CHADEMA ZANZIBAR YATUMA NENO KWA VIONGOZI

Na,Amina Ahmed Moh'd Pemba.

MAKAMU  Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Said Issa Moh`d amelitaka Bazara la viongozi wa chama hicho kanda ya Pemba kufanya kazi kubwa wa kukipambania chama hicho ili kiweze kushinda katika nafasi mbali mbali za uongozi kisiwani humo katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.

Amesema chama hicho kwa sasa kimekuwa kikiendelea kuimarika kila kukicha na kupata uungwaji mkono kutoka kwa wananchi hasa vijana, hivyo viongozi hao wakiendelea kufanya kazi nzuri nafasi ya kushinda katika uchaguzi mkuu wa mwakani ipo wazi.Issa ameyasema hayo leo alipokuwa akizungumza na viongozi wa Bazara hilo kanda ya Pemba katika mkutano mkuu wa kanda ulioambana na uchaguzi wa kuwachagua viongozi wa kanda hiyo uliofanyika huko  Hifadhi Hotel Tibirinzi Chake Chake.
Amesema baada ya muda mrefu wa kupambana na kukijenga chama hicho hapa visiwani Zanzibar sasa kina fursa ya kusimamia wagombea katika nafasi mbali mbali na kushindwa kwani tayari kimekubalika kwa wananchi ukilinganisha na ilivyokuwa kipindi cha nyuma.

Amesisitiza juu ya umuhimu wa wajumbe wa mkutano huo kuchagua vuiongozi kwa misingi ya sifa zao na wasifanye maamuzi ya kuchagua kwa shinikizo kwani kunaweza kukigawa chama hicho na kurejesha nyuma mipango na mikakati ya kukipatia ushindi Chadema katika uchaguzi huo.
Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) Salum Mwalim Juma amesema kuwa chama hicho kimepiga hatua kubwa kisiwani Pemba kwani kwa sasa imesimamisha jumla ya matawi 120 kwa kanda ya Pemba.
Amesema katika matawi hayo 120 matawi 115 yameshakabilisha uchaguzi na kupata viongozi wake, huku akieleza kuwa mafanikio hayo yametokana kazi kubwa iliyofanya na viongozi wa kanda hiyo kwa kuwa na moyo wa kujitolea na mashirikiano makubwa.
Katibu wa Kanda ya Pemba Chadema pamoja na kutoa shukurani zake za dhati kwa Mwenyekiti wa chadema kanda hiyo aliyemaliza muda wake amewasisitiza wajumbe kuchagua mrithi wa Mwenyekiti huyo atakayeendeleza mambo makubwa aliyoyasimamia wakati wake, pamoja na kuwataka kuendeleza umoja baada ya uchaguzi huo.

Comments

Popular posts from this blog

BARABARA 19 KUJENGWA KWA KIWANGO CHA LAMI PEMBA KUKAMILIKA DISEMBA 2024.

WAZAZI ZIDISHENI KUFUATILIA NYENENDO ZA WATOTO HUSUSAN NI VIJANA .

UONGOZI WA WILAYA CHAKE CHAKE KFHI WAPONGEZA JUHUDI