasingeweza kuniambia ivo ,lakini pia ingelikuwa nimeenda kwa usafiri wa heshima pia wangeniheshimu kwaio ni changamoto ambazo tunatamani ziangaliwe kuelekea 2025 zisije kujitokeza  zikarudisha nyuma ‘’
‘’Suala la Tume linahitaji kifua  unakwenda Tume  Chake chake pale maafisa wilaya maafisa wa jimbo  hawakuitikii muitikio ule   ambao wewe unaamini unapaswa kuitikiwa  wanakubeza ‘’
Wanapokuja wagombea wanaume unaona wanaongea lugha moja kwa vile  ni wanaume  wenzao  ndio mana wanawake wengine wanahofia kugombea kwa  kukosa mashirikiano kwa taasisi  inayohitaji itupe mashirikiano’’.

Hali pia haikuwa rafiki kwa  Maryam  Saleh  Juma  mzaliwa na  mkaazi wa Vitongoji Umangani  yenye wakaazi 13,044   wanaume  6,413 na wanawake 66,31 Wilaya ya Chake chake    ambae ni mzoefu wa siasa tangia mwaka 1995 Aliegombea nafasi ya ubunge 2020 katika  jimbo la Ole  wilaya ya Chake chake  kwa tiketi ya Chama cha Ukombozi wa Umma chama ambacho kwa uchaguzi wa mwaka 2020  kiliungwa mkono na wana chama  wa  ACT wazalendo.
  ‘’Saa nane za usiku bado tulikuwa njiani  tunarudi sehemu kituo cha kuhesabiwa kura,huku magari ya doria ya ulinzi na usalama tu ndio yanayozunguruka mitaani atuna hata walinzi sisi wagombea ’’
‘’Hofu zilitutawala hatukuwa na utulivu , Maafisa wa tume  wanaubaguzi,Ubabaifu hakukuwa na  uwazi wala uhuru ,wanawake hatuheshimiki tunapofika kipindi cha Uchaguzi,tunakosa ulinzi tulilala chini ya msheli sheli ‘’
‘’kituo cha kuhesabiwa kura haki haikuwepo , dhulma za wazi wazi nilizishuhudia mimi mwenyewe zikitendeka   nilikuwa na uhakika ndio mshindi   wa kiti cha uchaguzi kwa jimbo la Ole’’
‘’Mawakala wangu walibadilishwa na kuwekwa wengine ,na usiku wakati kura zikaesabiwa Madungu wakati tuliambiwa  Gombani udanganyifu tunatoka gombani kuja Madungu kura zimeshamaliza kuhesabiwa na wakala wangu alikuwa sie tume haikuwa huru hata kidogo’’ Alimaliza Maryam.

‘’Kuna ulazima haswa wa kupatiwa ulinzi kwa viongozi wote wanaogombea nafasi mbali mbali ili kulinda usalama wao dhidi ya hatari zinazoweza kuwakumba  isiwe wanapewa wale wanaogombea nafasi zaa juu tu za urais’’ .

‘’Jitihada zinahitajika kutoka  kwa serikali kuona sasa huu ni wakati wa kuwaunga mkono wanawake  kushika nafasi za uongozi wasiwawezeshe kwa vyama bali wawawezeshe kwa kundi lao la wanawake  tutafanikisha usawa wa kijinsia kuongezeka 2025’’ .

alisema Fat hiya Mussa Said mwanaharakati mwasuala ya wanawake Aliyewezeshwa na TAMWA ZNZ ambao ni miongoni mwa wadau wakubwa wa maswala ya usawa wa kijinsia kwa wanawake .

Rukia anaamini kuwa endapo changamoto hizi zitadhibitiwa kuelekea uchaguzi 2025 hakutokuwa na pingamizi ya wanawake kushindwa kuwa viongozi ndani ya majimbo kwa vile baadhi a vyama vyao vinawaamini katika utendaji.

‘’ Maryam nae akiiomba serikali kutowapa uhuru bila kuisimamia kisheria  maafisa wa Tume kwani ni miongoni mwa wavunjaji wa haki za wanawake hususan ni wakati wa Uchaguzi’’
 
MWISHO.

Comments

Popular posts from this blog

BAJAJI WAMLILIA RAIS DK MWINYI PEMBA ,WAOMBA MSAADA KWAKWE WASEMA WAMECHOSHWA NA HILI KUTOKA MAWASILIANO

Masheha wanawake wa Wilaya ya Magharib B walivyoleta mabadiliko na maendeleo kwenye shehia zao.

MPANG0 MKAKATI JUMUISHI WA JINSIA KATIKA MICHEZO UTEKELEZAJI WAKE UZINGATIWE.