WAANDISHI TUMIENI KALAMU ZENU TUPATE SHERIA MPYA HABARI

NA MARYAM SALUM
AFISA Programu na mchechemuzi wa mapitio ya sheria za habari Zanzibar, Zaina Abdulla Mzee amewataka waandishi wa habari Kisiwani Pemba kutumia kalamu zao vizuri kuendelea kutilia mkazo upatikanaji wa sheria mpya ya habari  itakayosaidia tasnia ya habari Zanzibar. 
Ameyasema hayo wakati akifungua mafunzo ya ukumbusho wa hizo, kwa waandishi wa vyombo mbali mbali Kisiwani humo, ambayo yalifanyika katika Ofisi ndogo ya TAMWA iliyopo Mkanjuni Chake Chake.
Afisa huyo alisema kuwa waandishi wa habari ndio wahusika wakubwa wa sheria hiyo mpya, hivyo wanaowajibu mkubwa kwao kutoa sauti zao sambamba na kuandika yale ,adhara mbali mbali ambayo yapo kwenye sheria zilizopo kwa sasa.
Ameeleza kuwa mchakato mzima wa upatikanaji wa sheria hiyuo mpya, umekuwa ukionekana ni wakusuasua, hivyo kama waandishi wenye kiu ya sheria ambayo itakuwa rafiki kwao ni vyema kiutumia kalamu zao, kupiga debe mchakato huo ili iweze kupatikana.
Alifahamisha kuwa wanahabari wanao uwezo wakusema kwa sauti ya kipekee itakayofanya kufanyiwa haraka mchakato wa kupatikana kwa sheria hiyo mpya,kwa kuandika makala mbali mbali, vipindi vya redi na television, pamoja na kuzielezea zile changamoto za sheria ambazo zinatumika kwa sasa hivi,amesema.
Mapema mkufunzi mshauri Bi Haure Shamte wakati akiwasilosha kifungu cha sheria ya Mgazeti, Vitabu na Mawakala wa Habari na,bari 5 ya mwaka 1988 na ile ya Utangazaji nambari 7 ya mwaka 1977, kwenye vifungu kandamizi, amesema kuwa bado vinahitaji ku[ogiwa kelele kwa namna yoyote ile kwa maslahi ya taifa.
Wakati akivitaja viofungu hivyo ambavyo ni kandamizi kwenye tasnia ya habari kupotia sheria ya Magazeti, Vitabu, na Mawakala wa Habari nambari 5 ya mwaka 1988, ameeeleza kuwa kifungu cha 27 kinachompa mamlaka  ama uwezo ofisa wa polisi kukamata Gazeti.
Wakati huo huo alikitaja kifungu cha 39, ambacho kimaelezaea sharti la kuusanya na ,kutoa habari na viofaa vya habari, ambapo uauzi wa Waziri wa kukataa kutoa kibali, haukatiwi rufaa.
Nao wanahabari hao wakati wakiwasilisha kazi zao za vikundi wamesema kuwa kuna haja kwao kuhakikisha wanafanya juhudi za kuona sheria mpya na rafiki kwao kwenye tasnia yao inapatikana Zanzibar.
Nae mwandishi wa habari wa redio jamii Mkoani Khadija Ali Yussuf na Fatma Hamad Faki mwandishi wa mtandao wa Plog ya Pemba ya Leo, walisema kuwa kutokana na uwezo aliopewa ofisa Polisi kuweza kuingia na kupekuwa kwenye majengo ya habari, ni moja wapo kwa waandishi wa habari kunyimwa uhuru wa tasnia yao.
Aidha  walisema kuwa wakati umefika kwa sasa kwa waandishi wa habari Zanzibar kupatiwa sheris mpya ya habari ambayo itaweza kuimarsha utawala mzima wa kisheria.
Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake TAMWA, Zanzibar hatua kwa hatua itahakikisha inaendelea kuwajengea uwezo zaidi waandishi wa habari ili waweze kuandika taarifa mbalimbali zitakazo saidia kupatika kwa sheria mpya ya habari  Zanzibar.
MWISHO.

Comments

Popular posts from this blog

BAJAJI WAMLILIA RAIS DK MWINYI PEMBA ,WAOMBA MSAADA KWAKWE WASEMA WAMECHOSHWA NA HILI KUTOKA MAWASILIANO

Masheha wanawake wa Wilaya ya Magharib B walivyoleta mabadiliko na maendeleo kwenye shehia zao.

MPANG0 MKAKATI JUMUISHI WA JINSIA KATIKA MICHEZO UTEKELEZAJI WAKE UZINGATIWE.