KIKUNDI CHA TUPENDANE AMBACHO NI CHA WATU WENYE MAHITAJI MAALUM WAOMBA KUKAMILISHIWA UJENZI WA OFISI YAO.
Na AMINA AHMED MOH’D KIKUNDI Cha Tupendane Mkoa wa Kaskazini Pemba Wameiomba Serikali na pamoja na wadau Kuwasaidia kukamilisha ujenzi wa Eneo ambalo litakapokamilika wataweza kulitumia kwajili ya Shughuli wanazofanya za kimaendeleo na kuongeza idadi ya uzalishaji wa bidhaa. Aliyasema hayo katibu wa kikundi hicho Time Juma Said Alipokuwa akizungumza na habari hizi huko katika ofisi za kikundi hicho wilaya Micheweni Shehia ya Majenzi ambapo kwa sasa wanaendelea kufanya shughuli zao za Ususi na Ufumaji. Alisema kutokana na wanakikundi hao asilimia 60 kuwa na ulemavu wa uoni Suala la kukosa ofisi hupeekea kusua sua kufanya shuhguli zao na wanapofanya hupelekea kubaki nazo nyumbani jambo ambalo linarudisha nyuma Juhudi zao za kutaka kujikomboa kiuchumi. "Tunaiomba Serikali wadau pia Watusaidie kumalizia ujenzi wa ofisi yetu sisi w...